Lawama za nini???

The Son

JF-Expert Member
Jul 30, 2012
459
58
Miongoni mwa ndugu, jamaa na marafiki wanaoishi mbali mbali yupo ambaye analazimika kuwajulia wenzake hali au yeyote anaweza kumjulia hali mwingine?
Nahitaji kujuzwa maana wapo wanaoona kuwa fulani ndiye anapaswa kutujulia hali. Kwa upande wangu naona si vibaya kwa yeyote ambaye atapata fursa kuwajulia hali wenzake. Sioni kama kuna haja ya kumtupia mtu lawama kuwa hakujulii hali wakati wewe pia unakaa kimya. Mara nyingi nikiulizwa swali la kwanini unakuwa kimya sana nalijibu kwa swali sababu anayeniuliza ana uwezo na majukumu kama mimi sasa iweje atake mimi tu nimjulie hali? Kwa nini naye asinijulie hali siku nyingine akiona niko kimya badala yake anabaki kulaumu tu? Mtu hujanipigia simu nikaacha kupokea wala hujanitumia sms nikaacha kuijibu. Pia hujanibipu nikaacha kukupigia... lawama za nini?

QUOTE]Lawama si mzigo[QUOTE
 
Back
Top Bottom