Lazaro Nyalandu arudi rasmi Chama cha Mapinduzi akitokea CHADEMA

johnthebaptist

JF-Expert Member
May 27, 2014
83,915
141,870
Lazaro Nyalandu wa CHADEMA amerejea CCM kupitia mkutano mkuu wa CCM leo jijini Dodoma.

Nyalandu aliyekuwa mjumbe wa Kamati Kuu ya CHADEMA amesema walikuwa wamechukuliwa na walilazimishwa kumwimbia bwana lakini wao pamoja na mzee Lowassa, Sumaye na Dkt. Slaa wamegoma kuimba kwani bwana yuko CCM peke yake.

Nyalandu ameiomba radhi CCM na amewashukuru kwa kumpokea tena.

Kadhalika mwenyekiti wa CHADEMA mkoa wa Lindi Dkt. Suleiman Methew naye amerejea CCM alikokuzwa kisiasa.

Kazi Iendelee.

Nyalandu.jpg

PIA, SOMA=> Mbunge wa Singida Kaskazini, Lazaro Nyalandu ajivua Ubunge; ajitoa CCM na kuomba kujiunga CHADEMA
 
Back
Top Bottom