Mgomo wa daladala na bajaji Arusha wamng'oa Mwakalebela wa LATRA Arusha

Bushmamy

JF-Expert Member
Aug 18, 2019
8,848
15,253
Migomo ya daladala na Bajaji a inayoendelea bila kupatiwa ufumbuzi katika jiji la Arusha,imetajwa kumg'oa aliyekuwa ofisa wa LATRA mkoa wa Arusha Amani Mwakalebela baada ya kushindwa kutatua migogoro hiyo na kusababisha usumbufu kwa wanchi ,wafanyabiashara na wanafunzi kukosa usafiri.

Kuhusu mgomo, zaidi soma
Arusha: Daladala zagoma tena Arusha, leo Agosti 14, 2023

Mwakalebela amepata uhamisho wa ghafla wakati bado sakata la mgomo wa daladala halijapoa huku mkuu wa mkoa wa Arusha John Mongela akiwa ameunda kamati ya usuluhishi juu ya mgogoro huo na kuja na majibu.

Leo Jumatatu wakati ofisa mpya Mwandamizi wa LATRA JOSEPH Michael akitinga ofisini rasmi kuchukua nafasi ya Mwakalebela, daladala zimegoma tena na kusababisha adha kwa wananchi.

Akiongea na vyombo vya habari ,Michael aliwataka wamiliki wa daladala katika jiji la Arusha, kusitisha mgomo wao mara moja na kurejesha usarifi kwa kuwa mamlaka hiyo imeanz kutekeleza maoni ya kamati iliyoindwa na mkuu wa mkoa .

Alisema iwapo daladala zitaendelea na msimamo wakutotii mamlaka ya kuwataka wasitishe mgono mara moja,LATRA itafuta leseni zao mara moja kama sheria inavyotaka.

"Mimi nimeingia ofisini Leo jana tulikutana na viongozi wa vyombo vyabusafirishaji kwa lengo la kujitambulisha kama afisa moya wa LATRA, na Leo nimejaribu kuzungukia baadhi ya maeneo ikiwemo ruti za daladala zaidi ya 145 ,mimi na wenzangu tupo katika hatua ya kutekeleza maoni ya kamati hiyo "

Kuhusu ofisa aliyekuwepo kuondolewa ghafla katika kituo chake cha kazi mkoani Arusha, alisema ni uhamisho wa kawaida haihusiani na mgogoro wa daladala na bajaj.
 
Madereva wa Dar tu hesabu hazifiki, sembuse arusha wala sio kweli bajaji zinamaliza abiria ni Upepo mbaya tu saivi kila mahali.

Biashara haziendi watu pesa hawana wala wasitake tafuta pakuangushia lawama zao.

Solution ni 1 tu anae ona bajaji inamaliza abiria arudshe gari kwa bosi aje aombe bajaji apewe atafute abiria.
 
Kazi ya Daladala Arusha ni Asubuhi Hadi saa tatu na Jioni kuanzia saa tisa. Hapo mchana hamna mtu atakaa kwenye daladala lisaa limoja asubiri ijae.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom