Unaposoma sayansi ya utambuzi wa mwili tunaambiwa kuwa mwili unauwezo wa kujikinga na mashambulizi ya kiufahamu na usidhuriwe na nguvu yoyote toka nje ishu ya laana imekuwa na tafiti nyingi zenye majibu tofauti yaliyoacha maswali mengi, baadhi ya maswali hayo ni kama haya,
1.je mwili unaweza kujidhuru?
2. Je kuna nguvu gani kati ya mtoa laana na mlaaniwa?
3.je ukilaaniwa kwa jambo la uongo laana yaweza shika?
4. Je mtu baki anaweza kukulaani na ukalaanika?
5. Je jambo la haki linalaanika?
6. Je kuna nguvu gani katika maneno yatolewayo na mtoa laana?
Maswali ni mengi lakini tunaweza kujadili hayo machache kwanza.
Maneno yanakwnda mwilini na rohoni. Laana kama laana ni roho kwa hiyo ili iweze kumpiga mtu lazima inzie rohoni (katika ulimwengu wa Roho) halafu inajidhihirisha katika mwili. Laana ni halisi, ina nguvu na inafanya kazi. kuna laana zinazomuingia mtu hata pasipo kutamkia, mazingira kwa mfano kumtupa mazazi au kumdhalau mzee inaweza ukuletea laana. Pia laana inaweza kusindikizwa na matamshi. au pengine unaweza kuwa umefanya jambo linalostahili laana, ila yule mhusika anaweza kutamka maneno ya kuomba laana hiyo ibatilike na ikawa hivyo. pia laana inaweza kuja kwa vita. yaani mtu analazimisha kumlaani mtu wake au kumtamkia neno baya mtu bila hata kosa. kumbuka mwanadamu ana nguvu za Mungu nadani yake hata kama hamtii Mungu kwani Mungu alitupatia nguvu hizo. kuzitumia vibaya au vizuri ni maamuzi ya mhusika, unaweza kuamua kutamka laana na inaweza kumpata mtu kama mtu huyo pia hana ulinzi wa kimungu. kwani tunaambia Kama Mbayuayu katika kutanga tanga kwake, kadhalika Laana isiyo na sababu haimpati mwenye haki. ila ukikaa vibaya na Mungu wako hata laana za kutupia pasipo sababu zinazewa kukupata. Pia laana hurithiwa. unawea kurithi laana ya Ukoo. na hii inafuatilia nasaba. lakini pia unaweza kuangukiwa na laana ya mtu ambaye alikusudia ikakufuata wewe. inakujaje. pale mtu alielaaniwa kutokana na makosa yake mwenyewe akawa katika shida. ile laana inapokuja ikakukuta wewe ambaye uliamua kuwa tumaini la yule alie laaniwa kiasi kwamba unamuepushia adhabu ambayo aatumikia kihalali. kama mtu amelaaniwa shughulikia kwanza laana kabla ya kumsaidia unless kama ni vitu vya kawaida.
mshana jr hebu leta majibu ya hizi hoja zako, naona watu wamekosa majibu.Unaposoma sayansi ya utambuzi wa mwili tunaambiwa kuwa mwili unauwezo wa kujikinga na mashambulizi ya kiufahamu na usidhuriwe na nguvu yoyote toka nje ishu ya laana imekuwa na tafiti nyingi zenye majibu tofauti yaliyoacha maswali mengi, baadhi ya maswali hayo ni kama haya,
1.je mwili unaweza kujidhuru?
2. Je kuna nguvu gani kati ya mtoa laana na mlaaniwa?
3.je ukilaaniwa kwa jambo la uongo laana yaweza shika?
4. Je mtu baki anaweza kukulaani na ukalaanika?
5. Je jambo la haki linalaanika?
6. Je kuna nguvu gani katika maneno yatolewayo na mtoa laana?
Maswali ni mengi lakini tunaweza kujadili hayo machache kwanza.
mshana jr hebu leta majibu ya hizi hoja zako, naona watu wamekosa majibu.
Mkuu tunakusubiri utupe majibu
Kwanza kabisa laana ni roho! Laana ni pepo laana ni nguvu(energy) yanye uhai usiokamilika kwa maana ya mwili, lakini vilevile laana ni nguvu hasi yenye uwezo wa kuharibu tu na kuleta matokeo hasi siku zote!
Pili laana haina madhara kwa kitu kisicho uhai ni lazima kuwe na viashiria vya uhai hapo ndipo laana inaweza kufanya Nazi
Tatu laana chanzo asili mwenendo mwendelezo wake na hatimaye matukio yake vinabebwa na lugha au maneno iwe kwa kutamkwa au kwa kuandikwa! Maneno haya au maandishi ndio kibebeo cha hiyo roho/nguvu ya laana
Sasa swali la kwanza Je mwili waweza kujidhuru!?
JIBU ni hapana, mwili una ulinzi binafsi kwenye ulimwengu wa roho na was nyama kichachotokea ni kile kianzilishi cha laana na impact aliyonayo mtoa laana kwa mlaaniwa lakini kwa mazingira fulani
Mzazi kwa mfano ana connection ya moja kwa moja nawewe hivyo roho yake inapoumia na JAMBO LA HAKI roho na mwili havina uwezo wa kuzuia shambulizi lolote toka kwa mzazi
Swali la pili no nguvu aliyonayo mtoa laana kwenda kwa mlaaniwa
Tumeshafahamu kuwa laana ni roho na roho ni uumbaji hivyo uumbaji hauchezewi kwa namna yoyote ile
Kwahiyo linapotokea jambo lenye kuumiza uumbaji halo lazima laana ifanye kazi
Maswali matatu ya mwisho majibu yake hayatofautiani sana na majibu halo juu lakini pia kuna ile perception kwamba mtu aliwazalo ndio huwa kuna baadhi ya laana hutokana na sisi wenyewe na matendo yetu bila hata kulaaniwa na wengine hii ni kwakuwa roho yako mwenyewe inakuwa haikubaliani na matendo yako mwenyewe.....
Ngoja niishie hapa kwanza ili niruhusu maswali na ufafanuzi
Mind na imani inaweza tumika kuzuia laana. Maana akili zetu na mawaza yanaweza kuwa msingi wa kutuweka sehem sahihi au sehem pabaya, kama mtu haamin hizi ishu zinaweza kuwa na impact kwake ?
Cha kwanza na muhimu kuliko chochote ni roho lazima iwe hai na connection kati ya roho mbili au zaidi kwahiyo hata kama huamini lakini ile core ya uhai kama iko live na jambo hilo ni la haki basi hata kama huamini lazima kuathirika kupo kwa namna moja au nyingine
Laana ikisha shika, mtoa laana anaeza tengua laana hii kwa process zipi ?
mwili una ulinzi binafsi kwenye ulimwengu wa roho ina maana ulinzi huo unaweza kuzuia magonjwa?
mbona watu wanaumwa?
roho ni nini?