Kilimanjaro: Ni lazima Abiria kuvaa Barakoa na Daladala zote zibebe Level seat

Miss Zomboko

JF-Expert Member
May 18, 2014
4,499
9,279
Moshi. Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Stephen Kagaigai amepiga marufuku abiria wanaoingia ndani ya daladala na mabasi yaendayo mikoani kutoruhusiwa kuingia bila kuvaa barakoa ili kupunguza maambukizi ya ugonjwa wa corona.

Agizo hilo amelitoa leo Julai 29, 2021 mkoani hapa huku akiwataka madereva wa mabasi pamoja na daladala kuhakikisha abiria hawasimami ndani ya gari pamoja na kuhakikisha abiria wote wanakaa.

“Ni lazima anayeingia kwenye mabasi awe amevaa barakoa, lakini pia hakuna kusimamisha abiria lazima wakae ‘level seat’ na nimeshamwelekeza Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kilimanjaro amwagize kamanda wake wa kikosi cha usalama barabarani wawe makini kwenye hilo,”amesema Kagaigai.

“Dereva atakayekwenda kinyume na hilo na kuondoka stendi na abiria ambaye hajavaa barakoa lazima wafauatiliwe na hatua zichukuliwe na hii tunafanya kwa nia nzuri kwa ajili ya kutunza afya za wananchi wetu, Serikali inapenda wananchi wake wawe na afya njema ili waweze kuzalisha,”amesema Kagaigai.

“Tunamshukuru sana Rais wetu Samia Suluhu Hassan kwa kutupigania na kutuletea chanjo, lakini wakati huu tukisubiri kwenye maeneo yetu tuletewe chanjo endeleeni kuchukua tahadhari zote zinazotolewa na wizara ya afya,”amesema.

Mwananchi
 
Barakoa inatekelezeka lakini kusimama, mh! Unaondoaje kusimama hapa TZ ,kwa mfano? Tayari mna mabasi ya kutosha au matreni yanayokwenda kwa muda maalumu au bado staili ni hiihii tuliyonayo sasa? Hapo unataka kuwapiga virungu wanaopandia njiani
 
Kusema ule ukweli maambukizi ya Corona na haswa Mkoa wa Kilimanjaro yako juu na vifo vimekuwa vingi sana
 
Miss Zomboko najua kuwa huenda umekopi na ku-paste tu hii habari lakini kwenye aya ya kwanza ni makosa matupu. Wanasema ''amepiga marufuku abiria wanaoingia ndani ya daladala na mabasi yaendayo mikoani kutoruhusiwa kuingia bila kuvaa barakoa''. Yaani amepiga marufuku wasikatazwe kuingia bila barakoa!
 
Barakoa inatekelezeka lakini kusimama, mh! Unaondoaje kusimama hapa TZ ,kwa mfano? Tayari mna mabasi ya kutosha au matreni yanayokwenda kwa muda maalumu au bado staili ni hiihii tuliyonayo sasa? Hapo unataka kuwapiga virungu wanaopandia njiani
Kipindi kile walivyoweka level seat ilikuwa unaweza kukaa kituoni hadi masaa matatu kulikuwa na usumbufu sana, tatizo serikali wao wanatoa matamko tu mengine mtajua wenyewe.
 
Kipindi kile walivyoweka level seat ilikuwa unaweza kukaa kituoni hadi masaa matatu kulikuwa na usumbufu sana, tatizo serikali wao wanatoa matamko tu mengine mtajua wenyewe.
Bila hata kuwa na korona, usafiri wa daladala unatakiwa usimamiwe ili abiria wasilundikwe tena. Wakisimamia hili la mabasi kutojaza skupita kiasi, siku za mwanzo mwanzo zinaweza kuwa za shida, lakini baada ya muda mambo yataji-adjust yenyewe na hali itarudi kawaida. Kivipi. Daladala hazitachelewa tena vituoni hivyo frequency za safari zitaongezeka, na pia watu wengi zaidi wataingiza magari kwenye hii biashara.
 
Basi wazuie hakuna kutoka wala kuingia huko Kilimanjaro na wapime watu corona.
Raisi wetu mpendwa Samia Suluhu Hassan ni msikivu tunamuomba Watu waanze kupimwa papo kwa hapo katika Mikoa inayoonekana kuwa na maambukizi mengi ili hatua nyingine zifuate
 
Raisi wetu mpendwa Samia Suluhu Hassan ni msikivu tunamuomba Watu waanze kupimwa papo kwa hapo katika Mikoa inayoonekana kuwa na maambukizi mengi ili hatua nyingine zifuate
Ni kweli msikivu ila sio mtendaji bali ni mzungumzaji tu.
 
Bila hata kuwa na korona, usafiri wa daladala unatakiwa usimamiwe ili abiria wasilundikwe tena. Wakisimamia hili la mabasi kutojaza skupita kiasi, siku za mwanzo mwanzo zinaweza kuwa za shida, lakini baada ya muda mambo yataji-adjust yenyewe na hali itarudi kawaida. Kivipi. Daladala hazitachelewa tena vituoni hivyo frequency za safari zitaongezeka, na pia watu wengi zaidi wataingiza magari kwenye hii biashara.
Walivyowekaga level seat magari yalikuwa yanakuja kituoni ila sasa ndio inachukua wachache kwa sababu ya hiyo level seat na kuwaacha abiria wengi na kadri muda unavyozidi kwenda na watu wanaongezeka kituoni. Hilo la level seat kufanya kuwa endelevu sidhani kama linawezekana kwa Dar labda tu waseme wasisimamishe watu wengi kujazana na shida zetu za usafiri sidhani kwamba suluhisho ni kuongeza magari tena barabarani.
 
Back
Top Bottom