Ushirombomoya
Member
- May 11, 2021
- 61
- 101
Naanza kwa kutambua mchango wa usafiri katika kusukuma gurudumu letu zito la maendeleo linaloenda kwa mwendo wa kusuasua, ila yote heri ili mradi gurudumu linasonga mbele, usafiri wa daladala utusaidia sana wakazi wa miji mikubwa nchini maana utuwezesha kufika katika maeneo yetu tunayojipatia mkate wetu wa kila siku, usafiri huu sio tu ni msaada kwa wengi wetu tusiokuwa na uwezo wa kumiliki usafiri binafsi lakini kwa nyakati tofauti umekuwa msaada hata kwa wale waliojaliwa kuwa na usafiri binafsi pale inapowabidi kuutumia usafiri huu. Natambua kuwa LATRA ndio taasisi inayoshughulikia suala zima la usafirishaji Nchini ila nimekuwa nikijuliza ni vigezo gani wanavyotumia kuwapatia wamiliki wa daladala" routes" maeneo mbalimbali ya jiji la Dar es Salaam maana kuna maeneo yana uhitaji mkubwa hili yamepewa idadi ndogo ya magari yanayotoauduma katika maeneo hayo mfano Bunju Sokoni- Morroco hii ni route yenye magari machache lakini ni yenye wahitaji wengi. kwa sababu ya uchache wa magari kero/matukio mbalimbali yakuhuzunisha yamekuwa yakitokea kama nitakavyoonyesha hapa chini:
- UharifuKutokuwepo kwa idadi ya daladala inayoenda na uhitaji, kuna tunalazimu wakazi wengi wa Bunju tunaotumia route ya Bunju- Morocco kudamka mapema kupita kiasi hili kujaribu kupata daladala, wakazi wengi wanaojishughulisha na shughuli mbalimbali pia wanafunzi waume kwa wake tumekuwa tukiamka mida ya saa tisa au saa kumi usiku, kumbuka muda huo bado kunakuwa na kiza hivyo waharifu wamekuwa wakipata mwanya wa kutenda matukio mbalimbali ikiwemo uporaji wa mali, ubakaji na aina nyinginezo za uharifu, matukio mengi ya uharifu yamekuwa yakitokea muda huo, matukio hayo yamewaacha watu wengi na hasara kwa kupoteza vitu vyao vya thamani, utu wao na kuna kipindi imesharipotiwa kwa watu kupoteza uhai. Idadi ndogo ya magari licha ya kutufanya wakazi wa Bunju kuamka mapema lakini suala hili la kuamka kwa wakati mwingine limekuwa halisaidii sana maana tumekuwa tukisubiri muda mrefu vituoni tukisubiri magari ambayo uja moja moja lakini kinachoshangaza route nyingine kama Bunju- kawe, Bunju- Sim 2000 zina magari mengi na mara nyingi zimekuwa zikienda tupu asubuhi, hapa ndio swali langu lilipo je ni kigezo gani utumika kugawa hizi routes.
2. Migogoro ya ndoa na kijamii kwa ujumla
Mnaweza kusema ninalikuza jambo hili, ila hakika nawaambia mara kwa mara ndoa nyingi huku zimekuwa zikiwekwa majaribuni na uchache wa daladala hususani route ya Bunju- Morocco, kutokana na kutokuwepo kwa idadi inayoendana na mahitaji kumesababisha wake kwa waume kuchelewa kufika majumbani kwa wakati jambo hili uleta ukakasi kwa wake na waume ambao mara nyingi uhisi kuibiwa, lakini wake pia wamekuwa wakishindwa kutimiza majukumu ya msingi, mfano saa kumi jioni ikiwakuta wakiwa Morocco kupata gari la Bunju masaa matatu au zaidi yanaweza kupita na hapo wamepambana kweli kweli, hadi kufika Bunju wanaweza kupoteza masaa mengine matatu au zaidi kutokana na foleni ya magari njiani, hivyo wakazi wengi wa njia hii tunaingia majumbani usiku sasa hapa tujiulize mke anatafanya majukumu ya msingi ya ndoa kama vile kupika na mengineyo saa ngapi, kwa hali hii uhai wa ndoa utakuwepo kweli?
3. kunasababisha gharama mara dufu za usafiri
Kama nilivyokwisha kusema hapo juu wakazi wengi tunaotumia route ya Bunju- Morocco licha ya kwamba tunaamka mapema ili kuwahi kupata usafiri wa umma lakini mara nyingi tumekuwa tukitumia muda mrefu sana hadi kupata magari hii inatokana na uchache wa magari hayo ukilinganisha na route nyingine, kwa sababu hiyo wakazi wa Bunju tumekuwa tukilazimika kutumia fedha zaidi kwa kutumia aina nyingine za usafiri au kapanda magari mawili yaani safari ya Bunju- Morocco inakulazimu upande gari la Bunju- Makumbusho halafu tena upande gari la posta, hali hii usababisha gharama na upotevu wa muda.
Ushauri kuepukana na kadhia tajwa hapo juu
kama nilivyoeleza changamoto mbalimbali zinazotukumba wakazi wa tunaotumia route ya Bunju- Morocco, japo ninatambua fika sio tu wakazi wa route hii ndio upata matatizo hayo naamini kuna maeneo mengine nao wana changamoto ya uchache wa daladala, hivyo ushauri nitakaoutoa hapa unaweza kwa namna moja au nyingine kusaidia kutatua tatizo hilo.
1. Kabla ya kugawa route utafiti ufanyike
kwa hali iliyopo sasa naamini ugawaji wa route hauongozwi na tafiti ambazo zingewawezesha LATRA na taasisi husika kugawa route kwa kuzingatia uwiano wa wahitaji na sio kama ambavyo ilivyo sasa, mji wa Dar es Salaam unakuwa kwa kasi, maeneo ambayo zamani yalikuwa yanakaliwa na watu wachache hizi sasa yana watu wengi sasa route zikigawanywa kwa kuzingatia tafiti za zamani naamini hali itaendelea kuwa tete kila kukicha, hivyo ni wakati sasa kwa LATRA kufanya tafiti ili kuangalia kama idadi ya magari inaakisi uhitaji uliopo na sio kufanya kazi kinadharia au kwa kukisia.
2. LATRA itoe idhini kwa magari ya route nyingine kutoa huduma
Mara nyingi nimekuwa nikiona daladala ambazo zipo kwenye route zenye watu wachache zikiiba route na kuchukua abiria wa Bunju- Morocco, hali hii inaonyesha sio tu kwamba route ya Bunju- Morocco ina wahitaji wengi lakini inatoa picha kwamba kuna route nyingine hazina watu wengi na ndio maana unaweza kuziona zikijaribu hata kuiba route ili kupata abiria hususani kwa kubeba abiria wa Bunju, kutokana na hali hii ninapendekeza LATRA waruhusu gari zinazofanya kazi ya usafirishaji kwenye maeneo yenye watu wachache zichukue abiria wa Bunju mida ya asubuhi na jioni kutupunguzia kadhia.
Mwisho: Maendeleo bila kuwa na usafiri wa umma wa uhakika ni vigumu kupatikana, usafiri wa uhakika utoa fursa ya kushiriki kikamilifu katika shughuli mbalimbali za uzalishaji mali na maendeleo kwa ujumla, hivyo ni vyema serikali kupitia vyombo vyake mbalimbali wakatupia macho jambo hili. Usafiri wa uhakika uwezesha watu kufika maeneo ya kazi kwa wakati, pia usisimua shughuli nyingine mbalimbali za kiuchumi, ni ndoto za abunuasi kuhubiri maendeleo ya haraka wakati hauna usafiri wa uhakika.