DOKEZO LATRA fanyeni hivi kutatua Tatizo la bodaboda na bajaji na usafiri wa mijini kwa ujumla

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
A

Anonymous

Guest
Sijui shida ni nini. Huku south Africa, botwasana, Námibia huwezi oná bodaboda. Zimejaa zile toyota hiace Kila mahali.

Sisi tuliondoa hiace mjini miaka hiyo. Sasa tumesajili bodaboda na bajaji.

Solution ni simple. Waache kusajili bodaboda na bajaji. Waacha kuimport. Hiz zilizopo zifanye route za mitaani Ndani, yaan mfanoukishuka kimara korogwe BRT. Boda na bajaji ndo zichukue watu huko mitaani.

Bodaboda na bajaji zisitumie barabara kubwa yoyote kufanya biashara.
kuhusu Uber na bolt. Hao wasajiliwe. Wavae vizibao, wavae Kila kitu kinachopaswa kuwepo wakati wa kuendesha pikipiki. Ikiwemo helmet mbili na wafuate sheria kama wanavyofanya Rwanda.

LATRA ni wazembe sana. Kusajili Daladala. Hiv vicoster vinazidiwa na watu wanabanana. Wafikirie kusajili mabasi yanayoweza kubeba hata watu 50 mijini na yawe mapana ili watu wasibanane kama sasa. Tena yawe na AC na viti vya kutosha na ikiwezekane wamiliki waweke WIFI. Wapandishe nauli Hata kidogo lakini mtu atoe nauli kulingana na huduma

TUjipende watanzania. Hakuna mtu atakuja kututatulia matatizo yetu

SIDHANI KAMA KUNAHITAJIKA BAJETI YOYOTE KUFANYA HIVI
 
Mimi kilio changu wasajili daladala mbadala wa mwendo kasi, ziwe kwenye ruti ya mbezi kivukoni via morogoro road, mbezi kariakoo via morogoro road, hii njia ukiacha mwendo kasi ambayo imefeli ni adha tupu, ndio imejaza hivi vibajaji na pkpk, kuwe na rout hizo kuisaidia BRT ambayo imezidiwa. Watu wa mbezi , kimara kwenda mjii sasahivi ni mateso makubwa
 
Back
Top Bottom