Lazaro Nyalandu, Miss Tanzania na 40,000 za Ujenzi wa Shule!

jmushi1

Platinum Member
Nov 2, 2007
24,987
22,515
Dk. Slaa amshukia mbunge mwenzake

2008-07-15 11:09:29
Na Elisante John, PST Singida

Mbunge wa Karatu (CHADEMA), Dk. Wilbroad Slaa, amemshukia mbunge mwenzake, Bw. Lazaro Nyalandu (CCM-Singida Kaskazini) akimtuhumu kumuoa Miss Tanzania kwa kutumia michango ya wananchi kwa ajili ya ujenzi wa shule.

Akitoa tuhuma hizo, Dk. Slaa ambaye pia ni kiongozi wa Kamati ya Bunge ya Kukagua Hesabu za Serikali za Mitaa, alidai kuwa, hivi karibuni, zilitolewa Sh. 40,000 kwenye fungu la ujenzi huo na kuchangia harusi ya Mbunge huyo.

Hata hivyo, Bw. Nyalandu alipoulizwa juu ya madai hayo, alikanusha kupewa.

Dk. Slaa, alitoa onyo hilo mjini hapa jana wakati akihutubia mamia ya wakazi wa Singida Mjini katika viwanja vya Shule ya Msingi Ukombozi.

Akihutubia kwa niaba ya ushirikiano wa vyama vitano vya siasa vya upinzani nchini, aliwataka wakazi wa Singida kuunga mkono jitihada zinazofanywa na vyama vya upinzani katika mapambano dhidi ya mafisadi, badala ya kuendelea kuing`ang`ania CCM huku wakijiita wakereketwa.

Dk. Slaa, alisema wakazi wa mkoa huo wanaona sifa na ufahari mkubwa kuitwa `Singida ni Mkoa wa CCM`, lakini bila kujua wananyonywa na mafisadi waliowaweka madarakani, huku wao wakiambulia kuvaa kofia, tisheti na khanga za mabango au dumu moja la pombe na kutoa kura kwa mtu akaibe mabilioni.

Akitoa mfano, Dk. Slaa alitoa nakala ya muhtasari wa kikao cha kamati ya maendeleo ya kata ya Kinyeto, wilayani Singida, kilichokaa Desemba, mwaka jana, kupitisha matumizi ya fedha za ujenzi wa sekondari, badala yake zimetumiwa isivyo halali.

Alitaja baadhi ya matumizi hayo kuwa ni pamoja na kuchangia harusi ya Mbunge wa Jimbo hilo, Sh. 40,000, posho kwa wajumbe wawili kwenda benki Sh. 40,000, posho kwa ajili ya kikao cha Halmashauri Kuu ya CCM, Sh. 30,000, kufuatilia mbao Sh. 20,000 na kufuatilia kibali wilayani Sh. 85,000.

``Kwa kweli haya ni matumizi mabaya kabisa ya michango ya wananchi ambao wamelazimika kuchangishana ili kujenga shule ya sekondari watoto wao wasome, lakini bila sababu za msingi mafisadi, wezi, wamekula fedha hizo,`` alidai Dk. Slaa.

Aliongeza ``haiwezekani jasho la wananchi litumiwe na mtu mmoja�Eti ili tu kumfurahisha Mbunge aweze kumuoa miss Tanzania�angalia jinsi watu wa Singida mnavyochekwa na wenzenu, huku mnajiita ni mkoa wa CCM.``

Dk. Slaa alisema kuwa iwapo mkoa huo ungekuwa na Diwani hata mmoja tu anayetoka chama cha upizani, angesaidia kukemea maovu mbali mbali yanayotokea katika mkoa huo, lakini kutokana na kujiita mkoa wa CCM, ndiyo maana maovu mengi yanachelewa kufichuliwa hadi wao watoke mbali.

Aidha, Dk. Slaa, alikemea tabia ya baadhi ya Watendaji wa Serikali kuwaandikia barua za vitisho watendaji wa kata na vijiji wasioiunga mkono CCM.

Alisema kuwa ana ushahidi wa kutosha juu ya aliyekuwa Mkurugenzi wa Manispaa ya Singida, Bi. Benadetta Kinabo, aliyehamishiwa Manispaa ya Moshi, juu ya kujihusisha na tabia hiyo ambayo ni kinyume na maadili ya kazi yake.

Ili kuhakikisha tabia hiyo inakomeshwa, Dk. Slaa alisema kuwa kwa kushirikiana na vyama vya upinzani bungeni, atahakikisha Mkurugenzi huyo anaitwa na kuhojiwa, ili iwe fundisho kwa watendaji wengine wa serikali wanaodhoofisha vyama vya upinzani nchini.
 
Ama kweli story za malikia na mfalme huanzia mbali!

Sasa hadi kwenye pesa za kujenga shule jamani?

Tena kwasababu tu ya Harusi?

Hizi harusi za kibongo za gharama na wakati huo huo mara baada ya harusi watu wanaanza kujiuliza namna ya kuishi ni mambo yasiyokuwa ya msingi kabisa!

Sasa huyo Miss Tanzania ni yupi huyo?

Na kama kweli yeye ni Miss Tanzania nni kwanini hajali kuhusu elimu?
Ama just beacause of their wedding ndi wasahahu wananchi tena na kitu muhimu kama shule?..Vipi akiwa FIRST LADY?

Atawajali wananchi kweli kabla hajaenda kufanya shopping PARIS?

Na ndio maana napinga sana watu masikini kufanya arusi za kifahari na viongozi wetu wangeutumia mfano huo kuwa licha ya kwamba ni kweli tukio la ndoa ni kubwa...

Tusijisahau kwenye hilo...

Bali pia tutowe kipa umbele kwenye maisha yao na si gharama za arusi kwani wakati wa arusi kila mtu yuko na kula na kunywa na kusaza lakini ni wanandoa hao hao ambao wana uwezekano wa ku suffer kwa njaa ama mahitaji mengine mara baada ya arusi na nderemo na vifijo kwisha!

Kama ni kweli haya basi tunaomba Nyalandu aombe msamaha..Arudishe pesa za wananchi na pia ahakikishe shule hiyo imejengwa hata kama ikibidi wao walale njaa!

TUMECHOSHWA NA UHUNI WA AINA HII!
 
Tunataka kusikiaa hizo 40,000 zilitokajae?isije kuwa wajumbe wa kamati hiyo.....walijikomba kumchangia ili wawe wakumbukwe kwenye ufalme wake.....hapo tunataka mazingira halisii ya kuchangiana yalikuwaje?
 
Ni jambo la kusikitisha sana kwani ufisadi huanzia chini!

Kama unaweza kuwafanyia ufisadi wananchi wanyonge tena wanaohitaji elimu basi hatuna viongozi!

Tena la kusikitisha ni arusi ichangiwe na pesa za ujenzi wa shule?

Hata kama ingekuwa ni elfu bado inaonyesha ubaradhuli wa hali ya juu!

Kwani ufisadi si tu ni vitendo...Bali ni MOYO WA MTU!

Kwani ndio maana tunasema tunataka haki kwenye level zote!

Mtu ambaye anajuwa kabisa kuwa elimu kwa watanzania ni sawa na kupata madini ya Tanzanite kwa Mwanapolo wa mererani!

Jinsi ambavyo elimu imekuwa anasa badala ya haki!

Hajuwi kuwa watoto wa Tanzania wanaopata elimu hawafikii hata nusu ya watoto wote wa Tanzania?

Hili limenisikitisha sana na kwa kweli mfano huo aliounyesha Nyalandu ni wa kulaaniwa kwa nguvu zote!
 
Kanifurahisha alivyowaambia ukweli wananchi wa Singida ,nasikitika sana wananchi jinsi wanavyoweza kufall na kuchagua mpuuzi kama nyalandu (namjua huyu mtu vizuri sana tulikuwa naye pamoja Marekani) ...hii mijitu na likes za kina Serukamba ndio ikiachiwa itakuwa pale muda mrefu na kuja kulimaliza Taifa kwa ufisadi...Nyalandu & Serukamba must go.
 
Koba..Ni utaratibu tulionao sisi wa bongo bila kujali ni wapi tupo duniani!
Na huu ni mfano halisi!
Yeye ameona arusi yake ni muhimu kuliko hata maisha ya watoto?
Na sasa sisi watanzania ndiyo hivyo hivyo tu!

Kwani utakuta mtanzani wa kawaida hata kazi hana...Lakini mchango wa arusi ni wa kifahari!

Sasa sisi hatuoni mbele kwani pesa badala ya kufanya matanuzi ya mvinyo na limosine..Inatakiwa iwasaidie wana ndoa hao ili waweze kujikimu kwenye maisha yao mapya!

Utamaduni wetu mwingine ni wa kukomesha na hilo ni lazima tulibadili kama tunataka kuibadili jamii yetu.

Ni kama mfano nilioutowa kuwa hatuangalii mbele ili kujuwa tutafika vipi kwenye safari ya kujikwamua..Sisi tunaangalia hapo chini tu kama kuku!

Tuna chakura chakura tu kupata wadudu!

Its time to FLY GUYS!
 
Ama kweli story za malikia na mfalme huanzia mbali!

Sasa hadi kwenye pesa za kujenga shule jamani?

Tena kwasababu tu ya Harusi?

Hizi harusi za kibongo za gharama na wakati huo huo mara baada ya harusi watu wanaanza kujiuliza namna ya kuishi ni mambo yasiyokuwa ya msingi kabisa!

Sasa huyo Miss Tanzania ni yupi huyo?

Na kama kweli yeye ni Miss Tanzania nni kwanini hajali kuhusu elimu?
Ama just beacause of their wedding ndi wasahahu wananchi tena na kitu muhimu kama shule?..Vipi akiwa FIRST LADY?

Atawajali wananchi kweli kabla hajaenda kufanya shopping PARIS?

Na ndio maana napinga sana watu masikini kufanya arusi za kifahari na viongozi wetu wangeutumia mfano huo kuwa licha ya kwamba ni kweli tukio la ndoa ni kubwa...

Tusijisahau kwenye hilo...

Bali pia tutowe kipa umbele kwenye maisha yao na si gharama za arusi kwani wakati wa arusi kila mtu yuko na kula na kunywa na kusaza lakini ni wanandoa hao hao ambao wana uwezekano wa ku suffer kwa njaa ama mahitaji mengine mara baada ya arusi na nderemo na vifijo kwisha!

Kama ni kweli haya basi tunaomba Nyalandu aombe msamaha..Arudishe pesa za wananchi na pia ahakikishe shule hiyo imejengwa hata kama ikibidi wao walale njaa!

TUMECHOSHWA NA UHUNI WA AINA HII!
Miss Tanzania FARAJA KOTA
 
Miss Tanzania FARAJA KOTA

Binti alikuwa kweli ana mvuto na mmojawapo wa warembo wa Tanzania waliostahili taji hilo licha a kwamba uwakilishi wake kwenye mashindano ya dunia haukufika mbali.

Sasa kama u Miss Tanzania huwezi kuwa balozi wa maendeleo ya myonge,haki yake na elimu..Je kweli unafaa kukaa kwenye nafasi ya kusema wewe ni mke wa kiongozi wa jamii mnayotaka kuisaidia?

Na kiongozi mwenyewe huyo Lazaro..Hakufikiria hilo?

Kama uzalendo unamshinda kwenye 40,000 za kumkwamua atauweza vipi pale kwenye kutetea mabilioni ya Taifa?

Hapo ni ubunge na sasa urais ukipewa itakuwa vipi?

Ni mfano gani huu unaoonyeshwa na hawa viongozi wetu?

Uzalendo na Uungawana si maneno bali ni vitendo!

Utu wema na fadhili pia huonekana kutokana na matendo yako kwa wale unaowaongoza.

Sasa kweli Nyalandu na umaarufu wake wote na ubunge wake walishindwa vipi kupata mtu wa kuwapa 40,000 ama hata michango ya jamaa na ndugu na viongozi wenzake...?!

Hadi kudeep kwenye mfuko wa kuokoa maisha ya vizazi vyetu vijavyo?

HII INA TOFAUTI GANI NA KITENDO CHA KUJARIBU KU EXTRACT BLOOD FROM THE MERELY DEAD BODY!?

Ama kwa kiswahili fasaha ni kwamba ni sawa na kitendo cha kujaribu kuinyonya maiti damu!
40,000 kutoka kwenye ujenzi wa shule jamani si kunyonya maiti damu huko?!

Mi nakwambia kama kweli huyu mtu angekuwa mzalendo wa kweli..Basi angezikataa hizo pesa!

SWALI LANGU LINGINE AMBALO LABDA LITANIFANYA NIMWONEE HURUMA HUYU LAZARO AMA KUMPA BENEFITI OF DOUBT..NI HILI..

JE NA YEYE ALISHAWAHI KUICHANGIA HIYO SHULE?

Nini hasa mchango wake kwenye ujenzi wa shule hiyo?

Je alijuwa kuwa pesa hizo za shule zinakwenda kwenye arusi yake?

PESA ZENYEWE 40,000?

WAPI UTU?

WAPI UBINADAMU?

DIGNITY...DIGNITY NDUGU ZANGU!
 
Jmushi

Wewe ni mtu mwenye matatizo ya kufikiri. Maswali yako na hoja zako huwa zinajichanganya changanya. Uwe unatulia na kusoma kwanza kabla ya kuandika andika tu! I am telling you as a friend.

Asha
 
Last edited:
Kuna watu waatakuja wadai ati 40,000 sio kitu! Lol....

Kaka Nashukuru kwa hii habari...

Washawahi kusikia "It's the principle, not the amount"

Hapo ndipo utakapomkuta Warren Buffet kanunua kitu some dollars and ninety nine cents halafu anangojea one penny yake.

Tell them it's the principle jack!
 
Jmushi

Wewe ni mtu mwenye matatizo ya kufikiri. Maswali yako na hoja zako huwa zinajichanganya changanya. Uwe unatulia na kusoma kwanza kabla ya kuandika andika tu! I am telling you as a friend.

Asha

WEWE ASHA si unadai wewe ni CHADEMA?

Muulize aliyetowa taarifa hizo!

Kama mmegawanyika kwa UFISADI WENU NI NYIE WENYEWE!

Mimi nachukulia maanani kauli ya Dr Slaa!

Bila kujali kama yeye ni chama gani!

Mimi ni HURU!

GET IT!

Ninakubaliana na mawazo ya watu wa tofauti saa nyingine pia ya wapinzani na saa nyingine ya baadhi ya ccm safi.

Hapa tunazungumzia watu wawili wenye influence kubwa sana kwenye jamii yetu!

Miss Tanzaia ni mrembo wa nchi na mwakilishi wetu!

Awe ameolewa ama la...Hilo halifuti ukweli wa nafasi yake kwenye jamii!

Bado yeye ni Miss Tanzania and also the wife of the MP!

Na MP mwenyewe pia ni mwakilishi wa wananchi ambaye kwanza kabisa alitakiwa ahakikishe ujenzi wa shule hiyo unamalizika mara moja kwa juhudi zake yeye kama mbunge na si kulamba 40,000 za wavuja jasho simply kwa kisingizio cha arusi na ama hata msiba!

HIVYO KWA HILI..WEWE NDIO UMEONYESHA KUJICHANGANYA!
 
1.Kumsema huyu dada kwa sababu tuu ni miss sio haki,na hata Dr.Slaa hakujua kama Lazaro alimuoa nani ila alipoletewa malalamiko hayo aliyasema na kuonyesha jinsi wananchi wanavyoliwa pesa zao.

2.Huyu mbunge anapaswa ajitakase ,kwani inawezekana kuwa kuna Diwani alienda kujipendekeza na hakusema kama alichukua mchango wa Secondary sasa anapaswa ama kumkana ama kumrudishia hizo pesa zake.

KUna haja ya kujadili hoja.
 
Binti alikuwa kweli ana mvuto na mmojawapo wa warembo wa Tanzania waliostahili taji hilo licha a kwamba uwakilishi wake kwenye mashindano ya dunia haukufika mbali.

Sasa kama u Miss Tanzania huwezi kuwa balozi wa maendeleo ya myonge,haki yake na elimu..Je kweli unafaa kukaa kwenye nafasi ya kusema wewe ni mke wa kiongozi wa jamii mnayotaka kuisaidia?

Na kiongozi mwenyewe huyo Lazaro..Hakufikiria hilo?

Kama uzalendo unamshinda kwenye 40,000 za kumkwamua atauweza vipi pale kwenye kutetea mabilioni ya Taifa?

Hapo ni ubunge na sasa urais ukipewa itakuwa vipi?

Ni mfano gani huu unaoonyeshwa na hawa viongozi wetu?

Uzalendo na Uungawana si maneno bali ni vitendo!

Utu wema na fadhili pia huonekana kutokana na matendo yako kwa wale unaowaongoza.

Sasa kweli Nyalandu na umaarufu wake wote na ubunge wake walishindwa vipi kupata mtu wa kuwapa 40,000 ama hata michango ya jamaa na ndugu na viongozi wenzake...?!

Hadi kudeep kwenye mfuko wa kuokoa maisha ya vizazi vyetu vijavyo?

HII INA TOFAUTI GANI NA KITENDO CHA KUJARIBU KU EXTRACT BLOOD FROM THE MERELY DEAD BODY!?

Ama kwa kiswahili fasaha ni kwamba ni sawa na kitendo cha kujaribu kuinyonya maiti damu!
40,000 kutoka kwenye ujenzi wa shule jamani si kunyonya maiti damu huko?!

Mi nakwambia kama kweli huyu mtu angekuwa mzalendo wa kweli..Basi angezikataa hizo pesa!

SWALI LANGU LINGINE AMBALO LABDA LITANIFANYA NIMWONEE HURUMA HUYU LAZARO AMA KUMPA BENEFITI OF DOUBT..NI HILI..

JE NA YEYE ALISHAWAHI KUICHANGIA HIYO SHULE?

Nini hasa mchango wake kwenye ujenzi wa shule hiyo?

Je alijuwa kuwa pesa hizo za shule zinakwenda kwenye arusi yake?

PESA ZENYEWE 40,000?

WAPI UTU?

WAPI UBINADAMU?

DIGNITY...DIGNITY NDUGU ZANGU!

Angalia maswali yako ya juu na ya chini halafu soma na habari yenyewe utaona kuwa unachouliza kishajibiwa kwenye habari yenyewe. So you are just flooding the thread.

Huyo Lazaro ni fisadi, Dr Slaa yuko sahihi huo ni ufisadi wa hiyo kata ya iliyochini ya CCM. Lazaro ana ufisadi wake mkubwa zaidi ya huo.

Asha
 
WEWE ASHA si unadai wewe ni CHADEMA?

Muulize aliyetowa taarifa hizo!

Kama mmegawanyika kwa UFISADI WENU NI NYIE WENYEWE!

Mimi nachukulia maanani kauli ya Dr Slaa!

Bila kujali kama yeye ni chama gani!

Mimi ni HURU!

GET IT!

Ninakubaliana na mawazo ya watu wa tofauti saa nyingine pia ya wapinzani na saa nyingine ya baadhi ya ccm safi.

Hapa tunazungumzia watu wawili wenye influence kubwa sana kwenye jamii yetu!

Miss Tanzaia ni mrembo wa nchi na mwakilishi wetu!

Awe ameolewa ama la...Hilo halifuti ukweli wa nafasi yake kwenye jamii!

Bado yeye ni Miss Tanzania and also the wife of the MP!

Na MP mwenyewe pia ni mwakilishi wa wananchi ambaye kwanza kabisa alitakiwa ahakikishe ujenzi wa shule hiyo unamalizika mara moja kwa juhudi zake yeye kama mbunge na si kulamba 40,000 za wavuja jasho simply kwa kisingizio cha arusi na ama hata msiba!

HIVYO KWA HILI..WEWE NDIO UMEONYESHA KUJICHANGANYA!

Jmushi,

Argue, don't shout!

1. Miss Tanzania ni Richa Adhia, au we unae wa kwako sasa?

2. Lazaro hajachukua yeye, zimechukuliwa kwa ajili yake na viongozi wake wa CCM. Hivyo ni ishara ya CCM kuwa Chama Cha Mafisadi.

Dr Slaa hapa amemtumia Lazaro na Miss wake kuanika tu ufisadi uliopo huko Singida wa fedha za wananchi.

That said: I insist Lazaro ana ufisadi mkubwa zaidi ya huo.

Asha
 
1.Kumsema huyu dada kwa sababu tuu ni miss sio haki,na hata Dr.Slaa hakujua kama Lazaro alimuoa nani ila alipoletewa malalamiko hayo aliyasema na kuonyesha jinsi wananchi wanavyoliwa pesa zao.

2.Huyu mbunge anapaswa ajitakase ,kwani inawezekana kuwa kuna Diwani alienda kujipendekeza na hakusema kama alichukua mchango wa Secondary sasa anapaswa ama kumkana ama kumrudishia hizo pesa zake.

KUna haja ya kujadili hoja.

Na ndio hapo pointi yangu ilipo!

Aje hapa huyo lazaro atupe ukweli kwani sisi hatuna HUSDA HAPA JF!

Tuna tabia ya kusikiliza pande zote za message ili kuwa na uwiano wa haki bila mtu kukandamizwa!

Fuatilia postings zangu zote hapo juu na utaelewa malengo yangu si PERSONAL!

Inapokuja kwenye HAKI YA MTANZANIA KILA KITU NI PEMBENI!

Aje hapa atuambie ushiriki wake kwenye ujenzi huo wa shule ni wa namna gani kwasababu haya mambo ya kuchukuwa 40,000 ni UBWANYENYE!

NARUDIA TENA....SI HAKI KABISA KWANI HII NI MBAYA ZAIDI KUTOKANA NA UKWELI KUWA SHULE YENYEWE HAIJAKAMILIKA!

Na labda kama hata angekuwa amekopa basi hiyo ni suala la tofauti!

Na kama tulivyoshuhudia Rostam alivyotowa pesa za Kwaya ya AMKENI!

Hivi unataka kuniambia huyo mchungaji alishindwa kutoa milioni mbili kwenye akaunti ya kanisa ili kununuwa generator?

Ama ni kutokujali kumetutawala pamoja na dharau kwa masikini wasio na elimu?

Nani hajuwi kuwa ni sera ya ccm kutowapa wananchi elimu!

KWENYE HILI KWAKWELI HATUTAKUBALIANA KABISA UNLESS LAZARO MWENYEWE AJE HAPA KUTOWA MAELEZO YA KINA!

Na hapo kwenye pointi ya Mrs Nyalandu kuwa Miss Tz ni issue amabyo haiwezi kufutika kwasababu kaolewa sasa!

Yeye bado ni kama nembo ya TAIFA na kama vile mumewe anavyowawakilisha wananchi buneni...Basi na yeye alituwakilisha Duniani na alibeba bendera ya Taifa kwa niaba yetu watanzania na Amiri Jeshi wetu mkuu!

Ni position ambayo inakwenda na responsibilities!

Hivyo kuwa makini ni SUALA LA MUHIMU HASWA INAPOKUJA KUWATUMIKIA WANANCHI.
 
Na ndio hapo pointi yangu ilipo!

Aje hapa huyo lazaro atupe ukweli kwani sisi hatuna HUSDA HAPA JF!

Tuna tabia ya kusikiliza pande zote za message ili kuwa na uwiano wa haki bila mtu kukandamizwa!

Fuatilia postings zangu zote hapo juu na utaelewa malengo yangu si PERSONAL!

Inapokuja kwenye HAKI YA MTANZANIA KILA KITU NI PEMBENI!

Aje hapa atuambie ushiriki wake kwenye ujenzi huo wa shule ni wa namna gani kwasababu haya mambo ya kuchukuwa 40,000 ni UBWANYENYE!

NARUDIA TENA....SI HAKI KABISA KWANI HII NI MBAYA ZAIDI KUTOKANA NA UKWELI KUWA SHULE YENYEWE HAIJAKAMILIKA!

Na labda kama hata angekuwa amekopa basi hiyo ni suala la tofauti!

Na kama tulivyoshuhudia Rostam alivyotowa pesa za Kwaya ya AMKENI!

Hivi unataka kuniambia huyo mchungaji alishindwa kutoa milioni mbili kwenye akaunti ya kanisa ili kununuwa generator?

Ama ni kutokujali kumetutawala pamoja na dharau kwa masikini wasio na elimu?

Nani hajuwi kuwa ni sera ya ccm kutowapa wananchi elimu!

KWENYE HILI KWAKWELI HATUTAKUBALIANA KABISA UNLESS LAZARO MWENYEWE AJE HAPA KUTOWA MAELEZO YA KINA!

Na hapo kwenye pointi ya Mrs Nyalandu kuwa Miss Tz ni issue amabyo haiwezi kufutika kwasababu kaolewa sasa!

Yeye bado ni kama nembo ya TAIFA na kama vile mumewe anavyowawakilisha wananchi buneni...Basi na yeye aliuwakilisha Duniani na alibeba bebdera ya Taifa kwa niaba yetu watanzania na Amiri Jeshi wetu mkuu!

Ni position amabyo inakwenda na responsibilities!

Hivyo kuwa makini ni SUALA LA MUHIMU HASWA INAPOKUJA KUWATUMIKIA WANANCHI.

There is a scarcity of commonsense amid the abundance of nonsense!

Asha
 
Jmushi,

Argue, don't shout!

1. Miss Tanzania ni Richa Adhia, au we unae wa kwako sasa?

2. Lazaro hajachukua yeye, zimechukuliwa kwa ajili yake na viongozi wake wa CCM. Hivyo ni ishara ya CCM kuwa Chama Cha Mafisadi.

Dr Slaa hapa amemtumia Lazaro na Miss wake kuanika tu ufisadi uliopo huko Singida wa fedha za wananchi.

That said: I insist Lazaro ana ufisadi mkubwa zaidi ya huo.

Asha

Wewe ndio umesema najichanganya..Nani kajichanganya?
Dr Slaa kazungumzia arusi ya Hao kina Lazaro..Na wewe unasema ni ccm!
Sasa ni arusi ya ccm na mafisadi wa chadema?
Acha hizo wewe hata kama mna tofauti humo ndani ya chama jaribu kutumia hekima!
Hapa unadai ni ccm..Sasa huyo lazaro ni mwakilishi huko bungeni kwa kupitia tiketi ya chadema ama ccm?
Kwanini kumekuwa na mgawanyiko mkubwa hivyo humo chadema?
Yani wewe ni heri usungekuwa mwakilishi wa chadema kwasababu sasa nimeshagunduwa kuwa hufai!
 
There is a scarcity of commonsense amid the abundance of nonsense!

Asha

Mi naona urudi tu kwenye ile thread yako ya madai ya Mpaka Kieleweke si MBOWE!

Na baada ya hapo...mwombe Slaa aje hapa kutowa ufafanuzi kama kweli wewe ni chadema!

Mimi sikusikilizi wewe wala huyo kieleweke!

Kwasasa ni Slaa na Zitto.

Wengine kama nyie mnatia shaka kwasababu mko ki upambe upambe!

MAENDELEO YA NCHI NA UKOMBOZI WA KWELI HAVILETWI NA UPAMBE WA MIPASHO...Bali FACTS!
 
Back
Top Bottom