Lazima Lowassa ashitakiwe kwa Ufisadi!!

Lazima Lowassa ashitakiwe kwa Ufisadi!!

Nani ampeleke EL mahakamani? Halafu asimamiwe na mawakili wasomi akina Lissu,Kibatala, Malya?Itabidi wajenge magereza karibu na Jakaya Kikwete Heart Institute.Richmond ni mtego wa panya. Labda wamwombe awe shahidi (kama walivyomwomba Mh Kibatala) siyo mshtakiwa namba moja.
 
Nakushukuru mheshimiwa Spika kwa kunifanya msemaji wa kwanza katika hoja hii. Lakini la pili nimpongeze Dr. Harrison Mwakyembe Mwenyekiti wa Kamati teule,kwa kuwasilisha kwa mbwembwe nyingi sana taarifa yake, mbwembwe zilikuwa nzuri sana.Kwa kazi nzuri kwa maoni yao na wameiwasilisha vizuri.Lakini Mheshimiwa Spika, nimesimama kuweka kwenye Kumbukumbu kutokuridhika kwangu na jinsi kazi hiyo ilivyofanywa.

Mhesimiwa Dr. Harrison Mwakyembe ni mwanasheria tena daktari alikuwa anafundisha wanafunzi Chuo Kikuu. Moja ya vitu alivyokuwa anafundisha ni Natural justice. Wewe pia Mheshimiwa Spika ni Mwanasheria, unafahamu suala la Natural Justice. Kwamba katika Kamati Teule, imesikiliza watu wengine wote, pamoja na waliowaita minong’ono ya mitaani. Wamesafiri mpaka Marekani kutafuta mashahidi, lakini mimi ambaye ni mmoja katika watuhumiwa mle hawakunihoji hata siku moja!

Mheshimiwa Spika. Nimesimama kueleza masikitiko yangu. Ofisi ya bunge mpaka ofisini kwangu hata wangeniita ningeenda kwa mguu kama hamna gari. Na nilikuwa tayari kufanya hivyo.Hawa ni watu makini sana, siwezi kuamini kwamba wanaweza kufanya Oversight kama hiyo. Kwa sababu katika kila hoja walizojenga, walisema Waziri Mkuu ilikuwa hivi, kulikuwa na shida gani kuja kuniuliza, Waziri Mkuu wanasema ulitoa dokezo hili ni sawa sawa ni kweli? Kulikuwa na shida gani kwa mfano Mheshimiwa Spika, kufuata utaratibu wa Westminster kuthibitisha hapo unaposema, wenye Richmond nifulani uka- table Record na ushahidi kwamba ni fulani.

Mheshimiwa Spika Taifa letu ni taifa changa, lakini chombo hiki ndiyo mahali pa Demokrasia pa kubwa katika nchi yetu pote, hapa ndipo penyewe. Kama katika chombo hiki haki haitaonekana kutendendeka, Mheshimiwa Spika nchi haitakwenda vizuri.

Hapa ndipo tunategemewa kuonyesha umakini, umahiri wetu katika mambo ya Demokrasia. Kwa hiyo nilichofanyiwa Mheshimiwa Spika napenda kuweka kumbukumbu sahihi…sawa. Kwamba naona si sahihi, na nimefadhaika sana, nimedhalilishwa sana na nimeonewa sana katika hili. Maana zimechukuliwa tuhuma zikaja kuelezwa hapa kwamba hivi ndivyo ilivyo, mimi sijaulizwa. Kulikuwa na shida gani kuniuliza. Kwa nini muamini minong’ono ya mitaani kuliko maelezo yangu?

Sisi wote hapa ni wanasiasa, tukianza kuamini minong’ono ya mitaani, niambieni mwanasiasa atakayesimama. Hatuwezi… Tume wamepewa muda wa kutosha kabisa, lakini inashindwa kumuona mtu ambaye wanamtuhumu na wanamsema kwa kirefu sana.

Lakini mheshimiwa Spika, hata pale uliponinong’oneza ukaniambia “una ushahidi wowote”? Nilikupa ushahidi huo wa maandishi. Katika taarifa yao hakuna hata moja ya ushahidi ambao umetoka Ofisi ya Waziri Mkuu, hata mmoja! Lakini kitabu cha Majedwali kimejaa majedwali meengi pamoja na Magazeti mpaka ya Udaku, lakini maelezo ya Waziri Mkuu hakuna hata moja.

Mheshimiwa Spika. Mimi naamini ingekuwa ni heshima wangeliweka halafu wakasema tunakataa kitambulisho hiki kwa sababu hii na hii na hii na hii. Mimi nadhani ingejengwa hoja. Lakini kujenga hoja na kuja hapa bungeni, tunahutubia nchi nzima na kusema Waziri Mkuu amefanya hiki, amefanya hiki, amefanya hiki bila kumsikiliza, nachelea kuuliza, hivi watu wa chini itakuwaje?

Lakini Mheshimiwa Spika nimetafakari kwa makini sana jambo hili, nikajiuliza, hivi hasa kulikoni. Mpaka watu wazima wenye uwezo wao, watu maarufu, wenye heshima zao. Mpaka wafike mahali waache jambo la msingi kama hilo, kulikoni?

