Laana ya mwanamke

Laana ya mwanamke

Mleta mada, mimi siamini kuwa machozi yake(yao) yatanipa laana, kwa sababu;
1. Mbele za M/Mungu tulifanya dhambi ya uzinzi, ngono na uchafu ambao Mungu hapendi.
2. Tulitenda dhambi ya uongo wote (mimi nilimdanganya, nae kadanganya kwa Mungu)
Hayo yaliyokupata ni sehemu ya maisha tu (ups and downs) na wala haihusiani na kumdanganya au kuchezea mwili na hisia zake. Mwanamke wa kweli hachezewi mwili coz anaitambua thamani ya mwili wake, the worst you can do ni kuchezea hisia. Mwanamke/mwanaume anayechezewa mwili ni mjinga mjinga tu..
Umemaliza kiongozi,I think wakuhukumu hapa ni Mungu na sio mtu tena kwa sababu wote mnakuwa mmetenda dhambi ila kuna mtu hapa yupo likely kuhukumiwa kwa dhambi nyingi zaidi
 
Hakuna kitu kinauma kama kupotezewa Muda, Ex wangu hadi leo pamoja na kuwa na kazi nzuri maisha yake hayaeleweki, kwenye mahusiano ndo usiseme, nabado napiga goti kwa Mungu siku atakayorudi kuomba msamaha kwakunikosea ndo amwachilie.
Nahisi kwamba nawe umejifunga. Huna raha mpaka umwone ameumia! Mwachilie, msamehe, msamehe kabisa. Utaona raha kubwa. Usijali kama ataenda mbele au atarudi nyuma. Wewe mwombee kwa Mungu kwa kumsamehe kabisa. Utajifungulia milango mingi zaidi.
 
I can feel you on this.. It hurts so much... But let him go so God can use you more ..Thanks..
Exactly..hakuna haja ya kumbeba mtu moyoni...samehe huko aliko ili nawe uwe na aman moyonI na upate nafasi ya kuweka mwingine...nisipomsamehe itanisaidia nn...mangapi namkosea Mungu na ananisamehe..mimi ni nanI ht nijibebeshe mizigo ...akhaaaaaa
Yn I thank God for that nitaumia mwanzoni but na let it go..nakuwa na amaani...hukupangiwa kuwa wangu ..go....full stop
Only God knows why amemuondosha
 
Hivi nisiposamehe nikienda kanisani kusali napiga goti naanzaje kumuomba Mungu.??kwanza nasikia aibuu ht kuomba..na ikitokea naenda kanisan nitakuwa tu km picha ...nashindwa kabisa kumuomba Mungu ipasavyo cz kuna kitu moyon kinanisuta....GUYS FORGIVE AND FORGET KUNA RAHA KUBWA SANA YA KUMSAMEHE ALOKUKOSEA
kwanza huko aliko vitamsuta
Pili unajiongezea baraka
Visasi na maugomvi sio mazuriiiii....dunia itakua chungu kila siku ukiendekeza mavisasi na kubeba watu moyoni
 
uploadfromtaptalk1460156871966.jpeg
 
Mambo kama hayo hayapo,huo ni uongo na uzushi, ni mambo tu ya kiswahili kupenda ushirikina na uchawi ambao kiuhalisia haupo.

Yani mtu awe na kinyongo na wewe mganga ndio ajue kua kuna mtu ana kinyongo na wewe? Sema unataka tu kusema hua unaenda kwa waganga wa kienyeji ila mambo kama hayo hayapo.
 
Habari za wakati huu ndugu na marafiki wapendwa wa JamiiForums....

Ni siku nyingine tena tulivu ikiambatana na manyunyu ya hapa na hapa pale kwa sisi wakazi wa Dar......

Leo ningependa kuwashirikisha katika jambo muhimu sana ndugu zangu ambalo hata mimi binafsi ninaweza kuwa shahidi kabisa....

Kuna kipindi nyakati za nyuma kidogo nilitokea kumtamani binti fulani hivi ambaye tulikuwa tukiishi nae karibu na nilipokuwa nikiishi mimi kusema ukweli huyu mimi sikumpenda isipokuwa nilikuwa namuhitaji kwa ajili ya kukidhi matakwa yangu ya kimwili, kutokana na ushawishi mkubwa nilifanikiwa kumnasa yule binti na tukaanza kushiriki ngono huku yeye akijua kuwa mimi ndiye mumewe mtarajiwa yule binti alikuwa ni binti mwenye kujitegemea maana alikuwa anafanya kazi kwenye kampuni fulani kubwa hivi ya kigeni kwa hiyo suala kipato alikuwa tatizo kwake alichokuwa anakihataji ni mapenzi au mume ambaye aliamini kuwa ameshampata.....

Baada ya kukidhi haja zangu nikaanza kumkwepa kwa maana nilimuona kama ni kero vile kwangu, yule dada nilimpa wakati mgumu sana kwa mabadiliko yale na alikuwa akilia mbele yangu mara kwa mara akinisihi nisimuache lakini mimi sikuelewa lolote lile,yule mwanamke akakata tamaa na akaamua kuachana na mimi lakini alinitamkia maneno mazito sana kuhusu maisha yangu ambayo nilianza kuyaelewa maana yake baada ya mwezi kupita tangu kukata mawasiliano naye......

Niliona ghafla mambo yangu yanabadilika na kuwa mabaya kabisa biashara zangu nyingi sana zilikwama mpaka nikawa nakosa hata hela ya kula ile hali ikanishtua sana maana haikuwa kawaida ikabidi kuahangaika katika mambo ya kiswahili ndipo wataalamu waliponifunulia kuwa kuna mtu ana kinyongo na wewe kwa hiyo unatakiwa ukamiombe msamaha maana ndio njia pekee ya wewe kuondokana na mikosi hiyo maana hakuna aliyeniroga.....

Ikanibidi kwa unyonge kabisa nijipendekeze kwa yule binti na kuanza kujenga naye ukaribu upya na kuomba misamaha mingi sana....

Baada ya muda nikaona mambo yanaanza kubadilika na kuwa kama kawaida.....

N:B Dhumuni la mimi kushare kisa hiki ni kuwaasa vijana kuwa kama mwanamke huna mipango naye ya muda mrefu basi usimpotezee muda wake bure maana utamuacha na sononeko ambalo litakuletea mikosi kwenye maisha yako wapo vijana wasomi wanaohangaika kutafuta kazi takribani miaka kumi wapo vijana wanaojaribu kuanzisha biashara zao lakini huwa zinakufa wapo vijana wanaofukuzwa kazi katika mazingira ambayo hata yeye hawayaelewi hizi ni moja ya athari za watu waliokuwa na vinyongo na wewe.....

Shtuka kijana
Nisamehewe tuu nanaomba huyu mwanaume apate pigo la maisha hadi ajue kweli macjoz yangu na mwanangu tumboni mungu anatusikia!!!
 
Bwana mdogo kuna hilo. Lakini lingine ni kiwa tunapotafuta wenza wetu huwa tunaweka.masikhara pembeni. Mwanamke wa kumwoa ni yule analeta rizki kwa maana ya upepo na utakula mbingu hapa hapa duniani. Mwanamke huyu kama.ulivosema akikuombea kwa.mungu basi mbingu inafunguka..akitoa machozi mbingu zinafunga....mheshimu sana huyo mwanamke kwani ndoa hufungwa peponi..

Kwani huyo mwanamke anatoka mbiguni
 
Wanawake wengi warembo ni watoto wa shetani...nuksi tupu...au hawana kibali chochote mbele ya mungu kukubariki....mara nyingi ukiingia hapo basi hata kile kidogo ulichonacho kinapotea...
Kwa kauli yako hii Basi Nyani Ngabu atakuwa mtoto wa malaika manake ana sura mbovu ka nyani kaonja ukwaju.
 
Mleta mada, mimi siamini kuwa machozi yake(yao) yatanipa laana, kwa sababu;
1. Mbele za M/Mungu tulifanya dhambi ya uzinzi, ngono na uchafu ambao Mungu hapendi.
2. Tulitenda dhambi ya uongo wote (mimi nilimdanganya, nae kadanganya kwa Mungu)
Hayo yaliyokupata ni sehemu ya maisha tu (ups and downs) na wala haihusiani na kumdanganya au kuchezea mwili na hisia zake. Mwanamke wa kweli hachezewi mwili coz anaitambua thamani ya mwili wake, the worst you can do ni kuchezea hisia. Mwanamke/mwanaume anayechezewa mwili ni mjinga mjinga tu..
Katika masuala ya mahusiano mwanaume ndio muanzilishi....ni agharabu sana kwa mwanamke kumtongoza mwanaume ingawa hutokea....
Katika kushawishi huko unaweza ukamtoa mwanamke katika hali fulani hivi ya kutokukuamini na hatimaye akakuamini na hatimaye mkawa kwenye mahusiano.....
Wakati mwingine huyo mwanamke anaweza kuwa alikuwa kwenye mahusiano na mtu mwingine wenye mipango ya muda mrefu lakini kuringana na sera zako za kuvutia hatimaye ukambadilisha maamuzi na kuingia kwenye imaya yako.....kumbuka hata hapo kwenye kumtoa mwanamke kwenye imaya ya mtu mwingine tayari umeshaumiza nafsi ya mtu mwingine.....

Hadi kufikia hapo mwanamke huyu atakuwa na matumaini makubwa sana kwako....mapenzi yake na yote atayahamishia kwako akiamini kuwa wewe ndiye yule aliyeletewa na Bwana.....wakati mwingine huwa anakuulizia masuala ya kuona na wewe unamuambia kuwa dear mbona mapema sana....

Kwa kuwa lengo lako ni kumvua tu nguo na kumuacha unaanza harakati za kuomba ngono kwa kushawishi kwa aina mbali mbali na yeye lazima atakupa akiamini kuwa ni moja wapo ya njia ya kudumisha penzi lenu ili mfike mbali.....mtoto wa kike anajiachia kwako kwa raha zote hakuna sehemu ya mwili wake usiyoijua kwa jinsi alivyojiachia kwako akiamini kabisa kuwa wewe ndiye mumewe.....

Siku zinavyoende kwa kuwa umeshapata ulichokuwa unakitaka mapenzi yanapungua....unaanza kumuona kama kero fulani hivi....yaani kama anajipendekeza fulani hivi kwako.....hali hiyo inaendelea mpaka mwanamke anaanza kuwa na wasi wasi kuhusu hali ya uhusiano wenu....unaamzungusha na hatimaye unaamua kumuambia live kuwa huna mpango nae....

Hebu jiweke katika nafasi ya mwanamke je ungejisikiaje...

Hakika ni jambo lenye kukera na kusononeka maaana katika muda huo labda alipuuzia mahitaji ya watu wenye upendo wa kweli huku akiishi katika uongo wako....
Ni jambo ambalo kwa mwanadamu mwenye akili ya kawiada hangependa limtokee kwani ni jambo kuumiza moyo kama sio kuuchoma moyo....

Yale manung'uniko, masononeko na machozi yasiyokauka muda wote kila akifikiria jinsi ulivyozikatisha ndoto zake nyingi tu kwa ajili ya uongo wako ndivyo vinavyokuletea mikosi kwenye maisha yako.....

Ndio maana hata nyakati hizi utafutaji ridhiki umekuwa ni mgumu sana kwa vijana wa kiume kwa sababu ya madhambi makubwa sana waliyowatendea mabinti wa watu.....maana kuna mabinti wengine walijitunza sana lakini wakashawishika kwa ulaghai wao.....
Na mambo ambayo ni ngumu kuyathibitisha kama ambavyo ilivyo kwa nguvu za giza lakini yapo na watu wanateseka kwa ajili ya hayo....
Hujawahi kuona anakuwa kama kachanganyikiwa baaada ya kuachika na mtu ampendaye....wengine huenda mbali mpaka kunywa sumu na kuutoa uhai wako mtukufu kwa ajili ya ulaghai wako tu......sasa hapo kuna baraka gani kwenye maisha yako ikiwa wewe ndiyo chanzo cha mahangaiko na vifo vya mabinti wengi sana mtaani......??
 
Nisamehewe tuu nanaomba huyu mwanaume apate pigo la maisha hadi ajue kweli macjoz yangu na mwanangu tumboni mungu anatusikia!!!
Pole sana dada yangu....Mungu humzidishia baraka yule mwenye kusamehe.....kuendelea kuhifadhi hasira kifuani mmwako ni sawa na kushikilia kaa la moto....maana yake kabla ya kumrushia mtu limuunguze kwanza linaanza kukuunguza wewe......samehe uone jinsi gani kama umezaliwa upyaa.....
 
Mambo kama hayo hayapo,huo ni uongo na uzushi, ni mambo tu ya kiswahili kupenda ushirikina na uchawi ambao kiuhalisia haupo.

Yani mtu awe na kinyongo na wewe mganga ndio ajue kua kuna mtu ana kinyongo na wewe? Sema unataka tu kusema hua unaenda kwa waganga wa kienyeji ila mambo kama hayo hayapo.
Huwezi kujua kuwa dunia ina mambo mpaka likukute jambo....
 
Pole sana dada yangu....Mungu humzidishia baraka yule mwenye kusamehe.....kuendelea kuhifadhi hasira kifuani mmwako ni sawa na kushikilia kaa la moto....maana yake kabla ya kumrushia mtu limuunguze kwanza linaanza kukuunguza wewe......samehe uone jinsi gani kama umezaliwa upyaa.....
Machungu ninayopitia anajua mungu pekee, na mwanangu àliepo tumboni, ndio màana naomba lolote baya juu yake nae aumie, japo haitofikia maumivu yangu hata theluthi
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom