Lazaro Nyalandu, Miss Tanzania na 40,000 za Ujenzi wa Shule!

mama mkapa hahusishwi na ufisadi kwa sababu tu ufisadi umefanywa na mumewe na pesa wanakula nyumbani!

mama mkapa ana husishwa na ufisadi wake mwenyewe. na mama kikwete ata husishwa na ufisadi wake mwenyewe kama anao.

sio kwa sababu umeolewa na fisadi ndio na wewe ujaziwe kashfa tele! sio haki hata kidogo.

na hasa ukizingatia kuwa kwa kesi hii walikuwa hawajaoana....kwa hiyo ndio kabisa HAHUSIKI na ufisadi huu uliofanywa na mtu ambaye baadae amemuoa

Mimi naona hata yeye kama ana taarifa anaweza kusema tu!
Kwani si mke na mume ndio wanashiriki kwenye maandalizi na hata kuwasiliana mambo yanavyokwenda?

Pia huyo dada ni Miss Tanzania...Tatizo ni wakati anatuwakilisha tunsema analiwakilisha taifa...Lakini hishma hiyo ghafla unamvuwa!?

Acha hizo!

Sasa turudi kwenye pointi...Hapa maelezo yanahitajika na tunamsubiri Nyalandu kwa maelezo na sasa mjadala uendelee!

Pia kumbuka kuwa hakuna aliyempa kashfa Miss Tanzania!
Mbona unatake personal?

Hapa tunazungumzia harusi yako na uache kuwa nyanyapaa wakina dada kwa kudhani kuwa ni wanaume tu wenye kuplay role kwenye majukumu ya ndoa.
 
imehusiana vipi ya kuwa yeye miss tanzania (wa zamani) na kujua pesa zilizochangwa kwenye harusi yake zinatoka wapi?

hivi wewe ukija kuoa unategemea pesa zitakazochangwa na marafiki, ndugu, jamaa wa mtu unayemuoa kuzijua zinatoka wapi?

didnt know kuwa wewe bado ni mdogo kiasi hicho!
 
sijamvua hishma ya kuwa alikuwa miss tanzania, lakini siwezi kumhukumu kwenye jambo ambalo hahusiki just kwa kuwa aliwahi kuwa miss tanzania.
 
Wewe na wapambe wako mimi sina muda na nyie...Mimi nawapa Facts!
Kwani inaonyesha mnasubiria tu kila wakati kama mafisi!
Hayo hapo chini ni mimi nimeyasema?
Kweli kama tuko hivi bongo basi risasi watu wanaweza pigana!
Yani TOPE TU!

kwi! kwi! kwi! hii kali wanasubili mzoga kisha wamalize na kumeza then.....
 
Hoja kuu hapa sio mheshimiwa na mchumba wake! hoja hapa ni shs 235,000/= za ujenzi wa shule kutumika visivyo.

Hoja nyingine ni WDC kuidhinisha fedha za umma kwa matumizi binafsi (40,000/= za harusi) nadhani huu ni wizi na walistahili kufikishwa kortini, kama bado basi mkaguzi wa hesabu wa mkoa anatakiwa asimamishwe kazi na ahojiwe kama kuna hatia afutwe kazi na afikishwe kortini maramoja.

Lakini pia isije kuwa procedures za kudhibiti fedha ngazi ya kata zinamapungufu hivyo inatakiwa zichunguzwe na kupitiwa upya.
 
Tumwite Miss Singida Jamani S Ameshakula Na Hela Za Wananchi Wa Uko!!!!
Kwa Taarifa Tu Hiyo 40,000 Ndiyo Iliyotangazwa Wamechukua 85,000
Kazi Kwenu
Chukua Chako Mapema Kama Mbunge Akuzipata Bhizi Afwatile Kilichoandikwa
 
Kama ukiona kimya na bado hawajajibu basi ujuwe ushahidi ni mzito!
Kaazi kweli kweli.
 
Nadhani madai haya siyo kweli sana kwani nina imani kuwa Mbunge ana hela nyingi sana kiasi kuwa hizo shiling 40,000 ni ndogo sana kwake kuiba unless jamaa mwenyewe awe ni kleptomaniac. Linaloweza kuwa limefanyika ni kuwa jamaa alipewa michango, halafu akasahau na kujikuta akiwa ameitumia bila kuwa na lengo la kuiiba.

Lakini, je ni kweli huyu bwana alisoma na kumaliza digrii mbili huko Iowa? kwenye tovuti ya Bunge anadai kuwa alipata digrii ya BA (Business Administration) kutoka Waldorf University College(U.S.A) alikosomea kuanzia mwaka 1994 hadi 1996, na digrii ya BA. (International Business) aliyopata Wartburg University College (U.S.A) alikosomea kuanzia mwaka 1996 hadi 1998. Kwanza, hakuna vyuo vyenye majina hayo huko Marekani, ila huko Iowa kuna chuo cha Waldorf College kilichopo pale Forest City, na chuo cha Wartburg College kilichopo pale Waverly. Vyuo vyote hivi ni vya miaka minne minne, kwa hiyo ni vigumu kwa Bwana Nyarandu kusoma vyuo vyote viwili kwa miaka miwili miwili kama anavyodai; just curious.
 
]mama mkapa hahusishwi na ufisadi kwa sababu tu ufisadi umefanywa na mumewe na pesa wanakula nyumbani[/B]!

mama mkapa ana husishwa na ufisadi wake mwenyewe. na mama kikwete ata husishwa na ufisadi wake mwenyewe kama anao.

sio kwa sababu umeolewa na fisadi ndio na wewe ujaziwe kashfa tele! sio haki hata kidogo.

na hasa ukizingatia kuwa kwa kesi hii walikuwa hawajaoana....kwa hiyo ndio kabisa HAHUSIKI na ufisadi huu uliofanywa na mtu ambaye baadae amemuoa
Duh!We dada ni mbishi jamani.
 
Nadhani madai haya siyo kweli sana kwani nina imani kuwa Mbunge ana hela nyingi sana kiasi kuwa hizo shiling 40,000 ni ndogo sana kwake kuiba unless jamaa mwenyewe awe ni kleptomaniac. Linaloweza kuwa limefanyika ni kuwa jamaa alipewa michango, halafu akasahau na kujikuta akiwa ameitumia bila kuwa na lengo la kuiiba.

Lakini, je ni kweli huyu bwana alisoma na kumaliza digrii mbili huko Iowa? kwenye tovuti ya Bunge anadai kuwa alipata digrii ya BA (Business Administration) kutoka Waldorf University College(U.S.A) alikosomea kuanzia mwaka 1994 hadi 1996, na digrii ya BA. (International Business) aliyopata Wartburg University College (U.S.A) alikosomea kuanzia mwaka 1996 hadi 1998. Kwanza, hakuna vyuo vyenye majina hayo huko Marekani, ila huko Iowa kuna chuo cha Waldorf College kilichopo pale Forest City, na chuo cha Wartburg College kilichopo pale Waverly. Vyuo vyote hivi ni vya miaka minne minne, kwa hiyo ni vigumu kwa Bwana Nyarandu kusoma vyuo vyote viwili kwa miaka miwili miwili kama anavyodai; just curious.
Ndugu Kichuguu,sikumbuki kama alikanusha ama vipi.Labda wenye kumbukumbu watatujulisha.
 
Siasa bwana kweli ni mchezo mchafu,kumbe tunapotaka kuoa tuwe tunaangalia source za michango dah ngumu mno kitanzania bila kutazama nyazifa zao kitaifa bibi na bwana haruc naona hawastahili lawama kwa hili,nilikuwa napita tu ila kama tutaendeleza zidumu fikra za viongoz hatutafika,kila lawama zielekezwe kwa wahusika ili tuwatendee haki wengine
 
Ndugu Kichuguu,sikumbuki kama alikanusha ama vipi.Labda wenye kumbukumbu watatujulisha.

Aaah akanushe wapi...?huyu naye haeleweki.... Mara mtu wa totos, Mara bi-sexual...basi tu haeleweki.....
Though anajuwa kujieleza sana na ku-play na media....
 
Dk. Slaa amshukia mbunge mwenzake

2008-07-15 11:09:29
Na Elisante John, PST Singida

Mbunge wa Karatu (CHADEMA), Dk. Wilbroad Slaa, amemshukia mbunge mwenzake, Bw. Lazaro Nyalandu (CCM-Singida Kaskazini) akimtuhumu kumuoa Miss Tanzania kwa kutumia michango ya wananchi kwa ajili ya ujenzi wa shule.

Akitoa tuhuma hizo, Dk. Slaa ambaye pia ni kiongozi wa Kamati ya Bunge ya Kukagua Hesabu za Serikali za Mitaa, alidai kuwa, hivi karibuni, zilitolewa Sh. 40,000 kwenye fungu la ujenzi huo na kuchangia harusi ya Mbunge huyo.

Hata hivyo, Bw. Nyalandu alipoulizwa juu ya madai hayo, alikanusha kupewa.

Dk. Slaa, alitoa onyo hilo mjini hapa jana wakati akihutubia mamia ya wakazi wa Singida Mjini katika viwanja vya Shule ya Msingi Ukombozi.

Akihutubia kwa niaba ya ushirikiano wa vyama vitano vya siasa vya upinzani nchini, aliwataka wakazi wa Singida kuunga mkono jitihada zinazofanywa na vyama vya upinzani katika mapambano dhidi ya mafisadi, badala ya kuendelea kuing`ang`ania CCM huku wakijiita wakereketwa.

Dk. Slaa, alisema wakazi wa mkoa huo wanaona sifa na ufahari mkubwa kuitwa `Singida ni Mkoa wa CCM`, lakini bila kujua wananyonywa na mafisadi waliowaweka madarakani, huku wao wakiambulia kuvaa kofia, tisheti na khanga za mabango au dumu moja la pombe na kutoa kura kwa mtu akaibe mabilioni.

Akitoa mfano, Dk. Slaa alitoa nakala ya muhtasari wa kikao cha kamati ya maendeleo ya kata ya Kinyeto, wilayani Singida, kilichokaa Desemba, mwaka jana, kupitisha matumizi ya fedha za ujenzi wa sekondari, badala yake zimetumiwa isivyo halali.

Alitaja baadhi ya matumizi hayo kuwa ni pamoja na kuchangia harusi ya Mbunge wa Jimbo hilo, Sh. 40,000, posho kwa wajumbe wawili kwenda benki Sh. 40,000, posho kwa ajili ya kikao cha Halmashauri Kuu ya CCM, Sh. 30,000, kufuatilia mbao Sh. 20,000 na kufuatilia kibali wilayani Sh. 85,000.

``Kwa kweli haya ni matumizi mabaya kabisa ya michango ya wananchi ambao wamelazimika kuchangishana ili kujenga shule ya sekondari watoto wao wasome, lakini bila sababu za msingi mafisadi, wezi, wamekula fedha hizo,`` alidai Dk. Slaa.

Aliongeza ``haiwezekani jasho la wananchi litumiwe na mtu mmoja�Eti ili tu kumfurahisha Mbunge aweze kumuoa miss Tanzania�angalia jinsi watu wa Singida mnavyochekwa na wenzenu, huku mnajiita ni mkoa wa CCM.``

Dk. Slaa alisema kuwa iwapo mkoa huo ungekuwa na Diwani hata mmoja tu anayetoka chama cha upizani, angesaidia kukemea maovu mbali mbali yanayotokea katika mkoa huo, lakini kutokana na kujiita mkoa wa CCM, ndiyo maana maovu mengi yanachelewa kufichuliwa hadi wao watoke mbali.

Aidha, Dk. Slaa, alikemea tabia ya baadhi ya Watendaji wa Serikali kuwaandikia barua za vitisho watendaji wa kata na vijiji wasioiunga mkono CCM.

Alisema kuwa ana ushahidi wa kutosha juu ya aliyekuwa Mkurugenzi wa Manispaa ya Singida, Bi. Benadetta Kinabo, aliyehamishiwa Manispaa ya Moshi, juu ya kujihusisha na tabia hiyo ambayo ni kinyume na maadili ya kazi yake.

Ili kuhakikisha tabia hiyo inakomeshwa, Dk. Slaa alisema kuwa kwa kushirikiana na vyama vya upinzani bungeni, atahakikisha Mkurugenzi huyo anaitwa na kuhojiwa, ili iwe fundisho kwa watendaji wengine wa serikali wanaodhoofisha vyama vya upinzani nchini.

Ukiishiwa si lazima uposti utumbo humu JF, habari yenyewe ni ya mwaka 2007 halafu ya kizushi isiyo na mashiko. Dk. Slaa anapenda sana mademu hivyo ulikuwa ni wivu tu kwamba jamaa kalamba Miss TZ. Kuzungumzia Sh 40,000 maana yake nini? haina mantiki.
 
Bado hajakanusha,unless unazo hizo taarifa.Mimi nilikuwa mjumbe tu.Mbane huyo Elisante John.Mimi nambana kiongozi.We vipi wewe?Dr Slaa ametumia pesa za wananchi kwa mademu?Unakurupuka tu.Kama wewe ndo waziri jibu.Kama siyo msaidie kama una data,kama huna kaa kimya,si lazima uchangie.
 
Watu wengine very PAMBAF!
Sasa wewe Indume iyene, Gaidijini na wenzake semeni kama ni nani aliyetowa hiyo kauli hapo juu maana mnaudhi na bakora mnahitaji kwa mwendo huu mpaka za vichwa ni haki!

Kwanini badala ya kuendelea na mijadala tunategana tu?

Mnafikiri niko kwenye maslahi hapa?

Tumieni Mbongo zenu na mtumie muda kwenye kujadili issue Taifa liko njia panda lakini kuna watu kila kukichwa hapa wanategea Jmushi achemshe!
Mnajichemsha wenyewe!

This thread reminded me how uncivilized some people are.
 
Cha muhimu ni kufanya mkutano jimboni kwake na kudai pesa yetu pamoja na riba ya 5000%.
 
Cha muhimu ni kufanya mkutano jimboni kwake na kudai pesa yetu pamoja na riba ya 5000%.
Ha ha ha!Halafu kuna watu wanadai eti ni 40,000 tu!Wao wanadhani analalamikiwa kwasababu ya kiwango peke yake.Nadhani ndo maana kadharau kujibu.
 
Back
Top Bottom