#COVID19 Dar: Daladala zatakiwa kuwa Level Seat, kutakuwa na ziara za kustukiza masokoni

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Feb 24, 2012
5,010
9,874
RC MAKALLA: UVAAJI BARAKOA KWENYE VYOMBO VYA USAFIRI NI LAZIMA

- Awataka LATRA kusimamia Level seat.

- Aelekeza Kamati za Ulinzi na Usalama za Wilaya kusimamia Utekelezaji wa Mwongozo wa Wizara ya Afya

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe. Amos Makalla amewataka Wananchi kuchukuwa tahadhari dhidi ya Ugonjwa wa Corona ambapo amepiga marufuku Wananchi kuingia kwenye vyombo vya usafiri na sehemu za kutoa huduma pasipo kuvaa barakoa.

RC Makalla ametoa maelekezo hayo Kufuatia Mwongozo uliotolewa na Wizara ya Afya ambapo amesema watafanya ziara za kustukiza kwenye Vituo vya Daladala, Feri, Stendi, Mabasi ya Mwendokasi, maeneo ya Masoko na sehemu zote za kutoa huduma ili kuangalia Utekelezaji wa agizo hilo.

Aidha RC Makalla amesema Serikali imejipanga kutoa huduma Bora za matibabu kwa wagonjwa wote watakaofika hospital na kuwataka Wananchi watakaoona dalili za Corona kuwahi vituo vya Afya.

TUNAKULINDA NA WEWE UTULINDE, VAA BARAKOA KWA MUSTAKABALI WA AFYA YAKO NA WENGINE

IMG-20210726-WA0006.jpg
IMG-20210726-WA0007.jpg
IMG-20210726-WA0008.jpg
 
Nimejiwazia tu kimoyo moyo sasa hivi mafuta per lita ni 2400,bosi anataka kipande chake kama kawaida huku na huku dereva na konda wake baada ya kazi wanataka wapate chochote kitu sasa kwakuwataka wapakie level seat wataweza kweli kufanikisha malengo waliojiwekea?

Kwenye hili naona kama tumekurupuka,tulifanikiwa mwaka jana wakati mafuta nayo yalikuwa bei pungufu lita 1500
 
Watu wanakurupuka matamko kila siku. yaani mtu akijisikia anaita media anatoa tamko. Nchi kuongozwa na Mwanamke makosa makubwa sana.

USA na demokrasia yao yote hawajahi kumkabidhi Nchi mwanamke ni rahisi kurubuniwa..wanaipa kiki Corona.
 
Matamko ndiyo yameshatoka utavaa au huvai barakoa? . Polepole utalegea tu mpaka utajipeleka mwenyewe uchanjwe. Unajua kitu kinaitwa SERIKALI
 
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe. Amos Makalla amewataka Wananchi kuchukuwa tahadhari dhidi ya Ugonjwa wa Corona ambapo amepiga marufuku Wananchi kuingia kwenye vyombo vya usafiri na sehemu za kutoa huduma pasipo kuvaa barakoa.

RC Makalla ametoa maelekezo hayo Kufuatia Mwongozo uliotolewa na Wizara ya Afya ambapo amesema watafanya ziara za kustukiza kwenye Vituo vya Daladala, Feri, Stendi, Mabasi ya Mwendokasi, maeneo ya Masoko na sehemu zote za kutoa huduma ili kuangalia Utekelezaji wa agizo hilo.

Aidha RC Makalla amesema Serikali imejipanga kutoa huduma Bora za matibabu kwa wagonjwa wote watakaofika hospital na kuwataka Wananchi watakaoona dalili za Corona kuwahi vituo vya Afya.

TUNAKULINDA NA WEWE UTULINDE, VAA BARAKOA KWA MUSTAKABALI WA AFYA YAKO NA WENGINE
Sijawahi kuona RC kimbunye kama huyu duniani
  1. Kuwataka daladala wapakie level seat tafsiri yake mabasi yaongezwe ili kukidhi mahitaji, wenye mabasi makubwa waliona hiyo changamoto kitambo wakawa wanaendelea na abiria mpaka mjini au kuwaanzishia safari mjini, huyu kimbunye akazuia ili bajaji zake zifanye biashara, sasa haoni maamuzi ya leo yanaongeza mateso kwa wananchi kwa maana ya wale abiria waliosaidiwa na mabasi makubwa wanakwenda kuongeza tatizo kwenye daladala ambazo ni za kugombania, anapata faida gani abiria wanapoteseka? Anapata faida gani mabasi makubwa yanapoondoka matupu huku abiria wakilazimika kwenda kupoteza muda kupigania daladala ambazo kimsingi ni chache?!
  2. Yupo kikaoni anatangaza uvaaji wa barakoa wakati yeye mwenyewe hana barakoa, anazungumzia mambo ambayo yeye mwenyewe ameshindwa kuyaonyeshea ushirikiano ili awe mfano. Bogus kabisa, hana ushirikiano kama meno yake yalivyo.
  3. Tulipendekeza watu wapimwe akili kabla ya kupewa nyadhiva, huyu RC ni shida hatufai wana Dar, si mshirikishaji kwenye decision making
 
Sasa ule wakati ambao kuna viongozi wanaenda kufa ndo huu!

Mnamuacha Mungu na kumpa mwanadamu utukufu!

Mungu ametupigania sna,lkn sshv watu wanajitoa ufahamu km vile Mungu hayupo,sawa! Ngoja tuone mwisho wake!
 
Ziara za kushtukiza alafu unakuja na wapiga picha, online TVs, polisi, walinzi etc. Upuuzi mtupu
 
Ujinga ujinga na ukichaa wa Magu tupa kule kwa Gwajiboy.. Maisha yaendelee
 
Sijawahi kuona RC kimbunye kama huyu duniani
  1. Kuwataka daladala wapakie level seat tafsiri yake mabasi yaongezwe ili kukidhi mahitaji, wenye mabasi makubwa waliona hiyo changamoto kitambo wakawa wanaendelea na abiria mpaka mjini au kuwaanzishia safari mjini, huyu kimbunye akazuia ili bajaji zake zifanye biashara, sasa haoni maamuzi ya leo yanaongeza mateso kwa wananchi kwa maana ya wale abiria waliosaidiwa na mabasi makubwa wanakwenda kuongeza tatizo kwenye daladala ambazo ni za kugombania, anapata faida gani abiria wanapoteseka? Anapata faida gani mabasi makubwa yanapoondoka matupu huku abiria wakilazimika kwenda kupoteza muda kupigania daladala ambazo kimsingi ni chache?!
  2. Yupo kikaoni anatangaza uvaaji wa barakoa wakati yeye mwenyewe hana barakoa, anazungumzia mambo ambayo yeye mwenyewe ameshindwa kuyaonyeshea ushirikiano ili awe mfano. Bogus kabisa, hana ushirikiano kama meno yake yalivyo.
  3. Tulipendekeza watu wapimwe akili kabla ya kupewa nyadhiva, huyu RC ni shida hatufai wana Dar, si mshirikishaji kwenye decision making
Yaani toka kaletwa Dsm anachonga sana huyu kuitwa anaita media utafkiri tupo Kabul kutwa anataka asikike
 
Back
Top Bottom