Ms mol naomba nikujibu kwanza kuhusu hili then kuhusu nafsi iliyotekwa ntakujibu mwishoni
Umeongelea issue ya mwenza mmoja kuwa mwema na mwingine kuwa majanga. Nilivyokuelewa ni kwamba is it possible watoto wa ndani ya ndoa wakarithi pia hiyo roho ya uzinzi kwa sababu mama yako ni mcha Mungu? Dhambi/laana inamtafutaga mtu mmoja (lango) ili iweze kuingia ndani na kujitawanya na kufanya uharibifu kwa kizazi chote. Kwa mfano wako, baba ndo anaweza kuwa lango la kupitishia laana ya uzinzi au na yeye ameibeba laana hiyo kutoka kwa mababu zake. So mtoto yoyote atakayepita kwenye viuno hivyo na anaweza kuibeba laana hiyo, regardless mama yake ni yupi. (Wanashare lango moja). Au kama ni laana ya ukoo fulani, watoto wote watakaozaliwa na ukoo huo wanaweza tu kurithi laana hiyo as long as ni wa ukoo huo). The same tu kwamba ni mtu mmoja tu anaweza kusimama akatumika kuiondoa laana hiyo
Yohana 6:3- "Kilichozaliwa kwa mwili ni mwili na kilichozaliwa kwa roho ni roho". Kwa hiyo mtoto anapozaliwa anakutana na ile laana tayari, unless hajajitenga na hizo laana basi hawezi kuwa salama. Kama ambavyo ili mtoto aanze kuishi an independent life lazima atenganishwe na kitovu cha mama yake, ndivyo ambavyo lazima tujitenge na laana za mababu zetu ili tusiendelee kufuatiliwa na laana hizo. Nafikiri hata wewe ni shuhuda mzuri tu, kuna watu ambao wamesimama na Mungu lakini still unaona maisha yao yana shida sehemu, yes wanamjua Kristo but hawakushughulika na historia zao ndo maana wanahangaika. Watakuwa tu free pale watakapojitenga na laana au madhabahu hizo. Dhambi anafanya mtu mmoja (lango ), ila uovu ndiyo ambao Mungu anaupatiliza hadi kwa kizazi chake cha nne. (Kutoka 20:5)
Wewe kama partner mwema mwenye maarifa juu ya ya hilo una neema ya kufanyika kuwa kuhani kwa ajili ya ukombozi wa watoto wako.
Ezekia 22:30- Nami Nikatafuta mtu miongoni mwao, atakayelitengeneza boma, na kusimama mbele zangu mahali palipobomoka, kwa ajili ya nchi, nisije nikaiharibu lakini sikuona mtu
Nyakati 7:14
Ikiwa watu wangu, walioitwa kwa jina langu, watajinyenyekesha, na kuomba, na kunitafuta uso, na kuziacha njia zao mbaya; basi, nitasikia toka mbinguni, na kuwasamehe dhambi yao, na kuiponya nchi yao.
Watenge watoto wako na laana za baba zao, hapo tu ndipo watakuwa salama. Nafikiri hili ni somo zuri sana when choosing a life partner, je mwenzi wako alivyo ndivyo unavyotamani watoto wako waje kuwa hivyo? Bila kusahau kujiuliza na wewe mwenyewe binafsi, utapenda wanao warithi tabia zako? Je familia mnazotoka zipoje? Zimebeba laana na maagano gani? etc
Kuhusu nafsi iliyotekwa please em soma huu uzi, in case of anything tuwasiliane
Mlango wa nafsi kwa jicho la kiroho.