Kwetu Yanga 'head to head' ni akiba tu, tunaenda robo fainali tukiwa vinara wa kundi

SALOK

JF-Expert Member
Sep 20, 2011
3,318
1,936
Naam, hakuchi, hakuchi kumekucha..
Siku nyingine tena tumeamka tukiwa na furaha, baada ya mbugi kali baina yetu sisi mabingwa wa kutandaza soka la kisasa na la viwango hapa TZ na waarabu wa Aljeria kisha kuibuka na ushindi mnono uliotuhakikishia kuingia robo fainali ya kombe la klabu bingwa Africa, kwa kipengele cha kisheria ya H2H.

Nipende kusisitiza na kuuhakikishia Umma kwamba Yanga Africa aka Wananchi tutamaliza kundi tukiwa on top. Tunaenda kumpiga Al-ahly kwao na kufuta dhana ya kwamba Al-ahly hawezekani!

Yes Yanga hii ya Gamondi inakazi moja tu, kufuta dhana za kwamba kuna mambo fulani ktk soka la Nchi yetu hayawezekani.

Yale yasiyowezekana kifikra za watanzania walio wengi kwa Yanga hii ya sasa yanawezekana!
MKAE KWA KUTULIA Na MTAONA.
TIME WILL TELL....
WANANCHI GOOOOO......!!!!!!!
[Cairo Misri ]Full time; Al-ahly 0 vs Yanga 1.
 
Naam, hakuchi, hakuchi kumekucha..
Siku nyingine tena tumeamka tukiwa na furaha, baada ya mbugi kali baina yetu sisi mabingwa wa kutandaza soka la kisasa na la viwango hapa TZ na waarabu wa Aljeria kisha kuibuka na ushindi mnono uliotuhakikishia kuingia robo fainali ya kombe la klabu bingwa Africa, kwa kipengele cha kisheria ya H2H.
Nipende kusisitiza na kuuhakikishia Umma kwamba Yanga Africa aka Wananchi tutamaliza kundi tukiwa on top. Tunaenda kumpiga Al-ahly kwao na kufuta dhana ya kwamba Al-ahly hawezekani! Yes Yanga hii ya Gamondi inakazi moja tu, kufuta dhana za kwamba kuna mambo fulani ktk soka la Nchi yetu hayawezekani..
Yale yasiyowezekana kifikra za watanzania walio wengi kwa Yanga hii ya sasa yanawezekana!
MKAE KWA KUTULIA Na MTAONA.
TIME WILL TELL....
WANANCHI GOOOOO......!!!!!!!
[Cairo Misri ]Full time; Al-ahly 0 vs Yanga 1.
Tunampiga nyingi Alhly Cairo

Yanga bingwa CAFCL

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hongera sana kwa viongozi wa Yanga, benchi la ufundi na wachezaji.
Upande wa mashabiki, kwa ukubwa wa Yanga kwa kweli inatia aibu sana. Mashabiki wa Yanga wengi wamekuwa na kelele mitandaoni na mitaani, lakini kwenye mahudhurio hakuna kitu kabisa.
Sitashangaa kama yale mahudhurio ya jana, nusu walikuwa ni mashabiki wa Yanga na nusu ni mashabiki wa Simba.
Mahudhurio ya jana hayana tofauti na mahudhurio ya mechi kati ya TP Mazembe na waarabu iliyofanyika Benjamin Mkapa. Yaani wenyeji tena timu kubwa kama yanya inashindana na wageni waliojamishia mechi yao nchini.
 
Back
Top Bottom