Tatizo ni Rais Samia, acheni kuwabebesha lawama wateule wake!

MsemajiUkweli

JF-Expert Member
Jul 5, 2012
13,171
23,976
Ukiangalia historia ya Marais nchini utagundua kuwa Marais dhaifu hutengeneza mazingira ya kuwabebesha lawama wateule wao. Kikubwa zaidi, viongozi dhaifu wana hulka ya unafiki.

Mwanasiasa mnafiki huepuka kuongelea masuala makubwa hadharani yanayoligawa taifa na pia huepuka kutoa maamuzi hadharani kwenye masuala yenye mabishano makubwa kitaifa.

Mara nyingi maneno na matendo kwa mwanasiasa mnafiki huwa hayaendani. Anachokisema ni tofauti na anachokitenda.

Mwanasiasa mnafiki ana hulka ya kutaka kupendwa na makundi yote ya kijamii.

Ikumbukwe kuwa Mwanasiasa mwadilifu(statesman) hutaka makundi yote ya kijamii yajue msimamo wake hata kwenye masuala makubwa yenye ubishani kitaifa. Kwa mantiki hii, mwanasiasa mnafiki hawezi kuwa mwadilifu.

Wakati wa utawala wa Rais Kikwete ambaye anajulikana alikuwa dhaifu katika maamuzi, wateule wake walibebeshwa lawama mpaka wengine kulazimishwa kujiuzulu. Unafiki wake ilikuwa ni njia ya kuepuka lawama. Alikuwa anajifanya mbele ya wananchi kuwa hajawatuma wateule wake kufanya walichokifanya ili asionekane mwenye makosa lakini ukweli alikuwa anawatuma. Wateule wake wakawa wanabebeshwa lawama ambazo kimantiki zilitakiwa zielekezwe kwa Rais Kikwete.

Yaliyotokea kwa Rais Kikwete kwa sasa inaonekana yameanza kujitokeza pia katika utawala huu!

Kwa sasa utawasikia baadhi ya watu wakisema eti Rais Samia anashauriwa vibaya! Wengine wakisema Rais Samia amezungukwa na kundi la watu wasiomtakia mema! Hii yote ni kujaribu kuficha udhaifu na unafiki wake. Hawa wanayasema yote kwa kujua au bila kujua kuwa katiba yetu ya Tanzania na Katiba ya CCM inampa madaraka ya “kifalme” Rais na pia Mwenyekiti CCM. Rais ana uwezo kikatiba wa kufukuza na kuteua mtu yeyote bila kuhojiwa na yeyote/au taasisi yeyote.

Fikiria jinsi ambavyo Waziri Mwigulu Nchemba alivyolaumiwa eti ndiye aliyeleta tozo mbali mbali kama vile hiyo sheria ya tozo haikupitia kwenye vikao vya baraza la mawaziri na kuidhinishwa na Rais, lakini kikubwa zaidi sheria zetu zinasema hakuna muswada wowote wa fedha utapelekwa kwenye bunge la Tanzania bila ridhaa ya Rais wa Tanzania. Hoja yangu sio kumtetea Mwigulu lakini jiulize, kwa nini mpaka leo Mwigulu bado ni waziri wa fedha kama anayotafanya hatumwi na Rais kuyafanya?

Kama Rais asingekuwa ameweka saini yake kwenye mkataba wa serikali na DP World ninaamini angekuwa ameishamkana na kumwangushia “zigo” Waziri wa ujenzi ma Uchukuzi, Prof. Mbarawa na kudai hakumtuma au amempotosha. Huu mkataba “umemvua” nguo ya unafiki na kumuacha “uchi” kisiasa kwa sababu hawezi kuukana wakati kuna saini yake.

“Chawa” wake wanashindwa wamwangushie mzigo wa lawama nani ili kumnusuru Rais. Kwa sasa wanachofanya ni kuanza kuwalaumu viongozi wengine wa juu huku wakisema, Kwa nini Makamu wa Rais na Waziri Mkuu hawautetei kwa nguvu zote Mkataba wa DP World? Wanadai wanamgomo baridi!

Suala la katiba mpya ni unafiki mwingine wa Rais Samia. Tukumbuke alipopata madaraka kwa njia ya “urithi” alijitokeza hadharani na kudai suala hilo atalishughulukia! Rais aliunda “kikosi kazi” ambacho hakikuwa hata na hadidu za rejea. Kwa mtu anayejua hulka za mtu mnafiki lazima alijua ule ulikuwa ni usanii wa kutaka mapendo kwa kundi linalotaka katiba mpya lakini pia kununua muda kwa njia ya usanii. Kikosi kazi kilifanya/kunafanya kazi ambayo kwa mtu anayezifahamu siasa za Tanzania anajua majawabu ya kile ambacho kikosi kazi kilikuwa kinatafuta kwa umma wa Watanzania.

Katiba ambayo ndio imemfanya kupata Urais wa “urithi” eti leo hii Rais Samia anatuambia Watanzania ni karatasi tu! Hizi ndizo hulka za mwanasiasa mnafiki.

Kuna msemo usemao, njia ya muongo na mnafiki ni fupi. Hii ina maana kuwa muongo na mnafiki huweza kugundulika kwa urahisi sana. Leo hii tumegundua suala la katiba mpya ilikuwa ni usanii ili kununua muda!

Tusije kushangaa tukisikia CHADEMA wanalaumiwa na Rais Samia kwa “kukwamisha” mchakato wa katiba mpya kwa sababu wamekataa kushirikiana na kikosi kazi! Hii yote ni kutaka kuepuka wajibu/majukumu yake kwa sababu wanasiasa wanafiki hawapendi kuchukua majukumu yao na kuyafanyia kazi kama inavyotakiwa.

Mnakumbuka tuliambiwa fedha zote za mikopo zitakuwa zinawekwa wazi matumizi yake! Mpaka sasa limefanyika mara ngapi? Serikali mpaka sasa imekopa mara ngapi na kiasi gani kimekopwa?

If you wear a face mask for too long, there will come a time when you can not remove it without removing your face.

The president is removing a face mask with her face!

Kama unapenda kuujua zaidi uongozi wa Rais Samia soma hii thread; Gonga hapa chini:-

Kwa Rais huyu, CCM wana hali mbaya sana!
 
IMG_0217.jpg
 
Ukiangalia historia ya Marais nchini utagundua kuwa Marais dhaifu hutengeneza mazingira ya kuwabebesha lawama wateule wao. Kikubwa zaidi, viongozi dhaifu wana hulka ya unafiki.

Mwanasiasa mnafiki huepuka kuongelea masuala makubwa hadharani yanayoligawa taifa na pia huepuka kutoa maamuzi hadharani kwenye masuala yenye mabishano makubwa kitaifa.

Mara nyingi maneno na matendo kwa mwanasiasa mnafiki huwa hayaendani. Anachokisema ni tofauti na anachokitenda.

Mwanasiasa mnafiki ana hulka ya kutaka kupendwa na makundi yote ya kijamii.

Ikumbukwe kuwa Mwanasiasa mwadilifu(statesmano) hutaka makundi yote ya kijamii yajue msimamo wake hata kwenye masuala makubwa yenye ubishani kitaifa. Kwa mantiki hii, mwanasiasa mnafiki hawezi kuwa mwadilifu.

Wakati wa utawala wa Rais Kikwete ambaye anajulikana alikuwa dhaifu katika maamuzi, wateule wake walibebeshwa lawama mpaka wengine kulazimishwa kujiuzulu. Unafiki wake ilikuwa ni njia ya kuepuka lawama. Alikuwa anajifanya mbele ya wananchi kuwa hajawatuma wateule wake kufanya walichokifanya ili asionekane mwenye makosa lakini ukweli alikuwa anawatuma. Wateule wake wakawa wanabebeshwa lawama ambazo kimantiki zilitakiwa zielekezwe kwa Rais Kikwete.

Yaliyotokea kwa Rais Kikwete kwa sasa inaonekana yameanza kujitokeza pia katika utawala huu!

Kwa sasa utawasikia baadhi ya watu wakisema eti Rais Samia anashauriwa vibaya! Wengine wakisema Rais Samia amezungukwa na kundi la watu wasiomtakia mema! Hii yote ni kujaribu kuficha udhaifu na unafiki wake. Hawa wanayasema yote kwa kujua au bila kujua kuwa katiba yetu ya Tanzania na Katiba ya CCM inampa madaraka ya “kifalme” Rais na pia Mwenyekiti CCM. Rais ana uwezo kikatiba wa kufukuza na kuteua mtu yeyote bila kuhojiwa na yeyote/au taasisi yeyote.

Fikiria jinsi ambavyo Waziri Mwigulu Nchemba alivyolaumiwa eti ndiye aliyeleta tozo mbali mbali kama vile hiyo sheria ya tozo haikupitia kwenye vikao vya baraza la mawaziri na kuidhinishwa na Rais, lakini kikubwa zaidi sheria zetu zinasema hakuna muswada wowote wa fedha utapelekwa kwenye bunge la Tanzania bila ridhaa ya Rais wa Tanzania. Hoja yangu sio kumtetea Mwigulu lakini jiulize, kwa nini mpaka leo Mwigulu bado ni waziri wa fedha kama anayotafanya hatumwi na Rais kuyafanya?

Kama Rais asingekuwa ameweka saini yake kwenye mkataba wa serikali na DP World ninaamini angekuwa ameishamkana na kumwangushia “zigo” Waziri wa ujenzi ma Uchukuzi, Prof. Mbarawa na kudai hakumtuma au amempotosha. Huu mkataba “umemvua” nguo ya unafiki na kumuacha “uchi” kisiasa kwa sababu hawezi kuukana wakati kuna saini yake.

“Chawa” wake wanashindwa wamwangushie mzigo wa lawama nani ili kumnusuru Rais. Kwa sasa wanachofanya ni kuanza kuwalaumu viongozi wengine wa juu huku wakisema, Kwa nini Makamu wa Rais na Waziri Mkuu hawautetei kwa nguvu zote Mkataba wa DP World? Wanadai wanamgomo baridi!

Suala la katiba mpya ni unafiki mwingine wa Rais Samia. Tukumbuke alipopata madaraka kwa njia ya “urithi” alijitokeza hadharani na kudai suala hilo atalishughulukia! Rais aliunda “kikosi kazi” ambacho hakikuwa hata na hadidu za rejea. Kwa mtu anayejua hulka za mtu mnafiki lazima alijua ule ulikuwa ni usanii wa kutaka mapendo kwa kundi linalotaka katiba mpya lakini pia kununua muda kwa njia ya usanii. Kikosi kazi kilifanya/kunafanya kazi ambayo kwa mtu anayezifahamu siasa za Tanzania anajua majawabu ya kile ambacho kikosi kazi kilikuwa kinatafuta kwa umma wa Watanzania.

Kuna msemo usemao, njia ya muongo na mnafiki ni fupi. Hii ina maana kuwa muongo na mnafiki huweza kugundulika kwa urahisi sana. Leo hii tumegundua suala la katiba mpya ilikuwa ni usanii ili kununua muda!

Tusije kushangaa tukisikia CHADEMA wanalaumiwa na Rais Samia kwa “kukwamisha” mchakato wa katiba mpya kwa sababu wamekataa kushirikiana na kikosi kazi! Hii yote ni kutaka kuepuka wajibu/majukumu yake kwa sababu wanasiasa wanafiki hawapendi kuchukua majukumu yao na kuyafanyia kazi kama inavyotakiwa.

Mnakumbuka tuliambiwa fedha zote za mikopo zitakuwa zinawekwa wazi matumizi yake! Mpaka sasa limefanyika mara ngapi? Serikali mpaka sasa imekopa mara ngapi na kiasi gani kimekopwa?

If you wear a face mask for too long, there will come a time when you can not remove it without removing your face.

The president is removing a face mask with her face!

Kama unapenda kuujua zaidi uongozi wa Rais Samia soma hii thread; Gonga hapa chini:-

Kwa Rais huyu, CCM wana hali mbaya sana!
umepita mulemule Kamanda the problem is samia not somebody else
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom