LATRA wanasita nini kutangaza 'level seat' kwenye daladala?

johnthebaptist

JF-Expert Member
May 27, 2014
41,839
2,000
Naelewa kwamba wametangaza social distance kwenye ya mita 1 kwenye stendi za daladala kama pale Makumbusho na Mbagala.

Sidhani kama hiyo inasaidia lolote kama ndani ya basi watu wanakanyagana.

Maendeleo hayana vyama
 
MastaKiraka

JF-Expert Member
Jan 10, 2015
1,497
2,000
Na Mikutano/Ziara ya/Za JPM Izingatie hili pia, Maana unaweza ukaminya Kwenye usafiri wa Umma Alafu ukaachia Kwenye Mikutano n.k Ikawa ni kazi bure
 
Matrix19

JF-Expert Member
Feb 24, 2020
1,658
2,000
Mfalme anaendeleza Ziara zenye mikusanyiko isiyo na barakoa LATRA watasemaje zaidi ya kufyata mkia?
 
GODZILLA

JF-Expert Member
Dec 26, 2014
5,722
2,000
Sio tu kwa sababu ya corona, lakini level seat ni muhimu pia kwa usalama wa maisha ya watu!

Unakuta gari limejaa watu wamesokomezwa ndani kama nyumbu wanapumua juu juu!

Ni biashara gani hiyo isiyojali maisha na utu wa watu?

Inashangaza sana! Ni pesa ndiyo inayotafutwa kwa namna hiyo?

Sijui ni kwanini tu serikali inawaacha hawa!? It is very risky and dangerous!

Mijitu inabambiana tu humo, wenye pumu na nimonia nao humo humo. Tuberculosis na makorona nayo humo humo!

Ikitokea ajali ndio kabisaaa.... ni kama kiama.
 
Babati

JF-Expert Member
Aug 7, 2014
41,304
2,000
Sasa jamaa yangu haya mambo ukiyafikiria kwa undani hayana maana.Fikiria hili:
Nimepanda level seat mbagala naelekea kazini Kariakoo shimon..unakua ume solve nini?!
Utakuwa umepunguza risk, inawezekana ukapata kwenye daladala na kwenye shimo usipate au kinyume chake
 
UPOPO

JF-Expert Member
Dec 17, 2010
2,913
2,000
Hatutafika uchumi wa kati ,maana tunajali uchumi wa kati nyie mfe tu kwani kuna shida kasema mwenye nchi jamani sio mimi.Ila Mungu mwache aitwe Mungu yapo yanayokuja yanafurahisha
 
ukikaidi utapigwa2

JF-Expert Member
Feb 24, 2015
1,343
2,000
Sio tu kwa sababu ya corona, lakini level seat ni muhimu pia kwa usalama wa maisha ya watu!

Unakuta gari limejaa watu wamesokomezwa ndani kama nyumbu wanapumua juu juu!

Ni biashara gani hiyo isiyojali maisha na utu wa watu?

Inashangaza sana! Ni pesa ndiyo inayotafutwa kwa namna hiyo?

Sijui ni kwanini tu serikali inawaacha hawa!? It is very risky and dangerous!

Mijitu inabambiana tu humo, wenye pumu na nimonia nao humo humo. Tuberculosis na makorona nayo humo humo!

Ikitokea ajali ndio kabisaaa.... ni kama kiama.
Kunywa beer na kitimoto bill kwangu
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom