Laana ya mwanamke

Laana ya mwanamke

Katika masuala ya mahusiano mwanaume ndio muanzilishi....ni agharabu sana kwa mwanamke kumtongoza mwanaume ingawa hutokea....
Katika kushawishi huko unaweza ukamtoa mwanamke katika hali fulani hivi ya kutokukuamini na hatimaye akakuamini na hatimaye mkawa kwenye mahusiano.....
Wakati mwingine huyo mwanamke anaweza kuwa alikuwa kwenye mahusiano na mtu mwingine wenye mipango ya muda mrefu lakini kuringana na sera zako za kuvutia hatimaye ukambadilisha maamuzi na kuingia kwenye imaya yako.....kumbuka hata hapo kwenye kumtoa mwanamke kwenye imaya ya mtu mwingine tayari umeshaumiza nafsi ya mtu mwingine.....

Hadi kufikia hapo mwanamke huyu atakuwa na matumaini makubwa sana kwako....mapenzi yake na yote atayahamishia kwako akiamini kuwa wewe ndiye yule aliyeletewa na Bwana.....wakati mwingine huwa anakuulizia masuala ya kuona na wewe unamuambia kuwa dear mbona mapema sana....

Kwa kuwa lengo lako ni kumvua tu nguo na kumuacha unaanza harakati za kuomba ngono kwa kushawishi kwa aina mbali mbali na yeye lazima atakupa akiamini kuwa ni moja wapo ya njia ya kudumisha penzi lenu ili mfike mbali.....mtoto wa kike anajiachia kwako kwa raha zote hakuna sehemu ya mwili wake usiyoijua kwa jinsi alivyojiachia kwako akiamini kabisa kuwa wewe ndiye mumewe.....

Siku zinavyoende kwa kuwa umeshapata ulichokuwa unakitaka mapenzi yanapungua....unaanza kumuona kama kero fulani hivi....yaani kama anajipendekeza fulani hivi kwako.....hali hiyo inaendelea mpaka mwanamke anaanza kuwa na wasi wasi kuhusu hali ya uhusiano wenu....unaamzungusha na hatimaye unaamua kumuambia live kuwa huna mpango nae....

Hebu jiweke katika nafasi ya mwanamke je ungejisikiaje...

Hakika ni jambo lenye kukera na kusononeka maaana katika muda huo labda alipuuzia mahitaji ya watu wenye upendo wa kweli huku akiishi katika uongo wako....
Ni jambo ambalo kwa mwanadamu mwenye akili ya kawiada hangependa limtokee kwani ni jambo kuumiza moyo kama sio kuuchoma moyo....

Yale manung'uniko, masononeko na machozi yasiyokauka muda wote kila akifikiria jinsi ulivyozikatisha ndoto zake nyingi tu kwa ajili ya uongo wako ndivyo vinavyokuletea mikosi kwenye maisha yako.....

Ndio maana hata nyakati hizi utafutaji ridhiki umekuwa ni mgumu sana kwa vijana wa kiume kwa sababu ya madhambi makubwa sana waliyowatendea mabinti wa watu.....maana kuna mabinti wengine walijitunza sana lakini wakashawishika kwa ulaghai wao.....
Na mambo ambayo ni ngumu kuyathibitisha kama ambavyo ilivyo kwa nguvu za giza lakini yapo na watu wanateseka kwa ajili ya hayo....
Hujawahi kuona anakuwa kama kachanganyikiwa baaada ya kuachika na mtu ampendaye....wengine huenda mbali mpaka kunywa sumu na kuutoa uhai wako mtukufu kwa ajili ya ulaghai wako tu......sasa hapo kuna baraka gani kwenye maisha yako ikiwa wewe ndiyo chanzo cha mahangaiko na vifo vya mabinti wengi sana mtaani......??
Mkuu uzi wako una cha kujifunza...swali nje ya uzi...kahtaan ni id yako nyingine au!
 
Habari za wakati huu ndugu na marafiki wapendwa wa JamiiForums....

Ni siku nyingine tena tulivu ikiambatana na manyunyu ya hapa na hapa pale kwa sisi wakazi wa Dar......

Leo ningependa kuwashirikisha katika jambo muhimu sana ndugu zangu ambalo hata mimi binafsi ninaweza kuwa shahidi kabisa....

Kuna kipindi nyakati za nyuma kidogo nilitokea kumtamani binti fulani hivi ambaye tulikuwa tukiishi nae karibu na nilipokuwa nikiishi mimi kusema ukweli huyu mimi sikumpenda isipokuwa nilikuwa namuhitaji kwa ajili ya kukidhi matakwa yangu ya kimwili, kutokana na ushawishi mkubwa nilifanikiwa kumnasa yule binti na tukaanza kushiriki ngono huku yeye akijua kuwa mimi ndiye mumewe mtarajiwa yule binti alikuwa ni binti mwenye kujitegemea maana alikuwa anafanya kazi kwenye kampuni fulani kubwa hivi ya kigeni kwa hiyo suala kipato alikuwa tatizo kwake alichokuwa anakihataji ni mapenzi au mume ambaye aliamini kuwa ameshampata.....

Baada ya kukidhi haja zangu nikaanza kumkwepa kwa maana nilimuona kama ni kero vile kwangu, yule dada nilimpa wakati mgumu sana kwa mabadiliko yale na alikuwa akilia mbele yangu mara kwa mara akinisihi nisimuache lakini mimi sikuelewa lolote lile,yule mwanamke akakata tamaa na akaamua kuachana na mimi lakini alinitamkia maneno mazito sana kuhusu maisha yangu ambayo nilianza kuyaelewa maana yake baada ya mwezi kupita tangu kukata mawasiliano naye......

Niliona ghafla mambo yangu yanabadilika na kuwa mabaya kabisa biashara zangu nyingi sana zilikwama mpaka nikawa nakosa hata hela ya kula ile hali ikanishtua sana maana haikuwa kawaida ikabidi kuahangaika katika mambo ya kiswahili ndipo wataalamu waliponifunulia kuwa kuna mtu ana kinyongo na wewe kwa hiyo unatakiwa ukamiombe msamaha maana ndio njia pekee ya wewe kuondokana na mikosi hiyo maana hakuna aliyeniroga.....

Ikanibidi kwa unyonge kabisa nijipendekeze kwa yule binti na kuanza kujenga naye ukaribu upya na kuomba misamaha mingi sana....

Baada ya muda nikaona mambo yanaanza kubadilika na kuwa kama kawaida.....

N:B Dhumuni la mimi kushare kisa hiki ni kuwaasa vijana kuwa kama mwanamke huna mipango naye ya muda mrefu basi usimpotezee muda wake bure maana utamuacha na sononeko ambalo litakuletea mikosi kwenye maisha yako wapo vijana wasomi wanaohangaika kutafuta kazi takribani miaka kumi wapo vijana wanaojaribu kuanzisha biashara zao lakini huwa zinakufa wapo vijana wanaofukuzwa kazi katika mazingira ambayo hata yeye hawayaelewi hizi ni moja ya athari za watu waliokuwa na vinyongo na wewe.....

Shtuka kijana
Mambo yako yalikuwa ni lazima yaende hovyo baada ya kuachana nae kwa kuwa demu alikuwa ana pesa na wewe ulukuwa unaitegemea pesa yake ila humpendi sasa wewe mario lazima ulivyomuacha uchumi wako utayumba tu teh teh kiding bro ila unaambiwa chozi la mwanamke likidondoka akikulilia ujuwe kuna madhara makubwa sana hapo baadae ila sio kila mwanamke achana na hawa wanawake korofi, ila ni vyema umejifunza mkuu...
 
Sawa sawa mkuu....yule mwanamke mpaka leo hii yupo na tunaonana kila siku kwa kuwa bado tunaishi jilani ingawa si karibu kama mwanzo.... sasa hivi ameshaolewa na mimi naiheshimu sana ndoa yake.....na tupo kama marafiki....ingawa kiuchumi mambo ni mazuri sana lakini sijawahi kumlilia shida hata siku moja ingawa hali yangu ni mbaya sana...nashukuru kupitia kikazi changu naweza kukidhi mahitaji yangu....
 
Ohhhhh kumbe alishaolewa mkuu, aisehhh nikupe pole sana,nahisi inakuathiri mpaka leo mkuu,huyo manzi alikuwa perfect for marriage mkuu,
 
Sikuwahi kumpenda hata robo....ndio maana nilifurahia harusi yake...
Ohhhhh kumbe alishaolewa mkuu, aisehhh nikupe pole sana,nahisi inakuathiri mpaka leo mkuu,huyo manzi alikuwa perfect for marriage mkuu,
 
Hakuna kitu kinauma kama kupotezewa Muda, Ex wangu hadi leo pamoja na kuwa na kazi nzuri maisha yake hayaeleweki, kwenye mahusiano ndo usiseme, nabado napiga goti kwa Mungu siku atakayorudi kuomba msamaha kwakunikosea ndo amwachilie.
Hakuna kitu kama hicho... Laan ipo kwa baba na mama tu na sio nying'au yeyote.. Ww ukifikir ex wako kayumba kwasababu ya kukuacha ww unajidanganya bure.. Ngoja maisha yageuke upande wa pili ndio utaona.
 
Ni kweli usemayo,hakuna kitu kinauma kama kupotezewa muda jamani, umejitunza na kuwakataa wengine wenye nia afu mtu anakuacha hewani gafla,uwiii.... Mungu niepushie isinitokee tena
Hahahaha inakusubir tena mbaya zaid utakuta umemtambulisha hadi kwenu
 
Habari za wakati huu ndugu na marafiki wapendwa wa JamiiForums....

Ni siku nyingine tena tulivu ikiambatana na manyunyu ya hapa na hapa pale kwa sisi wakazi wa Dar......

Leo ningependa kuwashirikisha katika jambo muhimu sana ndugu zangu ambalo hata mimi binafsi ninaweza kuwa shahidi kabisa....

Kuna kipindi nyakati za nyuma kidogo nilitokea kumtamani binti fulani hivi ambaye tulikuwa tukiishi nae karibu na nilipokuwa nikiishi mimi kusema ukweli huyu mimi sikumpenda isipokuwa nilikuwa namuhitaji kwa ajili ya kukidhi matakwa yangu ya kimwili, kutokana na ushawishi mkubwa nilifanikiwa kumnasa yule binti na tukaanza kushiriki ngono huku yeye akijua kuwa mimi ndiye mumewe mtarajiwa yule binti alikuwa ni binti mwenye kujitegemea maana alikuwa anafanya kazi kwenye kampuni fulani kubwa hivi ya kigeni kwa hiyo suala kipato alikuwa tatizo kwake alichokuwa anakihataji ni mapenzi au mume ambaye aliamini kuwa ameshampata.....

Baada ya kukidhi haja zangu nikaanza kumkwepa kwa maana nilimuona kama ni kero vile kwangu, yule dada nilimpa wakati mgumu sana kwa mabadiliko yale na alikuwa akilia mbele yangu mara kwa mara akinisihi nisimuache lakini mimi sikuelewa lolote lile,yule mwanamke akakata tamaa na akaamua kuachana na mimi lakini alinitamkia maneno mazito sana kuhusu maisha yangu ambayo nilianza kuyaelewa maana yake baada ya mwezi kupita tangu kukata mawasiliano naye......

Niliona ghafla mambo yangu yanabadilika na kuwa mabaya kabisa biashara zangu nyingi sana zilikwama mpaka nikawa nakosa hata hela ya kula ile hali ikanishtua sana maana haikuwa kawaida ikabidi kuahangaika katika mambo ya kiswahili ndipo wataalamu waliponifunulia kuwa kuna mtu ana kinyongo na wewe kwa hiyo unatakiwa ukamiombe msamaha maana ndio njia pekee ya wewe kuondokana na mikosi hiyo maana hakuna aliyeniroga.....

Ikanibidi kwa unyonge kabisa nijipendekeze kwa yule binti na kuanza kujenga naye ukaribu upya na kuomba misamaha mingi sana....

Baada ya muda nikaona mambo yanaanza kubadilika na kuwa kama kawaida.....

N:B Dhumuni la mimi kushare kisa hiki ni kuwaasa vijana kuwa kama mwanamke huna mipango naye ya muda mrefu basi usimpotezee muda wake bure maana utamuacha na sononeko ambalo litakuletea mikosi kwenye maisha yako wapo vijana wasomi wanaohangaika kutafuta kazi takribani miaka kumi wapo vijana wanaojaribu kuanzisha biashara zao lakini huwa zinakufa wapo vijana wanaofukuzwa kazi katika mazingira ambayo hata yeye hawayaelewi hizi ni moja ya athari za watu waliokuwa na vinyongo na wewe.....

Shtuka kijana
mhh kama Kuna ka ukweli ndani yake aisee...
 
Laaana... Sidhani ...
Kuyumba kimaisha hizo ni feedback..cha kufanya ni kutafuta sources ila sio hio ya uzinzi
 
Kama ni hivyo ningeshapata laana nyingi sana... lakini nipo poa na mambo yangu yananyoka tuu...
 
Ni kweli usemayo,hakuna kitu kinauma kama kupotezewa muda jamani, umejitunza na kuwakataa wengine wenye nia afu mtu anakuacha hewani gafla,uwiii.... Mungu niepushie isinitokee tena
...labda kuna definition nyingine ya kujitunza. Hamjitunzi miaka hii bwana!!
 
Hivi nisiposamehe nikienda kanisani kusali napiga goti naanzaje kumuomba Mungu.??kwanza nasikia aibuu ht kuomba..na ikitokea naenda kanisan nitakuwa tu km picha ...nashindwa kabisa kumuomba Mungu ipasavyo cz kuna kitu moyon kinanisuta....GUYS FORGIVE AND FORGET KUNA RAHA KUBWA SANA YA KUMSAMEHE ALOKUKOSEA
kwanza huko aliko vitamsuta
Pili unajiongezea baraka
Visasi na maugomvi sio mazuriiiii....dunia itakua chungu kila siku ukiendekeza mavisasi na kubeba watu moyoni
Word! wasemavyo vijana wengine.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom