LATRA wapo kwa niaba ya nani?

Abou Shaymaa

JF-Expert Member
Oct 19, 2022
501
1,025
Wakuu nauliza hawa LATRA alieanzisha aliiweka kwa niaba ya nani? Wafanya biashara wa magari au kwaniaba ya wananchi?

Mimi nina uhakika ipo kwaajili ya wafanya biashara wala si wananchi, kwasababu; mafuta yakipanda tu wafanyabiashara wanapiga kelele nauli ipande nao (LATRA) wanapandisha nauli.

Je, imeshawahi kutokea mafuta yameshuka bei wananchi wakalalamika na LATRA wakashusha bei? Au malalamiko ya wananchi hayawafikii yanafika ya wafanyabiashara wa magari tu? Au upole wetu unawapa jeuri wanatuchukulia sisi wananchi sawa na ng'ombe?

Na kuna watu walijitia wanathamin sana maslahi ya wananchi hapa wakasoma waraka kila jpili hivi hili nalo hawalioni? au kwa kuwa halina maslahi na wao?

Yaani nimeenda kukata tiketi leo ambapo nikilipa 25000 ikapanda ikafika 35000 sasa hivi 42000 na LATRA wapo kimya kama hawapo au wao wapo kwaajili ya wafanyabiashara tu?

Nawasilisha kwa uchungu kwasababu kuna wanaojifanya watetezi wa wananchi ila wao utetezi wao kwenye vitu vyenye maslahi na wao tu hawana ukweli wowote

Nawasilisha.
 
Au upole wetu una wapa jeur wanatuchukulia sisi wananchi sawa na ng'ombe?
Wananchi wa Tanzania ni kheri kwao kulalamika lakini sio kuwa wajibisha viongozi wao.
Na sijui hii linasababishwa na nini?
Ndio maana viongozi wana amua wanachotaka wao, kwasababu wanajua jamii wanayoiongoza haiwezi kuhoji.
 
Wakuu nauliza hawa LATRA alieanzisha aliiweka kwa niaba ya nan? Wafanya biashara wa magari au kwaniaba ya wananchi?

Mimi nina uhakika ipo kwaajili ya wafanya biashara wala si wananchi,
Kwasababu

• Mafuta yakipanda tu wafanya biashara wanapiga kelele nauli ipande nao(LATRA) wanapandisha nauli,

• Je ishawahi kutokea mafuta yameshuka bei wananchi wakalalamika na LATRA wakashusha bei?

Au malalamiko ya wananchi hayawafikii yanafika ya wafanyabiashara wa magari tu?

Au upole wetu unawapa jeuri wanatuchukulia sisi wananchi sawa na ng'ombe?

Na kuna watu walijitia wanathamin sana maslahi ya wananchi hapa wakasoma waraka kila jpili hivi hili nalo hawalioni? au kwa kuwa halina maslahi na wao?

Yaani nimeenda kukata tiketi leo ambapo nikilipa 25000 ikapanda ikafika 35000 sasa hivi 42000 na LATRA wapo kimya kama hawapo au wao wapo kwaajili ya wafanyabiashara tu?

Nawasilisha kwa uchungu kwasababu kuna wanaojifanya watetezi wa wananchi ila wao utetezi wao kwenye vitu vyenye maslahi na wao tu hawana ukweli wowote

Nawasilisha
Laiti ungekuwa unamiliki gari ukutane na kero za LATRA usingeandika haya
 
Kero ipi ya kupandishiwa nauli au ipi
Faini zisizo na msingi, kufungiwa bila Kusikilizwa, kulazimika kutoza nauli ndogo hata bei ya mafuta na vipuri ikiwa juu sana. Kutikutimiziwa mambo yaliyo chini yao kwa wakati. Kwa mfano niliomba kuunganishwa kwenye mifumo wa VTS kwa gari nne toka mwezi wa 11 2023 ila mpaka leo ninazungushwa kupatiwa akaunti. Yaani gari zina ving'amuzi tayari ila sina uwezo za kufuatilia mwenendo wake. Unapewa kibali Mkoa A lakini ukiwa Mkoa C unapigwa Faini ya kutokuwa na kibali.
Nunua gari ya abiria utanielewa.
 
Sawa mkuu kwahy baada ya kupanda nauli imefidia hayo matatizo yote?
 
Haijafifia na wala haina msaada sana kwetu. Kiuhalisia tunachaji bei za amani kwa asilimia kubwa. LATRA wao wanapanga kiwango cha juu na sisi tunatumia busara kuweka nauli inayoendana na wateja wetu. Ukikutana na sarange wa stand ndio watakuchaji bei ya LATRA. Mara nyingi kaka tie tiketi kwenye Ofisi rasmi za kampuni.
 
Wananchi wa Tanzania ni kheri kwao kulalamika lakini sio kuwa wajibisha viongozi wao.
Na sijui hii linasababishwa na nini?
Ndio maana viongozi wana amua wanachotaka wao, kwasababu wanajua jamii wanayoiongoza haiwezi kuhoji.
Uwoga, nchi ina vijana waoga waoga sanaa, na pia hawapendi heka heka au changamoto...
 
Wakuu nauliza hawa LATRA alieanzisha aliiweka kwa niaba ya nani? Wafanya biashara wa magari au kwaniaba ya wananchi?

Mimi nina uhakika ipo kwaajili ya wafanya biashara wala si wananchi, kwasababu; mafuta yakipanda tu wafanyabiashara wanapiga kelele nauli ipande nao (LATRA) wanapandisha nauli.

Je, imeshawahi kutokea mafuta yameshuka bei wananchi wakalalamika na LATRA wakashusha bei? Au malalamiko ya wananchi hayawafikii yanafika ya wafanyabiashara wa magari tu? Au upole wetu unawapa jeuri wanatuchukulia sisi wananchi sawa na ng'ombe?

Na kuna watu walijitia wanathamin sana maslahi ya wananchi hapa wakasoma waraka kila jpili hivi hili nalo hawalioni? au kwa kuwa halina maslahi na wao?

Yaani nimeenda kukata tiketi leo ambapo nikilipa 25000 ikapanda ikafika 35000 sasa hivi 42000 na LATRA wapo kimya kama hawapo au wao wapo kwaajili ya wafanyabiashara tu?

Nawasilisha kwa uchungu kwasababu kuna wanaojifanya watetezi wa wananchi ila wao utetezi wao kwenye vitu vyenye maslahi na wao tu hawana ukweli wowote

Nawasilisha.
latra haipo kwajili ya wafanya biashara wa magari wala wananchi,iyo ipo kwajili ya serikali mkuu ndio mana kama unakumbukumbu nzuri baada ya sumatra tu kuanzishwa scandnavia nayo ikaanza kupotea
 
Back
Top Bottom