Lazima Lowassa ashitakiwe kwa Ufisadi!!

Lazima Lowassa ashitakiwe kwa Ufisadi!!

Ndugu yangu hivi unamtakia nini Mheshimiwa mstaafu JK ??? unadhani uliyo yaandika hapa viongozi wa ccm wanayafurahia....shauri yako.
Kwa nini wasiyafurahie wakati ni wao walianzisha mahakama ya Mafisadi na wanasema Lowassa ndiye fisadi mkubwa nchini na CHADEMA walikosea kumpokea?
 
Mimi mwenyewe nimeshachoka na kelele Lowasa ni Fisadi bla bla wampeleke sasa mahakamani wakathibitishe ufisadi wa Lowasa ,

Ukistaajabu ya Musa ya Firauni sijui yatakuaje ,wizi wa Escorow ni mara mbili ya Richmond lakini hili limepita tayari kana kwamba hamna kilichotokea

Lowasa alikua waziri mkuu wa Tanzania na sio Tanganyika
Unajua hawawezi kumpeleka mahakamani kwasababu Magu kaapa kuwalinda marais wastaafu!Hebu jiulize,ni mwanaccm yupi ambaye alikuwa baraza la mawaziri wakati Lowassa akiwa PM aliyetoka hadharani na kusema Richmond ni ya Lowassa?Hakuna,ndio maana hata Magu hajawahi mtuhumu lowassa kwa jina kuwa ni fisadi,hata wakati wa kampeni!Unajua Lowassa akifikishwa mahakamani kiapo cha kutunza siri kinabatilishwa na mashahidi ambao bila shaka watakuwa mawaziri wa kipindi hicho itabidi viapo vyao vibatilishwe akiwemo Magu mwenyewe ili watoe ushahidi mahakamani!Hapo ndio picha itaungua,hata ile "maelekezo toka juu" itakuwa sehemu ya ushahidi wataotakiwa kuuthibitisha waliokuwa mawaziri!
Swali gumu litakuwa,Je,ni kweli lowassa hakutaka kusain mkataba ule?Je,taarifa ya maelekezo toka mamlaka ya juu yaliwalazisha wao kama mawaziri kubadili uelekeo na kusaini mkataba,chini ya viapo itawabidi waseme ukweli!
Kama ukweli uko in favour of lowassa,kwanin wajipalie mkaa kwa kumpeleka mahakamani na uozo uwekwe wazi!
Kama ukweli hauko in favour of lowassa basi serikali itakimbia(ingeshakuwa imekimbia) mahakamani ili kujijengea taswira mpya kwenye macho ya watanzania!

NB:Serikali mkishindwa kumfikisha mahakamani,tell your people to shut up!Hatuwezi kuwa watu wa kuimbiwa fulani fisadi fisadi ila mtu anapeta tu kitaa!
 
Kwa nini wasiyafurahie wakati ni wao walianzisha mahakama ya Mafisadi na wanasema Lowassa ndiye fisadi mkubwa nchini na CHADEMA walikosea kumpokea?
Mi naisubiri kwa hamu hiyo mahakama ya mafisadi...ili uchaguzi wa mwaka 2020 unoge vizuri....
 
Kuna mijitu ya hovyo sana humu ndani!

Motochini

Lizabon

Yehodaya

Faizafoxy

Etl

Jamani samahani Le Mutuz yuko wapi?

Toka mama yake atumbuliwe sijawahi kumuona humu jamvin
 
Nchi niyetu sote, hakuna haja yakunyosheana kidore, nakama niufisadi nani asiyefisad,tujege nchi upya kwa kufuta sheria siyo kwa kuagaria yario pita,ferix kayungiro
 
Hakuna kiongozi wa CCM anayeweza kufanya hili..Huyu mtu namkubali sana,hiyo speech yake ilionyesha ni kiasi gani ndani ya serikali ya CCM kuna uvunjifu wa haki za kikatiba. Viva Lowasa,you will always be remembered for everything you have done in this country.
am ready to die for lowasa even though he doesn't know me and I don't benefit a penny from
 
kwangu mimi chaguo la kwanza angekua A Chenge huyu ndo tishio haswa
 
Kiashiria cha udhaifu kwa binadamu wakati mwingine ni pale anaposhindwa kulifikisha mwisho jambo la muhimu analotakiwa kulikamilisha. Sisi kama taifa tumekuwa tunatangatanga na Jambo lililosababishwa na mtu mmoja tu na sisi kama taifa tumeshindwa kufikia mwisho wake.

