Kwikwi (Hiccups): Chanzo na Tiba (matibabu) yake

Hili tatizo limekuwa likinipata mara kwa mara, kuna kipindi ilinichukua zaidi ya saa tisa hadi ikabidi niende hospitali,nilikunywa maji haadi yakawa yanamwagika nikiinama! nilikwenda marie stopes pale mwenge wakanichoma sindano fulani (siikumbuki), ilinilevya nikajikuta nalala pale bila kujitambua lakini tatizo lilitulia kwa muda mrefu, siku hizi ikianza tuu huwa nachukua ndizi mbivu au muwa nikila tu inapotea, hii niliambiwa na mama yangu lakini sijui uhusiano uliopo baina ya hivi vitu viwili na tiba ya kwikwi, hebu jariibu na wewe inaweza kukusaidia.
 
Wakuu naomba kuuliza wataalamu na wataaluma,hivi ni nini kinasababisha kwi kwi?
 
kwikwi husababishwa na matatizo yanayohusisha neva au misuli ya upumuaji hasa diaphragm. mfano kula haraka haraka, kula chakula au vinywaji vyenye gesi, kula vyakula vyenye viungo vingi, magonjwa ya ini au mapafu, operation za tumbo(abdominal operations), madawa kama valium nk. kwa ujumla chochote kitakachosababisha irritation of the phrenic nerve.
 
Kwikwi ni dalili ya phrenic nerve irritation au raised serum urea kama mafigo hayafanyi kazi vizuri. Kama umekula ANTIACID tabs/PPI na hupati nafuu bora uende hosp. ukafanyiwe serum createnin na urea kuangalia ufanisi wa figo zako.
 
Wakuu naomba kuuliza wataalamu na wataaluma,hivi ni nini kinasababisha kwi kwi?
Rahisi tu, kuna mchangiaji mmoja hapa amesema kama antiacid hazijakusaidia basi uende hospitali, kwahiyo ni kama kusema asidi inaelekea kuzidi alkalini mwilini mwako. mwilini lazima ubaki katika hali ya ualikalini mara nyingi zaidi kuliko katika asidi. maelezo ni mengi sana, kwa ufupi unatakiwa kula na kunywa vyakula au vinywaji vingi vyenye alkalini zaidi kuliko asidi, sasa ukiacha mboga mboga za majani, matunda na maji au maji/chumvi, vitu vingine vyote vilivyobaki ni asidi, kwahiyo nyama, samaki, chipsi, kuku, kitimoto, soda na vingine vingi ni asidi. Jaribu hivi: kila nusu saa kabla ya kula chakula, kunywa glasi moja ya maj. www.maajabuyamaji.com
 
NDUGU ZANGU,

Naomba mnijuze hivi kupiga kwikwi kunamaanisha nini kibaiolojia? Kuna wengine wanasema ukiona unapiga kwikwi ujue mtu wako wa karibu anakusema au anakuwaza. Najua ni sababu isiyo na maana na kwamba lazima kuna maelezo ya kisayansi. Tafadhali wataalam karibuni.
 
Inaweza ikawa kiu au sign ya ugonjwa au kuna sehemu juu ya kifua haina gas ya Co2
1.Kunywa maji kwa kasi,au
2.Chukua mfuko wa nylon ziba mdomo na pua kisha uwe unapumulia humo na kuvuta hewa huo kwa sekunde kama 30 hiv

Lengo ni kupata carbondioxide gas na kama ilisababishwa na kiu basi itaisha.

kama ikiendelea muone daktareee
 
nilisikia inasababishwa na hewa kujaa tumboni ndio maana mtu akinywa maji yanaenda kuidisplace na kwikwi kuisha, au mtu mwenye kwikwi ukimshtua ule uoga anapumua kwa nguvu na hewa hutoka na kwikwi huisha, ila kama haiishi linaweza kuwa tatizo la kiafya na kuna dawa zake
 
Ziba pua na mkono alafu vuta hewa ndani kwa mdomo fanya kama alafu meza . Rudia tena haraka haraka bila kuachia hewa itoke nje .jitahidi kurudia kadri ya uwezo wako kwani itakua ngumu kidogo.

Jaribu inaweza kusaidia.
 
kwikwi inatokana na hewa kujaa tumboni so kunywa maji mengi ui displace. unakumbuka mambo ya downward dispacement upward delivery? chemistry ya form one.
 
Kiongozi kama ni kwikwi ya kawaida ambayo haijasababishwa na ugonjwa wowote,Tafuta Ganda la muwa,lichome halafu nyonya maji yake ni issue ya fraction of a seconds kwikwi itakuwa imekwisha kabisa Inshallah (Kwa hisani ya marhum bibi 'MAY GOD REST HER SOUL IN PEACE').
 
Kiongozi kama ni kwikwi ya kawaida ambayo haijasababishwa na ugonjwa wowote,Tafuta Ganda la muwa,lichome halafu nyonya maji yake ni issue ya fraction of a seconds kwikwi itakuwa imekwisha kabisa Inshallah (Kwa hisani ya marhum bibi 'MAY GOD REST HER SOUL IN PEACE').

asante sana mdau....
 
kwikwi inatokana na hewa kujaa tumboni so kunywa maji mengi ui displace. unakumbuka mambo ya downward dispacement upward delivery? chemistry ya form one.

daaaah,,,sasa ndo nahusianisha matukio mdau,,,jana nilikua na pilikapilika nyingi,nikaingia kwenye mgahawa mmoja hapo kariakoo baada ya kula tu,,,tumbo lilijaa sana nikawa nabeua mno,,,,just 30 mins baada ya kula,nikahisi ule MSOSI ULIKUA UMEWEKWA HAMIRA,baada ya maelezo yako now napata jibu,asante sana
 
Back
Top Bottom