Lazima Lowassa ashitakiwe kwa Ufisadi!!

Lazima Lowassa ashitakiwe kwa Ufisadi!!

Alishasema mumpeleke tangu 2014.But no one dare to do that. You never know who are in the chain. So nyamaza.
 
1478154751994.jpg
 
Kiashiria cha udhaifu kwa binadamu wakati mwingine ni pale anaposhindwa kulifikisha mwisho jambo la muhimu analotakiwa kulikamilisha. Sisi kama taifa tumekuwa tunatangatanga na Jambo lililosababishwa na mtu mmoja tu na sisi kama taifa tumeshindwa kufikia mwisho wake.

Tarehe 7/2/2008 aliyekuwa Waziri wa Mkuu wa Tanzania wakati ule, Edward Ngoyai Lowassa alijiuzulu wadhifa wake baada ya kutuhumiwa kuingilia mchakato wa Zabuni ya Ufuaji Umeme iliyosababisha kuletwa kwa Kampuni ya Ufuaji Umeme ya Richmond nchini. Tangu kujiuzulu kwa Lowassa mpaka sasa imeshapita miaka zaidi ya 8 na miezi kadhaa, lakini bado suala la sakata la Richmond halijaisha

Mitambo iliyoletwa na Kampuni ya Richmond ambayo bado ipo Pale Pale ilipofungwa na Kampuni ya Richmond, imeshabadilishwa umiliki wake mara mbili. Imetoka kwa Richmond ikanunuliwa na Dowans na sasa inamilikiwa na Kampuni ya Symbion ya Marekani. Lakini sisi kama taifa tumeachwa pale pale tulipokuwa Mwaka 2008.

Kwa kuwa kuna Mahakama ya Mafisadi inaundwa na sisi kama taifa tunayumbishwa na suala la mtu mmoja tu, ambaye si kiongozi wa serikali kwa sasa, nashauri Kesi ya Kwanza kwenye Mahakama ya Mafisadi iwe ni hii ya "Ufisadi" wa Edward Ngoyai Lowassa kuhusu Ufisadi wa zabuni ya ufuaji umeme iliyosababisha Sakata la richmond.

Ni lazima Lowassa ashitakiwe ili kama yeye anao ushahidi tofauti na ule ambao wapinzani wake wanao aje nao mahakamani ili upimwe kwenye mizani ya kisheria tujue nani mkweli kati yake yeye na wapinzani wake.

Haiwezekani mitambo ile iliyoletwa na Kampuni (Feki?) ya Richmond bado ipo nchini mwetu, inafua umeme, Tannesco wanalipa Capacity charges tanesco wanauziwa umeme kutokana na mitambo ile ile iliyokuwa ya Richmond, mkataba ule ule wa kati ya Richmond na Tannesco ndiyo umekuwa ukihuhishwa na Dowans na sasa Symbion, lakini sisi kama taifa bado tunakumbushana mambo ya mwaka 2008.

Kuukata Mzizi wa fitina ni lazima Lowassa na kama wapo na wengine waliohusika na sakata la Richmond wafikishwe kwenye Mahakama ya mafisadi mara tu Mahakama hiyo itakapoanza kazi. Tunataka Kesi ya kwanza kwenye mahakama hiyo iwe dhidi ya Lowassa na wenzake waliohusika na suala la Richmond.

KESI YA LOWASSA ISIPOKUWA YA KWANZA KWENYE MAHAKAMA YA MAFISADI NITASHANGAA KWELI KWELI!!
Umeambiwa mafisadi have vanished on thin air
 
Hivi mbona watu tunajiondoa fahamu zetu na kujifanya hatujui baadhi ya mambo ambayo yapo wazi kwa sababu tu ya chuki za kisiasa. Ni jambo lililo wazi kuwa no vigumu kwa waziri kuingia mikataba mikubwa ya kimataifa peke yake bila bosi wake kujua na kukubaliana nayo...isitoshe waziri mkuu ni mtendaji mkuu wa serikali hivyo kitendo cha kumwishtaki ni kuishtaki hadi bosi wake....ikitokea kama alipokea maagizo na shinikizo toka juu nini kitatokea kama si kuivuruga nchi...shutuma nyingine zipo kiitikadi na chuki binafsi za kisiasa tu.(sina maana ya kuutetea uhujumu na ufisadi ndani ya nchi yetu).
 
Yaani bado mna akili zile zile za kitoto kung'ang'ania vitu visivyowezekana, hambadiliki?
Tafuteni mambo mengine ya kuwaza, iwe kweli kwamba Lowassa ana hatia au isiwe kweli hakuna kesi za ufisadi wala vita dhidi ya ufisadi hapa Tanzania.
Acheni kuleweshwa kijinga na makelele ya wanasiasa wa Kitanzania.
Nadhani mmeshasikia kwamba mahakama yao walioianzisha sasa imekumbwa na uhaba si wa vitendea kazi bali wa kesi halafu bado mnaleta hizi habari mfu.
Fanyeni mengine siyo haya.
 
Afadhali sasa mahakama ya mafisadi imeshaanza kufanya kazi. Ila nimesikitika sana mtu wa kwanza kushitakiwa siyo Lowassa.
hakuna wakupeleka pua yake kwa Lowasa ,na mpaka 2020 kama hajapelekwa kwa hiyo mahakama ya mafisadi hakuna wa kumzuia kuingia ikulu
 
Back
Top Bottom