Latest: Asha-Rose Migiro the new UN Deputy General Secretary

Mahiga na timu yake naona wako very busy
lakini hiyo haiondoi ukweli kuwa Mahiga alishamaliza muda wake na wengine waliobaki ni damu ya zamani sasa hivi tunahitaji damu mpaya na vile vile hatuhiaji ma security analyss kuwa ma diplomats wetu vile vile

Look at the bigger picture
 
JK itabidi amtafute mtu ambaye ataweza kuifanya kazi bila kumtazama usoni.

Mlalahoi

Endelea kulala maana ukiamka utakuwa hoi na mimi siwezi kubishana na mtu anaye lala mpaka anakuwa hoi kwani kutakuwa hamna tofauti.
 
Kitu kimoja kinachonichosha kuhusu JK ni jinsi ambavyo watu wanaweza kumtabiri kirahisi! Yaani ndugu yangu JK huwezi kuwa na siri?
 
Naam hakika ni uteuzi ambao hatuna budi kujivunia nao kwa sana tu wananchi wa tanzania.

Hivi punde leo hii nimezungumza na Katibu Mkuu Mteule huyu wa UN akiwa Afrika Kusini.

Attached is the interview.
 
Namna Said, ni interview murua kabisa. Uliuliza maswali safi kabisa na mama naye akajibu ipasavyo, ametulia kisawa sawa. Labda niongeza tu kuwa ni heshima pia kwa chuo kikuu cha Dar es Salaam. Ametuwakilisha ipasavyo. Sasa kama Nungwi atameza chupa hiyo shauri yake!
 
Mwanasiasa

Sasa wewe unaanza ubishi mwingine ambao hauna msingi hapa. Sasa sisi wengine tuliosoma vyuo vyenye majina kuanzia mwanzo tusemaje?

Haya mambo ya UDSM na Mzumbe hayana nafasi kwenye hii thread nenda anzisha thread nyingine kwa hilo.
 
Mwanasiasa

Sasa wewe unaanza ubishi mwingine ambao hauna msingi hapa. Sasa sisi wengine tuliosoma vyuo vyenye majina kuanzia mwanzo tusemaje?

Haya mambo ya UDSM na Mzumbe hayana nafasi kwenye hii thread nenda anzisha thread nyingine kwa hilo.


Nimekusikia mzee; nilikuwa namchokoza kidogo ndugu yangu Nungwi, maana yeye na Mzumbe, acha kabisa. Ahsante
 
Mwawado.
Mie nimesikia na Adam Malima yumo humo. sababu ana elimu nzuri na exposure kitu muhimu kwa wizara hiyo.

kuna jamaa kadokeza kuhusu Msabaha nae kuwemo kutokana na uzoefu wa masuala hayo na alikuwa katibu mkuu wa wizara hiyo.

na kuna dada mhagama nae anatajwa.
 
Sina nia ya kuwarudisha nyuma ila nami nampongeza Dk. A-R Migiro kuwa Naibu Katibu Mkuu wa UN.

Kuhusu kumpata mtu mwingine makini kwenye Wizara hiyo siwezi kutabiri. Ila Wizara hiyo tangu aondoke B. Mkapa enzi zile za Nyerere waliofuata wote walikuwa wababaishaji, ukiondoa Dr. A-R Migiro. Hata JK mwenyewe was a total failure, wakati wa JK tulianza kupoteza marafiki kwa uswahili wake mwingi, ilibidi Mzee Mkapa amrudishe Mh. Shariff kutoka London kuja kuokoa jahazi. Ndio maana sishangai JK akiendleza uswahili wake hata sasa yupo Rais. JK alipoana .Mh. Sharif anamzidi kwa upande wa Foreign isues alimchukia na hakumkumbuka mpaka leo hataki kumsikia. Anambeba "kiazi" mwenzake Luhanjo kwa kuwa alikuwa akimsadia ku-foji risiti za safari.
 
CCM KWELI NI KIBOKO,WAMEAMUA KUTEKA KUCHAGULIWA KWA HUYU MAMA KAMA VILE NI LA CHAMA BADALA YA KITAIFA.
LEO CCM WAMEANDAA MAPOKEZI YA MAMA MIGIRO PALE TERMINAL ONE SAA 8.15 ATAPOKEWA NA VIONGOZI NA WAPENZI WA CCM NA KUSINDIKIZWA HADI IKULU KUSALIMIANA NA JK THEN SAA KUMI ATAENDA MAKAO MAKUU YA CCM LUMUMBA KUHUTUBIA MKUTANO MDOGO WA WAPENZI NA WANACHAMA PALE
sasa hii sio vizuri sisis wengine ambao hatupendi sana kuwa side na vyama kwenye mabo ya kitaifa ,tulitegemea wizara ya mambo ya nje au mkuu wa mkoa aandae mapokezi,hili jambo ni la kitaifa si busara kuliteka nyara,ndio maana jana tulisema hapa jana namna walivyojisifu kumaliza mgawo wa umeme ,wakati ni Mungu tu katuonea huruma kaleta mvua si busara kupapasa mafanikio na kuyafanyia siasa.....
 
kwa kweli jafar true...jk alivyomfanyia dr sherriff sio fresh ,kamtosa kabisa mtu ambaye alikuwa anamsaidia kazi huku yeye akiuhangaikia urais...jamaa ni smart...na kasoma ...mwanzoni pale alimpa kazi ya kilemba cha ukoka eti mwenyekiti wa kamati ya kuitangaza tanzania nje ,hiyo kamati ni kilemba kwa sababu hadi leo haijazinduliwa na wala hatujui imefanya nini na wala hatujui ofisi zake so ilikuwa ni mbinu ya ke kumtoa sherrif kwenye reli tu,na utajuaje labda sherriff alikua kambi ya SAS
 
Jafar na Philemon Mikael hampo sahihi kabisa.

Abdul Kadir Sharif na Kikwete mwenye uzoefu zaidi kiserikali alikuwa ni JK alietumikia serikali tangu enzi za mwalimu, Sharifu aliondoka tanzania almost 30 yrs before na alipewa lifeline na Mzee Mwinyi, kwa kuteuliwa kuwa Balozi kwanza Saudi Arabia then UK, kabla ya hapo hajawahi kufanya kazi Tanzania let alone serikalini....there is no way unaweza kusema alikuwa na uzoefu kuliko JK...

Halafu ile ''DR'' nadhani inawashughulisha, hebu chekini vizuri alikuwa na Phd ya nini... then ndio mtajua uwezo wake...

Ati JK kamtupa Sharifu nadhani hamna data za kweli, yeye ndio mwenye kazi ya kuiuza Tanzania kimataifa, mradi wake unaitwa BRAND TANZANIA INITIATIVE, unakwenda sambamba na issue nzima ya economic diplomacy...kazi ipo chini ya Ofisi ya Rais, mnataka 'akumbukwe' vipi zaidi ya hapa?!


Vitu vingine ni beneath discussion yaani eti JK as waziri alikuwa anashirikiana na Luhanjo kufoji risiti za safari?!!.....come on guys you can do better than this....

Research should be the key aspect in instituting allegations.....
 
Inasikitisha kuona kuwa kwa watu wengine uteuzi wa Dr Migiro haukuwapendeza,lakini hili ni jambo la kawaida tu,lakini kama sababu zenyewe ni pamoja na yeye kutofungua ubalozi Brazil,kwa kweli hapo naona kidogo tunamuonea.Maana yeye kakaa mwaka mmoja tu,na mpango wa kufungua ubalozi uko mbioni,atakayefuata atamalizia hio kazi. Kitu kimoja ambacho ningependa kuuliza ni kuhusu process nzima ya kumteua naibu katibu mkuu....kwani si ni lazima jina lake lipitishwe na Baraza la Usalama?Please correct me if i'm wrong. Na wale ninvyojua mimi,wanachojali sio tu mtu mwenyewe ni nani tu,bali pia nchi yake inasimamia nini,serikali yake inaendesheshwaje,raisi wake ana msimamo gani au matazamo gani kwenye masuala ambayo ni muhimu kwao.Kwa mtazamo huo ni lazima watanzania tujisifu maana kama walivyosema wengi,ni sifa kwa nchi yetu,pia CCM lazima nao wajisifu,maana ni policy zinazotambulika hapa,na ndio zilijomfanya Dr Migiro afike huko alipofika.Ni mtazamo wangu tu...
 
...Lakini hii ya JK kufoji risiti na Luhanjo kiboko! Duh!!! Tuacheni utani jamani
 
...mwanzoni pale alimpa kazi ya kilemba cha ukoka eti mwenyekiti wa kamati ya kuitangaza tanzania nje ,hiyo kamati ni kilemba kwa sababu hadi leo haijazinduliwa na wala hatujui imefanya nini na wala hatujui ofisi zake[/QUOTE]

tafiti ,nimekusoma suala la sherriff kuwa mwenyekiti wa hilo kamati nililiongelea ,ila kama nilivyosema sijui kamati inafanya nini...kuhusu mh migiro namfagilia sana na nafrahia kama mafanikio ya taifa letu ,,wooote tunafurahi hakuna haja ya kuteka nyara mafanikio ya taifa ....mbona mpirani tunashangilia wote...mengine tafiti nakubaliana na wewe kaaka..saluuti!!!!
 
Back
Top Bottom