Lazima Lowassa ashitakiwe kwa Ufisadi!!

Lazima Lowassa ashitakiwe kwa Ufisadi!!

Kama mashine bado inaendelea ina maana ni authentc! Kwa nini muda wote wameshindwa kuiondoa?
Wale waliobeba masandarusi ya hela stambic wako wapi? Wote wachukuliwe pamoja na Lowasa!
 
Hawana uwezo wa kumpeleka Low as A .Kuna chain ya watu wengi wazito hapo ,taifa litatikisika

Huwezi mshtaki nywele nyeupe bila kumgusa yule mkwere mtu wa watu
 
Tafsiri ya ulichokiwasilisha likely ni hiki;

Kama kampuni ya Richmond ilikuwa ya mfukoni isiyo na ofisi wala uwezo, mbona mpaka leo hii mitambo yake imetoka kuwa ya Richmond > Dowans > Symbion inazalisha umeme na TANESCO inanunua na capacity charge inalipwa??

......Hili haliwezekani, ni lazima Edward Ngoyai Lowassa ni fisadi kupindukia na chanzo cha matatizo yote ya wa - Bongo woote na sharti awe wa kwanza kusimama kwenye kizimba cha mahakama ya mafisadi wa Magufuli!!

Nimewaelewa sana ,ila tusahau Serikali hii iliyo jiapiza kuwafunga Mafisadi kama itathubutu kufanya hivi..Unafikiri Mfalme atathubutu kufukua Makaburi?...Alishaapa na kujiapiza(pamoja na kuwepo kinga Kikatiba) kuwalinda Wafalme wastaafu ...

Lile lilikuwa ni zengwe la kisiasa na mission ya muda mrefu kukata watu kwa sababu Mfalme wa wakati ule alikuwa na jina lake mfukoni....
 
Wamshtaki ili iwe kama kesi ya Balozi Mahalu ilivyoyeyuka. Maana kuna watu watapaswa kushitakiwa pamoja naye.
 
Kila aliyejimilikisha mali nyingi kwa njia za kiujanja ni fisadi tunasubili ,washitakiwe
 
Nami najivua gamba.Nilikuwa na chuki na hasira dhidi ya Lowassa kwa muda mrefu.Kwa sasa nahisi kujuta na kutubu kwa kumnenea,kumwombea ubaya pengine bila hatia!
Kwa kuwa Magufuli( rais) kaanzisha mahakama ya mafisadi,basi wa kwanza awe Lowassa! Asipopatikana na hatia itakuwa aibu kwetu na taifa!
 
MANENO YA MWAKYEMBE ALIPO HOJIWA KUHUSU SAKATA LA RICHMOND
July 21 2016 Waziri wa katiba na sheria, Dk. Harrison Mwakyembe alikuwa akihojiwa katika kipindi cha Clouds 360 cha clouds TV na kujibu maswali mbalimbali yanayohusu katiba na sheria na hili sakata la Richmond likagusiwa.

Mtangazaji wa clouds TV, Hudson Kamoga alimuuliza Waziri mwakyembe kuhusiana na sakata la Richmond wakati akiwa mwenyekiti wa kamati iliyokuwa inachunguza sakata hilo ambapo walikuja na ripoti ambayo ilipelekea aliyekuwa Waziri mkuu kwa wakati huo, Edward Lowassa kujiuzulu. Hudson ametaka kujua kama kuna mambo ambayo watanzania hawakuyajua kuhusu sakata la Richmond

Waziri Mwakyembe amesema ….>>>‘kesi ya Richmond tuliifanya kwa roho safi na kwa kupiga magoti kwa Mungu na tuliifanya haki kwa kila mtu tulichoamua hata tuamue kesho asubuhi nirudie tena hata koma haitabadilika itakuwa vilevile na mimi nitafurahi sana’

>>>’chini ya kanuni tunaruhusiwa kuifufua tena Richmond ili ichunguzwe upya na ninaaapa wanaweza wote wakahama wakaniacha peke yangu na uhakika mimi mwenyewe nilichonacho nitajenga hoja sidhani kama kuna mtu hata mmoja atasalimika kwenda jela‘
Kweli nyie ni vi laza sana maana hamjui hata kuwa hii mahakama itamuaibisha JK. Wallah naapia akiitwa Lowassa huko ndo itakuwa mwisho wa hiyo mahakama. Maana Lowassa atatoa ushahidi wote na namna JK alivyokuwa anamwelekeza kuvunja sheria. Let us wait and see
 
Shida ya kuvua kwa wavu, watavuliwa na 'kasa' ambao serikali imeshasema 'wakae wastarehe, itawalinda'
 
CCM Acheni siasa za kupandikiza chuki.wote tunajua kama mahakama ya mafisadi ikifanya kazi yake hakuna atakayepona ata uyo mnaemuita chaguo la mungu.
 
CCM Acheni siasa za kupandikiza chuki.wote tunajua kama mahakama ya mafisadi ikifanya kazi yake hakuna atakayepona ata uyo mnaemuita chaguo la mungu.
Kashfa ya uuzwajibwa nyumba za serikali nadhani hawataisema
 
MANENO YA MWAKYEMBE ALIPO HOJIWA KUHUSU SAKATA LA RICHMOND
July 21 2016 Waziri wa katiba na sheria, Dk. Harrison Mwakyembe alikuwa akihojiwa katika kipindi cha Clouds 360 cha clouds TV na kujibu maswali mbalimbali yanayohusu katiba na sheria na hili sakata la Richmond likagusiwa.

Mtangazaji wa clouds TV, Hudson Kamoga alimuuliza Waziri mwakyembe kuhusiana na sakata la Richmond wakati akiwa mwenyekiti wa kamati iliyokuwa inachunguza sakata hilo ambapo walikuja na ripoti ambayo ilipelekea aliyekuwa Waziri mkuu kwa wakati huo, Edward Lowassa kujiuzulu. Hudson ametaka kujua kama kuna mambo ambayo watanzania hawakuyajua kuhusu sakata la Richmond

Waziri Mwakyembe amesema ….>>>‘kesi ya Richmond tuliifanya kwa roho safi na kwa kupiga magoti kwa Mungu na tuliifanya haki kwa kila mtu tulichoamua hata tuamue kesho asubuhi nirudie tena hata koma haitabadilika itakuwa vilevile na mimi nitafurahi sana’

>>>’chini ya kanuni tunaruhusiwa kuifufua tena Richmond ili ichunguzwe upya na ninaaapa wanaweza wote wakahama wakaniacha peke yangu na uhakika mimi mwenyewe nilichonacho nitajenga hoja sidhani kama kuna mtu hata mmoja atasalimika kwenda jela‘
Wakwanza atakuw jk hapo!
 
Back
Top Bottom