Lazima Lowassa ashitakiwe kwa Ufisadi!!

Lazima Lowassa ashitakiwe kwa Ufisadi!!

Huu uzi unachonganisha,iwapo lowasa atapelekwa mahakamani,ile kauli tata ya kuwalinda wazee itatenguliwa na mengi yataibuka,uzi huu utakuwa umeandaliwa kuwaibua wazee waliahidiwa na jpm kuwa wako salama atawalinda.
 
Kwakuwa wakati Lowasa akiwa CCM wana CHADEMA wote walituaminisha ni fisadi

Na alipohama CCM wana CCM wote akiwepo Magufili wamekuwa wakisema majizi na mafisadi wamehamia CHADEMA

Basi naomba mahakama ikianza kazi awe mtu wa kwanza kushtakiwa maana ndo fisadi ambaye kila mtu amekuwa akimtia kama mfano

ukitaka kujua magu mdogo sana kwa luwasa, ajarbu aone moto. labda mahakama hio iwe na uwanja wa karate atakaeshindwa anaenda segerea
 
Hakuna mtu yeyote nchi hii ana uwezo wa kumgusa Lowasa.
Walishindwa kumgusa mshona viatu Lugumi watamuweza mtu aliekuwepo kwenye system toka akiwa kijana?
 
Natetemeka kivipi!!?
Nina uhakika Lowassa fisadi tena bila chenga
Na awamu hii lazima asage meno
Mbona mnachelewa?Nakuhakikishia miaka 5 itakatika huyo lowassa hajafikishwa mahakamani
 
Nalipa kodi na ni mpiga kura pi!!
moron kama wewe una ajenda yako ya siri kama wewe mtanzania halisi vipi kuhusu Buzwagi.Meremeta,,MV Kigamboni.Nyumba za serikali..Escrow .Mabehewa feki.Rada .Idiot mkubwa
 
Kiashiria cha udhaifu kwa binadamu wakati mwingine ni pale anaposhindwa kulifikisha mwisho jambo la muhimu analotakiwa kulikamilisha. Sisi kama taifa tumekuwa tunatangatanga na Jambo lililosababishwa na mtu mmoja tu na sisi kama taifa tumeshindwa kufikia mwisho wake.

Tarehe 7/2/2008 aliyekuwa Waziri wa Mkuu wa Tanzania wakati ule, Edward Ngoyai Lowassa alijiuzulu wadhifa wake baada ya kutuhumiwa kuingilia mchakato wa Zabuni ya Ufuaji Umeme iliyosababisha kuletwa kwa Kampuni ya Ufuaji Umeme ya Richmond nchini. Tangu kujiuzulu kwa Lowassa mpaka sasa imeshapita miaka zaidi ya 8 na miezi kadhaa, lakini bado suala la sakata la Richmond halijaisha

Mitambo iliyoletwa na Kampuni ya Richmond ambayo bado ipo Pale Pale ilipofungwa na Kampuni ya Richmond, imeshabadilishwa umiliki wake mara mbili. Imetoka kwa Richmond ikanunuliwa na Dowans na sasa inamilikiwa na Kampuni ya Symbion ya Marekani. Lakini sisi kama taifa tumeachwa pale pale tulipokuwa Mwaka 2008.

Kwa kuwa kuna Mahakama ya Mafisadi inaundwa na sisi kama taifa tunayumbishwa na suala la mtu mmoja tu, ambaye si kiongozi wa serikali kwa sasa, nashauri Kesi ya Kwanza kwenye Mahakama ya Mafisadi iwe ni hii ya "Ufisadi" wa Edward Ngoyai Lowassa kuhusu Ufisadi wa zabuni ya ufuaji umeme iliyosababisha Sakata la richmond.

Ni lazima Lowassa ashitakiwe ili kama yeye anao ushahidi tofauti na ule ambao wapinzani wake wanao aje nao mahakamani ili upimwe kwenye mizani ya kisheria tujue nani mkweli kati yake yeye na wapinzani wake.

Haiwezekani mitambo ile iliyoletwa na Kampuni (Feki?) ya Richmond bado ipo nchini mwetu, inafua umeme, Tannesco wanalipa Capacity charges tanesco wanauziwa umeme kutokana na mitambo ile ile iliyokuwa ya Richmond, mkataba ule ule wa kati ya Richmond na Tannesco ndiyo umekuwa ukihuhishwa na Dowans na sasa Symbion, lakini sisi kama taifa bado tunakumbushana mambo ya mwaka 2008.

Kuukata Mzizi wa fitina ni lazima Lowassa na kama wapo na wengine waliohusika na sakata la Richmond wafikishwe kwenye Mahakama ya mafisadi mara tu Mahakama hiyo itakapoanza kazi. Tunataka Kesi ya kwanza kwenye mahakama hiyo iwe dhidi ya Lowassa na wenzake waliohusika na suala la Richmond.

KESI YA LOWASSA ISIPOKUWA YA KWANZA KWENYE MAHAKAMA YA MAFISADI NITASHANGAA KWELI KWELI!!

Lowassa hawezi kushitakiwa bila Kikwete. Kikwete alimusafisha Lowassa, akasema hana makosa, kwa hiyo huwezi kusema ashitakiwe bila Kikwete, sheria haiendi hivyo.
 
Mi nilisha apa kuwa lowasa asipopelekwa mahkaman sitaipigia CCM kura kuanzia mwenyekit had Raic.

H
 
Tafsiri ya ulichokiwasilisha likely ni hiki;

Kama kampuni ya Richmond ilikuwa ya mfukoni isiyo na ofisi wala uwezo, mbona mpaka leo hii mitambo yake imetoka kuwa ya Richmond > Dowans > Symbion inazalisha umeme na TANESCO inanunua na capacity charge inalipwa??

......Hili haliwezekani, ni lazima Edward Ngoyai Lowassa ni fisadi kupindukia na chanzo cha matatizo yote ya wa - Bongo woote na sharti awe wa kwanza kusimama kwenye kizimba cha mahakama ya mafisadi wa Magufuli!!
 
Back
Top Bottom