Rutashubanyuma
JF-Expert Member
- Sep 24, 2010
- 219,502
- 911,254
Pilau ale yeye tena kwa kificho huku akjijua ni mwizi tu.............akiwa kwenye chumba alichokishindilia komeo tena la viro ili asije kubambwa na mwenye mlo wale.............baada ya uporaji wa pilau ya watu aja mtaani na huanza kutubehulia.........na kuacha mafuta ya pilau na vipunjepunje vyake mdomoni.......
Hivi, hiyo shombo amletea nani?
Mwingine ametoka kumtafuna kuku wa watu khalafu kwa kasi ya ajabu hurukia kitandani kwa mkewe na kumshulizia manukato yatokanayo na siagi ya samli aliyopikiwa kuku wa watu aliyemtafuna ............kwa kufanya hivyo ni mithali ya kumtambia mkewe ya kuwa amejinoma kuku wa watu..........lakini swali ni
Hivi, hiyo shombo amletea nani?
Kwa nini asiende bafuni akaoga na kutakata na abakie akichekwa na dhamira yake badala ya kuwaadhibu waliokuwamo na wasio kuwamo..........kama ile hadithi ya panya aliyekusudiwa kuuawa na mtego lakini mtego ukamnasa nyoka ambaye mwenye nyumba aliposikia umenasa akawahi kummalizia panya gizani na matokeo yake akaumwa na nyoka mwenye hasira na kufa hapohapo.........matangani ng'ombe na kuku walichinjwa kumsindikiza mwendazake............na hivyo kukamilisha maono ya panya ya kuwa mtego ulomlenga yeye wataingia waliomo na wasiokuwamo........
Hivi walakini...........hiyo shombo amletea nani?

Lugha uliyotumia inahitaji utulivu sana ili mtu aweze kuchangia, any way nikipata breakfast nitaangalia uwezekano wa kuchangia:coffee:
Ngonjera nzuri sana hii, umefundishwa na nani? Mk'were mzee wa misemo?
Ruta
Aksante kwa mada hii hivi ni kweli mla nje hujisahau na kuja na shombo kweli??Haogopi kubambwa?
Eti mwingine kalishwa mijichips kuku huko na kidume cha jirani...anakuja kitandani na kuanza kuachia hewa zisizovutika sawia puani kwa mwenzie..hilo shombo amleteee nani??
Ana lambwa lambwa mdomo kama paka akiwa na kijike au kidume pori, anarudi nyumbani hataki hata kunawa mdomo anataka akugushishe mdomo wake..hilo shombo amletee nani??
Kaachia, kanyonywa nyonyo weeeee hata kuliko anavyoweza kuwamchia mwanae, eti baadae anarejea nyumbani anataka kumnyonyesha mtoto wake mchanga pasipo hata kujishwafi uzuri....eti hilo shombo anamletea nani??
Karuhusu kidume shume kimguse sehemu ambazo hata wewe mumewe/boy friend hujawahi kugusa, kanogewa huko, anarejea nyumbani, anakugezia nawe uguse huko asijue wewe sie yule aliyezoea mambo hayo..sasa hilo shombo la mtandao huo wenye wateja kidogo amleteee nani??
Bwana Ruta naona leo umetumia Tafisida kubwa sana hapa
Ngoja na mie nitafute namna ya kutumia Tafisida ili twende sambamba
ajivunia kufuli la viro..........lakini basi hata aoge lol.........