Tarehe 7/2/2008 aliyekuwa Waziri wa Mkuu wa Tanzania wakati ule, Edward Ngoyai Lowassa alijiuzulu wadhifa wake baada ya kutuhumiwa kuingilia mchakato wa Zabuni ya Ufuaji Umeme iliyosababisha kuletwa kwa Kampuni ya Ufuaji Umeme ya Richmond nchini. Tangu kujiuzulu kwa Lowassa mpaka sasa imeshapita miaka zaidi ya 8 na miezi kadhaa, lakini bado suala la sakata la Richmond halijaisha

Mitambo iliyoletwa na Kampuni ya Richmond ambayo bado ipo Pale Pale ilipofungwa na Kampuni ya Richmond, imeshabadilishwa umiliki wake mara mbili. Imetoka kwa Richmond ikanunuliwa na Dowans na sasa inamilikiwa na Kampuni ya Symbion ya Marekani. Lakini sisi kama taifa tumeachwa pale pale tulipokuwa Mwaka 2008.

Kwa kuwa kuna Mahakama ya Mafisadi inaundwa na sisi kama taifa tunayumbishwa na suala la mtu mmoja tu, ambaye si kiongozi wa serikali kwa sasa, nashauri Kesi ya Kwanza kwenye Mahakama ya Mafisadi iwe ni hii ya "Ufisadi" wa Edward Ngoyai Lowassa kuhusu Ufisadi wa zabuni ya ufuaji umeme iliyosababisha Sakata la richmond.

Ni lazima Lowassa ashitakiwe ili kama yeye anao ushahidi tofauti na ule ambao wapinzani wake wanao aje nao mahakamani ili upimwe kwenye mizani ya kisheria tujue nani mkweli kati yake yeye na wapinzani wake.

Haiwezekani mitambo ile iliyoletwa na Kampuni (Feki?) ya Richmond bado ipo nchini mwetu, inafua umeme, Tannesco wanalipa Capacity charges tanesco wanauziwa umeme kutokana na mitambo ile ile iliyokuwa ya Richmond, mkataba ule ule wa kati ya Richmond na Tannesco ndiyo umekuwa ukihuhishwa na Dowans na sasa Symbion, lakini sisi kama taifa bado tunakumbushana mambo ya mwaka 2008.

Kuukata Mzizi wa fitina ni lazima Lowassa na kama wapo na wengine waliohusika na sakata la Richmond wafikishwe kwenye Mahakama ya mafisadi mara tu Mahakama hiyo itakapoanza kazi. Tunataka Kesi ya kwanza kwenye mahakama hiyo iwe dhidi ya Lowassa na wenzake waliohusika na suala la Richmond.

KESI YA LOWASSA ISIPOKUWA YA KWANZA KWENYE MAHAKAMA YA MAFISADI NITASHANGAA KWELI KWELI!!
Kama Kuna jeuri hiyo waanze na kikwete,riz1,chenge, mkapa, kitwamga na waziri wa zamani wa miundombinu
 
Mimi naunga mkono hoja ndugu Allen..lowasa m moja tu hawezi kulihangaisha taifa....apelekwe mahakamani
 
Mimi naunga mkono hoja ndugu Allen..lowasa m moja tu hawezi kulihangaisha taifa....apelekwe mahakamani
Si kila siku tunatoa matamko, basi hata kesho litolewe tamko la kumfikisha Lowassa mhakamani!!
 
Ni vizuri hiyo mahakama ikaanzishwa mapema sana. Hii itatuondelea sintofahamu ya maufisadi makubwa hapa nchini kama RICHMOND, ESCROW, KAGODA, MEREMETA, MAJENGO PACHA, MV BAGAMOYO, nk, nk.

Na iwafunge jela kwelikweli na kuwafilisi wahusika; kwakua itahukumu wote (naamini kwa haki kabisa) sitajali kama ni raisi wa moyo wangu Lowassa au mwingine yeyote yule, kama umeliibia taifa, umewaibia wananchi wanyonge hukumu ikihusu. Bahati nzuri mafisadi wengi wapo upande ulee, msumeno ukate pande zote!!

I
 
Back
Top Bottom