Lazima Lowassa ashitakiwe kwa Ufisadi!!

Lazima Lowassa ashitakiwe kwa Ufisadi!!

Tufikilie tu hivi lowasa akishitakiwa wangapi watakua mbele yake na wangapi watakua nyuma yake...iyo kesi itaishia kusemwa kwenye vijembe tu na wale waheshimiwa wapenda mipasho...
 
Mimi nilikuwepo Kizota wewe unasikiliza hadithi za mitaani. Mwalimu aliyepata shida kuishawishi Halmashauri Kuu imwalike mwaka 1993 ndiyo awe na nguvu ya kumkataa Lowassa? Lowassa alitoa jina lake kama mkakati wa kumsaidia Kikwete kwa kuwa ni Kikwete ndiye alikuwa na ushawishi kwenye chamachao kuliko yeye, lengo likiwa akipata Kikwete na yeye atakuwa amepata!!
Acha Uongo wewe! Lowassa hakujitoa. Lowassa, John Malecela walikatwa kwa maelekezo ya Mwl na hata kwny Cabinet ya kwanza ya Mkapa 1995 Lowassa hakuwepo.
 
Acha Uongo wewe! Lowassa hakujitoa. Lowassa, John Malecela walikatwa kwa maelekezo ya Mwl na hata kwny Cabinet ya kwanza ya Mkapa 1995 Lowassa hakuwepo.
Wewe ulikuwepo Kizota au unaleta hadithi za mitaani?
 
Umesema Richmond haihisiani na List of shame nikakuuliza kashfa gani ndio ilipelekea Chadema wakaweka jina la Lowasaa kwny list of shame?
Kuvunja mkataba wa City Waters ya Uingereza na DAWASA
 
Umepoteza Kumbukumbu, alieleta msamiati wa Fisadi Papa kwa mara ya Kwanza ni Reginald Abraham Mengi akiwata Wahindi watano Rostam Azizi, Somaiya, Jeetu patel, Somaiya na Yusuf Mehboob Manji kuwa ndio Mafisadi wakubwa zaidi wanaoharibu nchi.

Lakini Baada ya Chombo kwenda mrama na Lowassa kuhamia Chadema Reginald Mengi na Rostam wakawa kwny Timu ya Kampeni ya Lowassa na bifu likaisha na hatimae List of shame ikaondolewa kwny tovuti ya Chama na tabia ya kutaja taja jina la Rostam kama Fisadi ikakoma kabisa
Uko sahihi
 
Pohamba! Hoja hapa WATANZANIA TUMECHOKA NA HADITHI ZA MIAKA NENDA RUDI- TUNATAKA LOWASSA APELEKWE MAHAKAMANI

Kila kukicha Lowassa fisadi

Lowassa hana dola na wala si mwanachama tena wa CCM

Mpelekeni mahakani watanzania wajue moja
 
Watu wenye akili timamu walishang'amua kuwa zote zilikuwa siasa za maji taka
 
Pohamba! Hoja hapa WATANZANIA TUMECHOKA NA HADITHI ZA MIAKA NENDA RUDI- TUNATAKA LOWASSA APELEKWE MAHAKAMANI

Kila kukicha Lowassa fisadi

Lowassa hana dola na wala si mwanachama tena wa CCM

Mpelekeni mahakani watanzania wajue moja
ccm wanaujua ukweli kuhusu Richmond.. katu hawawezi kumshtaki mh.Lowassa ..hilo hata magufuri analijua.. hawa mapimbi wadogo wadogo acha waendelee kujifutahisha.. Mwakyembe c ni mwanasheria? Aende yy akafungue kesi kuhusu hiyo Richmond asimtume mtu , aone atakavyoaibika asubuh tu...
 
Niliwaona wajumbe wa mkutano mkuu maalumu wa CCM watu wa ajabu na wenye uwezo mdogo tena wa kutilia mashaka kumuongelea mwanaume mwenzao tena ambaye si mwanachama

Very hopeless and shameful
 
Hotuba ya Mheshimiwa Edward Lowassa aliyotoa Bungeni wakati anajiuzulu Uwaziri Mkuu.

Nakushukuru mheshimiwa Spika kwa kunifanya msemaji wa kwanza katika hoja hii. Lakini la pili nimpongeze Dr. Harrison Mwakyembe Mwenyekiti wa Kamati teule,kwa kuwasilisha kwa mbwembwe nyingi sana taarifa yake, mbwembwe zilikuwa nzuri sana.Kwa kazi nzuri kwa maoni yao na wameiwasilisha vizuri.Lakini Mheshimiwa Spika, nimesimama kuweka kwenye Kumbukumbu kutokuridhika kwangu na jinsi kazi hiyo ilivyofanywa.

Mhesimiwa Dr. Harrison Mwakyembe ni mwanasheria tena daktari alikuwa anafundisha wanafunzi Chuo Kikuu. Moja ya vitu alivyokuwa anafundisha ni Natural justice. Wewe pia Mheshimiwa Spika ni Mwanasheria, unafahamu suala la Natural Justice. Kwamba katika Kamati Teule, imesikiliza watu wengine wote, pamoja na waliowaita minong’ono ya mitaani. Wamesafiri mpaka Marekani kutafuta mashahidi, lakini mimi ambaye ni mmoja katika watuhumiwa mle hawakunihoji hata siku moja!

Mheshimiwa Spika. Nimesimama kueleza masikitiko yangu. Ofisi ya bunge mpaka ofisini kwangu hata wangeniita ningeenda kwa mguu kama hamna gari. Na nilikuwa tayari kufanya hivyo.Hawa ni watu makini sana, siwezi kuamini kwamba wanaweza kufanya Oversight kama hiyo. Kwa sababu katika kila hoja walizojenga, walisema Waziri Mkuu ilikuwa hivi, kulikuwa na shida gani kuja kuniuliza, Waziri Mkuu wanasema ulitoa dokezo hili ni sawa sawa ni kweli? Kulikuwa na shida gani kwa mfano Mheshimiwa Spika, kufuata utaratibu wa Westminster kuthibitisha hapo unaposema, wenye Richmond ni fulani uka- table Record na ushahidi kwamba ni fulani?

Mheshimiwa Spika Taifa letu ni taifa changa, lakini chombo hiki ndiyo mahali pa Demokrasia pa kubwa katika nchi yetu pote, hapa ndipo penyewe. Kama katika chombo hiki haki haitaonekana kutendendeka, Mheshimiwa Spika nchi haitakwenda vizuri.

Hapa ndipo tunategemewa kuonyesha umakini, umahiri wetu katika mambo ya Demokrasia. Kwa hiyo nilichofanyiwa Mheshimiwa Spika napenda kuweka kumbukumbu sahihi…sawa. Kwamba naona si sahihi, na nimefadhaika sana, nimedhalilishwa sana na nimeonewa sana katika hili. Maana zimechukuliwa tuhuma zikaja kuelezwa hapa kwamba hivi ndivyo ilivyo, mimi sijaulizwa. Kulikuwa na shida gani kuniuliza. Kwa nini muamini minong’ono ya mitaani kuliko maelezo yangu?

Sisi wote hapa ni wanasiasa, tukianza kuamini minong’ono ya mitaani, niambieni mwanasiasa atakayesimama. Hatuwezi… Tume wamepewa muda wa kutosha kabisa, lakini inashindwa kumuona mtu ambaye wanamtuhumu na wanamsema kwa kirefu sana.

Lakini mheshimiwa Spika, hata pale uliponinong’oneza ukaniambia “una ushahidi wowote”? Nilikupa ushahidi huo wa maandishi. Katika taarifa yao hakuna hata moja ya ushahidi ambao umetoka Ofisi ya Waziri Mkuu, hata mmoja! Lakini kitabu cha Majedwali kimejaa majedwali meengi pamoja na Magazeti mpaka ya Udaku, lakini maelezo ya Waziri Mkuu hakuna hata moja.

Mheshimiwa Spika. Mimi naamini ingekuwa ni heshima wangeliweka halafu wakasema tunakataa kitambulisho hiki kwa sababu hii na hii na hii na hii. Mimi nadhani ingejengwa hoja. Lakini kujenga hoja na kuja hapa bungeni, tunahutubia nchi nzima na kusema Waziri Mkuu amefanya hiki, amefanya hiki, amefanya hiki bila kumsikiliza, nachelea kuuliza, hivi watu wa chini itakuwaje?

Lakini Mheshimiwa Spika nimetafakari kwa makini sana jambo hili, nikajiuliza, hivi hasa kulikoni. Mpaka watu wazima wenye uwezo wao, watu maarufu, wenye heshima zao. Mpaka wafike mahali waache jambo la msingi kama hilo, kulikoni?

Mimi nadhani, they have a wish which I am going to grant, ni Uwaziri Mkuu. Nadhani tatizo ni Uwaziri Mkuu. Kwamba ionekane Waziri Mkuu ndiye amefanya haya, ionekane Waziri Mkuu amefanya haya, tumuondolee heshima au tumwajibishe. Mheshimiwa Spika. Nimetafakari sana, kwa niaba ya chama changu, kwa niaba ya serikali yangu, nimeamua kumwandikia Rais barua ya kumwomba niachie ngazi.

Nafanya hivyo kwa moyo mweupe kabisa, kwa moyo mweupe kabisa ili kuonyesha dhana ya uwajibikaji lakini na kutokukubaliana na utaratibu uliotumika kusema uongo ndani ya bunge wa kunisingizia.

Mheshimiwa Spika nitumie nafasi hii kumshukuru sana Rais kwa heshima aliyonipa ya kutumikia nchi hii kwa Uwaziri Mkuu kwa miaka miwili, namshukuru sana mheshimiwa Rais. Nakushukuru wewe, nawashukuru Mawaziri na Manaibu Mawaziri, nawashukuru waheshimiwa Wabunge, na wanachama wa CCM tuliosimamia Ilani ya Uchaguzi ya Chama chama Mapinduzi. Baada kusema hayo nakushukuru Mheshimwa.
Ndugu yangu hivi unamtakia nini Mheshimiwa mstaafu JK ??? unadhani uliyo yaandika hapa viongozi wa ccm wanayafurahia....shauri yako.
 
Kwakuwa wakati Lowasa akiwa CCM wana CHADEMA wote walituaminisha ni fisadi

Na alipohama CCM wana CCM wote akiwepo Magufili wamekuwa wakisema majizi na mafisadi wamehamia CHADEMA

Basi naomba mahakama ikianza kazi awe mtu wa kwanza kushtakiwa maana ndo fisadi ambaye kila mtu amekuwa akimtia kama mfano
 
Mimi mwenyewe nimeshachoka na kelele Lowasa ni Fisadi bla bla wampeleke sasa mahakamani wakathibitishe ufisadi wa Lowasa ,

Ukistaajabu ya Musa ya Firauni sijui yatakuaje ,wizi wa Escorow ni mara mbili ya Richmond lakini hili limepita tayari kana kwamba hamna kilichotokea

Lowasa alikua waziri mkuu wa Tanzania na sio Tanganyika
navisiaga comments zako Che!
 
Back
Top Bottom