Mimi nadhani, they have a wish which I am going to grant, ni Uwaziri Mkuu. Nadhani tatizo ni Uwaziri Mkuu. Kwamba ionekane Waziri Mkuu ndiye amefanya haya, ionekane Waziri Mkuu amefanya haya, tumuondolee heshima au tumwajibishe. Mheshimiwa Spika. Nimetafakari sana, kwa niaba ya chama changu, kwa niaba ya serikali yangu, nimeamua kumwandikia Rais barua ya kumwomba niachie ngazi.

Nafanya hivyo kwa moyo mweupe kabisa, kwa moyo mweupe kabisa ili kuonyesha dhana ya uwajibikaji lakini na kutokukubaliana na utaratibu uliotumika kusema uongo ndani ya bunge wa kunisingizia.

Mheshimiwa Spika nitumie nafasi hii kumshukuru sana Rais kwa heshima aliyonipa ya kutumikia nchi hii kwa Uwaziri Mkuu kwa miaka miwili, namshukuru sana mheshimiwa Rais. Nakushukuru wewe, nawashukuru Mawaziri na Manaibu Mawaziri, nawashukuru waheshimiwa Wabunge, na wanachama wa CCM tuliosimamia Ilani ya Uchaguzi ya Chama chama Mapinduzi. Baada kusema hayo nakushukuru Mheshimwa.
 
Allen Kilewella uko sahihi kabisa mkuu tumeshachoka hizi kelele za siku kuhusu Lowasa tunataka kuona ashtakiwa kwenye mahakama ya mafisadi na sheria kuchukua mkondo wake kama hana hatia au hana uamuzi utatolewa na mahakamani.
 
Kuna watu wanataka hii hotuba hivyo nimeiweka tena. Kumetokea matatizo ya kiufundi ambayo yapo nje ya uwezo wangu yaliyoiondoa pale ilipokuwa mapema!!
 
Kwa upuuzi wa ccm, Lowassa yupo salama pamoja na tuhuma zake.
 
Umepoteza Kumbukumbu, alieleta msamiati wa Fisadi Papa kwa mara ya Kwanza ni Reginald Abraham Mengi akiwata Wahindi watano Rostam Azizi, Somaiya, Jeetu patel, Somaiya na Yusuf Mehboob Manji kuwa ndio Mafisadi wakubwa zaidi wanaoharibu nchi.

Lakini Baada ya Chombo kwenda mrama na Lowassa kuhamia Chadema Reginald Mengi na Rostam wakawa kwny Timu ya Kampeni ya Lowassa na bifu likaisha na hatimae List of shame ikaondolewa kwny tovuti ya Chama na tabia ya kutaja taja jina la Rostam kama Fisadi ikakoma kabisa
hizo zote porojo...jamhuri impeleke mahakamani fisadi lowasa. ...haraka sana
 
hizo zote porojo...jamhuri impeleke mahakamani fisadi lowasa. ...haraka sana
Mkikumbushwa historia ya matamko yenu mnaita porojo. Muwe mnaweka akiba ya maneno sio mnaropoka baadae tukiwakumbusha mnaita Porojo
 
Nashukura Mkuu. Nashangaa wanaokesha kila siku kumwita Lowassa fisadi siwaoni humu wakishabikia apelekwe mahakamani kasoro MOTOCHINI ambaye naye alisema apelekwe huku akitetemeka!!
Nashukura Mkuu. Nashangaa wanaokesha kila siku kumwita Lowassa fisadi siwaoni humu wakishabikia apelekwe mahakamani kasoro MOTOCHINI ambaye naye alisema apelekwe huku akitetemeka!!

Natetemeka kivipi!!?
Nina uhakika Lowassa fisadi tena bila chenga
Na awamu hii lazima asage meno
 
Mkikumbushwa historia ya matamko yenu mnaita porojo. Muwe mnaweka akiba ya maneno sio mnaropoka baadae tukiwakumbusha mnaita Porojo
Hapa tunataka tuungane Lowassa afikishwe mahakamani. Au wewe mwenzetu unaonaje?
 
Kama Kuna jeuri hiyo waanze na kikwete,riz1,chenge, mkapa, kitwamga na waziri wa zamani wa miundombinu
Lugumi, Dau wa NSSF, Mwakyembe na mabehewa feki , kivuko kibovu, escrow, chenji ya Rada , chenji ya bunge la latiba, NIDA nk kumbumba Richmond ni ya kikwete .
 
Ni kweli, hata na wale jamaa wa escrow nao wakihamia chadema wapelekwe kwenye mahakama za mafisadi..
 
Natetemeka kivipi!!?
Nina uhakika Lowassa fisadi tena bila chenga
Na awamu hii lazima asage meno
Utasubiri milele Lowasa Hana kosa lolote na mwenye Richmond ni kikwete .
 
Jengo likikamilika tu waiteni wale wanasheria wenu wa serikali wamfungulie Lowasa kesi ya Richmond tuone.
 
Back
Top Bottom