Titizo la mtoto kunyonya anatoa sauti kama ya kwikwi

escrow

JF-Expert Member
Sep 27, 2016
371
321
Jf doctor naomba ushauri, mimi na mke wangu tumepata mtoto ambaye kwa sasa umri wake ni miezi 2.
Mtoto huyu ana tatizo ambalo imekuwa ngumu kwetu kuelewa, ni kwamba akiwa ananyonya anatoa sauti kama vile kwikwi, hivyo bado ufahamu wetu kwenye tatizo hili hatuna.

Jf doctor naomba ushauri ndugu zangu hili tatizo limekuwa linaongezeka kila siku na wakati mwingine anakuwa kawaida tu.

Naomba kuwasilisha, natanguliza Shukrani za dhati.
 
Mimi sio daktari, Ila mama ajitahidi kumuweka mkao mzuri anapomnyonyesha (wanaelekezaga clinic), asimnyonyeshe akiwa amelala, ahakikishe amekaa na mtoto amshike vizuri, ahakikishe mtoto anapata sehemu kubwa ya chuchu Ili kuzui hewa kuingia anaponyonya....kisha akimaliza kumnyonyesha ahakikishe anamtoa gesi tumboni Kwa kumuweka begani na kumpiga piga mgongoni.
 
Sijui kuna uhusiano gani hapo lkn nnachokijua ni kwamba mtoto mchanga akiwa anasumbuliwa na kwikwi ya mara kwa mara basi dawa yake ni kunyofoa nyuzi kutoka katika nguo aliovalishwa au kama ni kitenge alichowekwa na hiyo nyuzi unailowesha na mate kidogo unaipachika kwa paji la mtoto mda kidogo utaona mtotot anakaa sawa haichukui muda sana ,

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom