Laana ya Mapenzi .....

Laana ya Mapenzi .....

Habari za usiku wadau,
Poleni na mishughuliko ya kutwa nzima na hongereni kwa kujibidiisha na kujituma shurti ule vizuri, uvae vizuri, ulale vizuri na kuhudumia familia (kwa wenye nazo). Asiye fanya kazi na asile.

Nina mifano hai ya ninachokizungumzua hapa japo sitawataja wahusika. Kama kichwa cha uzi kinavyosema, laana ya mapenzi ipo sema watu huwa hawaifatilii au hawajichunguzi, kiufupi umtendeacho mtu hasa kwa ubaya au kitakachomuumiza hukurudia wewe mtendaji au ubaya huja kuwapata kizazi chako kama si cha kwanza basi cha pili au tatu au nne.

Kuna baba mmoja alikuwa na mke na watoto ndani ya ndoa. Ila hakuacha kuchepuka na kuongeza watoto wa nje ya ndoa. Kati ya wadada na wamama aliotembea nao mmoja alimdanganya kuwa hajaoa na hana familia binti aliamini kabla hajapachikwa mimba, akagundua ukweli.

Huyu binti alimchunguza mke wa yule baba akagundua ni mtaratibu na mkimya. Siku moja akamfata na kumuomba msamaha yule mama kuwa amesitisha mahusiano na mumewe kwani alianzisha akijua hajaoa wala hana familia.

Hivyo aliomba msamaha na akalia sana mbele ya yule mama. (Haikujulikana kama yule mama alimsamehe au alimjibuje ila hakuanzisha ugomvi wowote wala maneno makali wala kuonesha hasira kwa yule dada).

Yule dada alifanya vile akiamini mke wa huyu baba atakuwa amelalamika na kuumia kwa mumewe kutokulala nyumbani na kuchelewa kurudi siku ambazo walikuwa wote wakila bata. Alijua iko laana ambayo mke akilia mbele za Mungu basi humpata mtesi (Mwizi wa penzi la mumewe).

Huyu binti aliamini mke wa yule baba akimsamehe basi hatopata laana iwapo akija kuolewa aidha mumewe asirubuniwe na vimada pia uzao wake usipate laana ya mapenzi ya wizi. Kufupisha habari yule baba watoto wake walikuwa na umri wa kuwa na familia zao.

Kati ya watoto wake 6 wa ndoa ni mmoja tuu ndo alifanikiwa kuingia kwenye ndoa wengine wameishia kuzaa bila kuoa wala kuolewa. Binti zake walizalishwa hovyo na vijana wa kiume hawakudumu kwenye mahusiano yao na kuishia kuleta wajukuu nyumbani. Baadhi ya watoto wa nje ya ndoa waliingia kwenye ndoa ila, ndoa zao hazikudumu wote wameacha na kuachika. Na wengine hawakuzaa kabisa yaani hawakupata uzao au walikuwa tasa.

Maneno haya aliya andika huyu baba baada ya kustaafu na kuyaweka kwenye nyaraka zake za urithi. Akaacha maandishi siku akifa hiyo taarifa isomwe kwenye msiba wake na mwisho akaweka sala fupi ya kutubu kuwa laana iliyowapata watoto wake kutofanikiwa kudumu kwenye familia zao isiwapate wajukuu zake.

Ilimuuma sana kuona uzao wake wamesoma wanamafanikio kikazi na kibiashara ila familia hawana. Na akatoa robo ya mali zake ziende kuwasaidia mayatima akiamini inawezekana pia kuna watoto wake wa nje ya ndoa waliishia kuwa mtoto wa mtaani bila yeye kujua. (Hizi ndo zile mnaita one night stand asubuhi kila mtu na lwake hamjuani majina wala anuani mimba ikinasa mtoto hamjui baba yake).

Hivo !alitoa robo ya mali zake iwe kama sadaka ya toba ili kizazi chake cha pili na tatu (wajukuu na vitukuu) wasipate ile laana. Hii habari niliisikia baada ya kuhuduria mazishi ya huyu baba miaka flani hivi huko nyuma. Kilichonisukuma kuleta hii habari hapa, ni baada ya kuona familia nyingine ikipatwa na shida kama aliyopata yule baba (miaka kadhaa tangu yule baba afariki).

Bila kufatilia kama wajukuu wa yule baba walinusurika na ile laana kwa toba la babu yao, hii familia ingine hadi wajukuu wake kwa waume waliishia kuoa na kuolewa kisha kuachika na wengine waliishia kuzalishwa na kuwapa mimba binti wa watu na vitukuu luletwa nyumbani walelewe na bibi.

Hii huwaumiza sana wazazi bila kujua kwa asilimia kubwa wao waliwaumiza binti wengi sana wakati wako vijana kwa kuwa chezea, kuwapa mimba na kuwaacha huku wakijua wazi hawana mpango wa kuwaoa. Malalamiko na huzuni na uchungu (laana) wa kuumizwa kimapenzi kwa waschana hao na wadada huwapata wahusika na mara nyingine huwapata uzao wake (mtendaji).

Iwapo hukuwa unamfahamu kitu kama hiki kipo duniani na siajabu unaweza kuta mtu anajiuliza wapi nakosea mbona wanaume wananichezea na kuniacha bila sababu ya msingi au unajistukia mschana akikwambia ana mimba yako basi unamuona kama malaika Israel mtoa roho unamkimbia hutaki hata kumuona. Chunguza uzao wenu baba na babu yako walikuwaje au babu yake baba yako.

Nafasi ya kurekebisha ipo na kukata mnyororo wa laana ya malenzi iwapo unaamini. Waweza sema siamini mambo haya kama yapo na hayanipati na mie nachezea waschana wa watu bila kujali..... omba uhai ushuhudie wajukuu zako kama watanusurika na uchungu wa uliowaumiza. Ikiwa hivo ujue wewe ni wapekee laah, labda..... uliowaumiza wasikulalamikie mbele za miungu yao.... au wakusamehe.

(Najua kuna ambao watasema hawajaelewa. ..) washee mshana jr waweza nisaidia kudadavua kwa ufanisi zaidi kuhusu hili jambo? Naamini una ufahamu nalo.

Alamsiki nyote.

Kasie Mahaba.
Yaani Kaise nikiwa katikati ya Kuosma hivi japo ulimalizia kuwa ni Wosia alioucha Baba mmoja ila Kuliniijia Majina ya embers kibao ambao wana Uhanga wa haya Mambi na Kila kukicha wanalia na hawajui wataondokaje na hii kitu.. Nice Story and it tells what goes around
 
Aisee Kasie umenikumbusha kisa fulani hivi kuna kijana nampa jina la [HASHTAG]#John[/HASHTAG] alimtia mimba bint fulani,alafu akaikataa. Baada ya miaka ya miaka kadhaa kupita mdogo wake wa mwisho na [HASHTAG]#john[/HASHTAG] alitiwa mimba na kijana fulan jiran yao,yule kijana nae akaikataa ile mimba. Miaka miwili baade [HASHTAG]#John[/HASHTAG] akaoa, kabla ya ndoa hakuwah kuzini na yule bint,usiku wa kwanza wa ndoa [HASHTAG]#John[/HASHTAG] akagundua mkewe hakuwa bikra kama alivyoambiwa kabla ya kumuoa,Mkewe akamuomba msamaha [HASHTAG]#John[/HASHTAG] na kumuomba amfimchie aibu ile, basi kwakuwa # john nae hakuwa msafi kiivyo akaamua kumsamehe mkewe. Baada ya kama miaka mitatu [HASHTAG]#John[/HASHTAG] na mkewe walifanikiwa kupata mtoto wa kike,yule bint alipofikisha umri wa miaka 5 alipatwa na dhoruba la kubakwa na mlinzi wa nyumban kwao. Baada ya lile tukio [HASHTAG]#John[/HASHTAG] alilia sana akaanza kureflect maisha yake yote kwa ujumla,akawashirikisha na viogozi wa dini juu ya ile kadhia. Akaambiwa afanye toba kwani yale yote yalikuwa yamechangiwa na ushiriki wake wa kuwaumiza mabint wakati wa ujana wake. Hakika hawa dada zetu tujitahidi kuishi nao kwa wema,kuwaumiza hakuwezi kutuacha salama.

Mama yangu alikuwa ananiambia niwafanyie wema watoto wangu ambao bado hawajaziliwa kwa kuwachagulia mwanamke mwema na maneno haya nawaambia na dada zangu humu wafanyieni wema watoto wenu mnaowatarajia kwa kuwachagulia wanaume wema vinginevyo vizazi vyetu haviwezi kuwa salama.

ZINAA NI DENI IPO SIKU LITALIPWA NA MUMEO,MKEO.MTOTO WAKO,MJUKUU AU KITUKUU ETC Cc Kasie
Asante nimekubali kuwa kuwa ZINAA NI DENI IPO SIKU LITALIPWA NA MUMEO,MKEO.MTOTO WAKO,MJUKUU AU KITUKUU
 
I believe... Biblia inasema. Chochote mtakachomtendea mmoja wenu nanyi. Mtatendewa.


Ufanyalo utatendwa.



Sent using Jamii Forums mobile app
Yap siyo kwenye mimba tu,
Lolote baya unalomtendea MTU kwa makusudi na ubabe ama dhuruma Mungu husikia machozi ya adhurumiwae,
Kwenye ngono za kawaida inaweza kuwa si sana maana mtendaji na mtendwa wote ni wazinzi na Mungu hashugulishwi na maumivu yatokanayo na dhambi maana ndo malipo stahiki,
Km mnapeana mimba huku mkijua mnazini mtavuna wote madhara ya dhambi,
Lkn kumlaghai binti makusudi,na kuahidi kumuoa au hata binti kumdanganya mvulana kuolewa nae huku ukijua unadanganya,inaweza kukuletea laana

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom