Laana ya mwanamke

KikulachoChako

JF-Expert Member
Jul 21, 2013
18,896
36,213
Habari za wakati huu ndugu na marafiki wapendwa wa JamiiForums....

Ni siku nyingine tena tulivu ikiambatana na manyunyu ya hapa na hapa pale kwa sisi wakazi wa Dar......

Leo ningependa kuwashirikisha katika jambo muhimu sana ndugu zangu ambalo hata mimi binafsi ninaweza kuwa shahidi kabisa....

Kuna kipindi nyakati za nyuma kidogo nilitokea kumtamani binti fulani hivi ambaye tulikuwa tukiishi nae karibu na nilipokuwa nikiishi mimi kusema ukweli huyu mimi sikumpenda isipokuwa nilikuwa namuhitaji kwa ajili ya kukidhi matakwa yangu ya kimwili, kutokana na ushawishi mkubwa nilifanikiwa kumnasa yule binti na tukaanza kushiriki ngono huku yeye akijua kuwa mimi ndiye mumewe mtarajiwa yule binti alikuwa ni binti mwenye kujitegemea maana alikuwa anafanya kazi kwenye kampuni fulani kubwa hivi ya kigeni kwa hiyo suala kipato alikuwa tatizo kwake alichokuwa anakihataji ni mapenzi au mume ambaye aliamini kuwa ameshampata.....

Baada ya kukidhi haja zangu nikaanza kumkwepa kwa maana nilimuona kama ni kero vile kwangu, yule dada nilimpa wakati mgumu sana kwa mabadiliko yale na alikuwa akilia mbele yangu mara kwa mara akinisihi nisimuache lakini mimi sikuelewa lolote lile,yule mwanamke akakata tamaa na akaamua kuachana na mimi lakini alinitamkia maneno mazito sana kuhusu maisha yangu ambayo nilianza kuyaelewa maana yake baada ya mwezi kupita tangu kukata mawasiliano naye......

Niliona ghafla mambo yangu yanabadilika na kuwa mabaya kabisa biashara zangu nyingi sana zilikwama mpaka nikawa nakosa hata hela ya kula ile hali ikanishtua sana maana haikuwa kawaida ikabidi kuahangaika katika mambo ya kiswahili ndipo wataalamu waliponifunulia kuwa kuna mtu ana kinyongo na wewe kwa hiyo unatakiwa ukamiombe msamaha maana ndio njia pekee ya wewe kuondokana na mikosi hiyo maana hakuna aliyeniroga.....

Ikanibidi kwa unyonge kabisa nijipendekeze kwa yule binti na kuanza kujenga naye ukaribu upya na kuomba misamaha mingi sana....

Baada ya muda nikaona mambo yanaanza kubadilika na kuwa kama kawaida.....

N:B Dhumuni la mimi kushare kisa hiki ni kuwaasa vijana kuwa kama mwanamke huna mipango naye ya muda mrefu basi usimpotezee muda wake bure maana utamuacha na sononeko ambalo litakuletea mikosi kwenye maisha yako wapo vijana wasomi wanaohangaika kutafuta kazi takribani miaka kumi wapo vijana wanaojaribu kuanzisha biashara zao lakini huwa zinakufa wapo vijana wanaofukuzwa kazi katika mazingira ambayo hata yeye hawayaelewi hizi ni moja ya athari za watu waliokuwa na vinyongo na wewe.....

Shtuka kijana
 
Bwana mdogo kuna hilo. Lakini lingine ni kiwa tunapotafuta wenza wetu huwa tunaweka.masikhara pembeni. Mwanamke wa kumwoa ni yule analeta rizki kwa maana ya upepo na utakula mbingu hapa hapa duniani. Mwanamke huyu kama.ulivosema akikuombea kwa.mungu basi mbingu inafunguka..akitoa machozi mbingu zinafunga....mheshimu sana huyo mwanamke kwani ndoa hufungwa peponi...

Ndio maana wengine hukosea mke wa kwanza wanaangalia kuoa matako au miss bantu halafu nuksi zinaanza. Akistuka anasaihisha kwa mke wa pili ndipo anaanza kuonja pepo....

Wanaweke wengine ni nuksi tu...ukimnunulia tu hata soda lazima ukitoka hapo gari igonge
 
Wanawake wengi warembo ni watoto wa shetani...nuksi tupu...au hawana kibali chochote mbele ya mungu kukubariki....mara nyingi ukiingia hapo basi hata kile kidogo ulichonacho kinapotea...
 
Hii kitu ni kweli lakini kwa wasio mjua Mungu, wale wanaoamini kwenye uganga na mambo ya nyota. Vijana mlio single...usitishwe kutooa au kutoingia kwenye mahusiano na mwanamke usimpenda. Watasema umefatamakalio yake au sura au hela zake...maadamu mmependana, na hata mkaingia kwenye ndoa...na alaaniwe aliye kinyume chenu, maana walipo wawili...Mungu yupo hapo.

Kuhusu mwenza kumtamkia mwenzake maneno mabaya...ukiyaamini itakuwa hivyo, ni sawa na utakapoamini neno la Mungu...utapata linachosema na ahadi zake utazipokea. Kwahiyo binafsi sioanishi majanga unayoweza kukumbana nayo na uwezo wa mwanadamu awaye yote. Laana na Baraka zipo mikononi mwa Mungu tu.
 
Halafu wanaume wengi huwa hawajui tu hili wao ni kuumiza feelings za wanawake kumchezea na kumu dap baada ya kupata walichokitaka ndo mana wengi ndoa zao zimewashinda, no success watajiuliza tatizo liko wapi bora ukikutana na mwanamke mwambie ukweli kuwa tuna toana ngenye basi sasa mijianaume mingine inakua inaji proud kabisa machozi ya MTU ni laana mojawapo
 
Habari za wakati huu ndugu na marafiki wapendwa wa Jamii Forums....
Ni siku nyingine tena tulivu ikiambatana na manyunyu ya hapa na hapa pale kwa sisi wakazi wa Dar......

Leo ningependa kuwashirikisha katika jambo muhimu sana ndugu zangu ambalo hata mimi binafsi ninaweza kuwa shahidi kabisa....

Kuna kipindi nyakati za nyuma kidogo nilitokea kumtamani binti fulani hivi ambaye tulikuwa tukiishi nae karibu na nilipokuwa nikiishi mimi...kusema ukweli huyu mimi sikumpenda isipokuww nilikuwa namuhitaji kwa ajili ya kukidhi matakwa yangu ya kimwili.....kutokana na ushawishi mkubwa nilifanikiwa kumnasa yule binti na tukaanza kushiriki ngono huku yeye akijua kuwa mimi ndiye mumewe mtarajiwa.....yule binti alikuwa ni binti mwenye kujitegemea maana alikuwa anafanya kazi kwenye kampuni fulani kubwa hivi ya kigeni kwa hiyo suala kipato alikuwa tatizo kwake....alichokuwa anakihataji ni mapenzi au mume ambaye aliamini kuwa ameshampata.....
Baada ya kukidhi haja zangu nikaanza kumkwepa kwa maana nilimuona kama ni kero vile kwangu.....yule dada nilimpa wakati mgumu sana kwa mabadiliko yale....na alikuwa akilia mbele yangu mara kwa mara akinisihi nisimuache lakini mimi sikuelewa lolote lile....yule mwanamke akakata tamaa na akaamua kuachana na mimi lakini alinitamkia maneno mazito sana kuhusu maisha yangu....ambayo nilianza kuyaelewa maana yake baada ya mwezi kupita tangu kukata mawasiliano naye.......
Niliona ghafla mambo yangu yanabadilika na kuwa mabaya kabisa....biashara zangu nyingi sana zilikwama mpaka nikawa nakosa hata hela ya kula......ile hali ikanishtua sana maana haikuwa kawaida ikabidi kuahangaika katika mambo ya kiswahili ndipo wataalamu waliponifunulia kuwa kuna mtu ana kinyongo na wewe kwa hiyo unatakiwa ukamiombe msamaha maana ndio njia pekee ya wewe kuondokana na mikosi hiyo maana hakuna aliyeniroga.....

Ikanibidi kwa unyonge kabisa nijipendekeze kwa yule binti na kuanza kujenga naye ukaribu upya na kuomba misamaha mingi sana....

Baada ya muda nikaona mambo yanaanza kubadilika na kuwa kama kawaida.....

N:B Dhumuni la mimi kushare kisa hiki ni kuwaasa vijana kuwa kama mwanamke huna mipango naye ya muda mrefu basi usimpotezee muda wake bure maana utamuacha na sononeko ambalo litakuletea mikosi kwenye maisha yako.....wapo vijana wasomi wanaohangaika kutafuta kazi takribani miaka kumi....wapo vijana wanaojaribu kuanzisha biashara zao lakini huwa zinakufa.....wapo vijana wanaofukuzwa kazi katika mazingira ambayo hata yeye hawayaelewi...hizi ni moja ya athari za watu waliokuwa na vinyongo na wewe.....

Stuka kijana
Laana wanawake tu?,mbona sie wanaume tukitoa laana haifiki,tutaachwa sana
 
Hakuna kitu kinauma kama kupotezewa Muda, Ex wangu hadi leo pamoja na kuwa na kazi nzuri maisha yake hayaeleweki, kwenye mahusiano ndo usiseme, nabado napiga goti kwa Mungu siku atakayorudi kuomba msamaha kwakunikosea ndo amwachilie.
 
Hakuna kitu kinauma kama kupotezewa Muda, Ex wangu hadi leo pamoja na kuwa na kazi nzuri maisha yake hayaeleweki, kwenye mahusiano ndo usiseme, nabado napiga goti kwa Mungu siku atakayorudi kuomba msamaha kwakunikosea ndo amwachilie.
kwani bado hujamsamehe
 
Back
Top Bottom