Robo fainali na Al Ahly Vs Simba iongeze uwekezaji wa mbinu katika maeneo haya

Mwadilifu Mdhulumiwa

JF-Expert Member
Jul 22, 2021
418
630
Siku ya Tarehe 29 Mwezi huu wa March 2024, Timu ya Simba itatupa karata yake ya mchezo wa mkondo wa kwanza wa mechi za robo fainali dhidi ya miamba ya soka Afrika, Al Ahly Sporting kutoka nchini Misri . Sote tunatambua ugumu na umuhimu wa mchezo huo ambao kwa upande wa Simba ndio utakaotoa mwelekeo wa ama kuvuka hatua hiyo au kuumaliza mwendo tukiwa hapahapa nchini hasa ukizingatia mechi ya mkondo wa pili Simba haitakuwa nyumbani tena, hivyo mipango yote kuhusu kusonga mbele Simba inapaswa kukamatia hapahapa kwenye mchezo itakaocheza nyumbani.

Katika kuhakikisha hesabu hizi zinakamilika tukiwa hapahapa nyumbani, Pamoja na mambo mengine, Benchi la ufundi Simba halina budi kuongeza mbinu za kivita katika kikosi chake kwenye maeneo yafuatayo;-

1.SPEED
Simba imekuwa na utamaduni wa kupiga zaidi soka la taratibu, madhara ya aina hii ya uchezaji mkikutana na timu inayopiga mpira wa kasi, huwafanya kuchoka haraka na hivyo kuwa hatarini kupoteza mchezo. Al Ahly wana uwezo wa kupiga mpira wa haraka, na wenye usahihi katika maamuzi na matendo. Hivyo Simba inapaswa kuwekeza kwenye soka la speed ili kuendana na kasi ya wapinzani wake. Faida ya kucheza mpira wa kasi ni kwamba;
  • Kwanza husaidia katika ukabaji pale timu inapokuwa haina mpira kwani inasaidia kuwavamia wapinzani na kuwapoka mpira kabla hawajiandaa kupanga shambulizi.
  • Pia katika upande wa ushambuliaji, huwezesha kulifikia lango la wapinzani kwa haraka na pengine kupachika bao kabla hawajajiandaa kutibua mipango ya shambulizi.
2. USHAMBULIAJI WA MIPIRA YA KONA
Kwasasa Simba imeonekana kutokuwa na mfumo mzuri wa ushambuliaji wa mipira ya kona inazopata. Katika mechi kadhaa , Simba imekuwa ikipata kona nyingi lakini zote zinaishia kuwa tasa, kinyume na matarajio ya sayansi ya mpira. Katika sayansi ya mpira tunaamini kona ni nusu ya penalty, hivyo kama timu husika itawekeza vyema katika mbinu za ushambuliaji wa hizi kona ni vyanzo muhimu vya mabao na ushindi kwa timu husika.

Kuna mbinu kadhaa za ushambuliaji wa kona ambazo zikichezwa kijanja huweza kuzaa mabao;-
  • Mbinu ya kwanza ni ile ya kuutokea mpira wa kona na kupiga kichwa cha mbizi au kichwa cha hewani mbele kidogo ya mlingoti wa goli kuelekea upande inakopigwa kona, vichwa vya aina hii husaidia kuchepusha mipira na kuilekeza langoni katika namna ya kumshtukiza kipa na walinzi wake na kuzaa bao, Mshambuliaji Medie Kagere aliwahi kufunga mabao ya aina hii zaidi ya 3. Kibu, Malone Fondo na Kanute wakiandaliwa vema wanaweza kucheza hii trick.
  • Mbinu ya pili ni kumsimamisha mchezaji mrefu kama fabrice Ngoma au Innonga mbele kidodo ya mlingoti wa goli toka inakopigwa kona, mchezaji huyu anaweza kutumika kumuhadaa kipa kiaina, kisha wachezaji wa nyuma yake wakamalizia mpira na kuipatia timu bao.
  • Mbinu ya tatu ni kuanzisha shambulizi la kona kutokea pembeni kisha inapigwa pasi ndefu ya chinichini kwenda kwa wamaliziaji katikati nje ya 18. Katika shambulizi la aina hii mshambuliaji aliyeandaliwa anatakiwa kuwa na wazo moja tu la kuunganisha kombora langoni bila kutuliza wala kugugumiza.
Kwa timu kama Al Ahly ambayo 90% ya wachezaji wake na hasa mabeki wote ni warefu, sishauri Simba ishambulie kwa mipira ya juu vinginevyo itawapa faida zaidi wapinzani wao.

3. SAIKOLOJIA YA WACHEZAJI KATIKA MAAMUZI SAHIHI
Baadhi ya wachezaji wa Simba na hasa washambuliaji wamekuwa na tatizo la kutokuwa na maamuzi sahihi wanapolikaribia lango la wapinzani wao. Si kila mahala ukipiga shuti unaweza kufunga goli au si kila sehemu ni pa kutoa pasi kwa mchezaji mwingine. Kwa Mfano Saido Ntibazonkiza, Jobe na Fredy wana tabia za papara wanapolikaribia lango la wapinzani wao. Wachezaji hawa hupiga mashuti hovyo hata mahali ambapo mchezaji mwenzake tayari alikuwa ameshajiweka kwenye nafasi nzuri ambayo lait kama angempa huo mpira labda timu ingeweza kupata bao. Ni hawahawa akina Saido, Jobe na Fredy ambao akiwa na mpira badala ya kutoa pasi kwa mtu aliyefungua , yeye anaanza kupiga chenga na mwishowe anapoteza mpira. Hivyo bench la Simba liwakalishe chini wachezaji hawa na kuwapika kisaikolojia. Watambue kuwa timu tunayoenda kucheza nayo ni timu makini hivyo wasitegemee kama wapinzani wao watakuwa wa kufanya makosa mengi au kutoa mianya ya kuruhusu mashambulizi mengi kiurahisi. Hivyo wanapaswa kutulia na kutumia kikamilifu nafasi chache za mabao watakazozipata.

4. KUWA WEPESI KATIKA KUBADILI MFUMO WA UCHEZAJI NA WACHEZAJI
Ni jambo la kawaida kwa timu kuingia na aina flani ya uchezaji , lakini kwa bahati mbayamfumo huo ukawakaba! Hivyo ni vizuri sana kwa timu kuwa na mifumo mingi ya kiuchezaji kama plan B, iwapo mfumo watakaoingia nao utawakaba. Mabadiliko hayo yanaweza yasiwe kwa aina ya uchezaji tu bali hata aina ya wachezaji ambao timu ilianza nao lakini mfumo ukawakataa. Mathalani katika mchezo dhidi ya Azam Beki Husein Kazi alishindana na mfumo, alikuwa wa kumtoa ndani ya dadkika 15 za mwanzo lakini benchi la ufundi la ufundi lilimuacha mpaka tukafungwa goli na kukoswakoswa mengine ya hatari. Lakini pia Kiungo Babacar pamoja na ukabaji wake , anacheza mpira wa taratibu kupita kiasi, anapaswa kurekebishwa haraka au kuwekwa bench asome kwa akina Kanute na Mzamiru.

Aidha Simba wawe wepesi pia katika uchezaji wa faulo. Kuna faulo nyingine sio za kusubiri mpaka refa akachore mstari na kuwapanga wapinzani pa kusimama, Sheria inaruhusu kuanzisha faulo fasta bila kusubiri filimbi ya refa labda tu kama faulo hiyo sio ya kucheza watu wawili. Hili pia linatakiwa kufanyika kwenye mipira ya kurusha, Simba wanapaswa kuwa sharp katika kuianzisha mipira hiyo kabla wapinzani wao hawajajipanga sawasawa.

HITIMISHO
Na mwisho nitowe wito kwa Simba kuyasahau kabisa, matokeo waliyoyapa katika mechi zao za African Supper League dhidi ya Al Ahly ambapo walimudu kutoka nao sare ya 2-2 kwa Mkapa na kisha 1-1 kule Cairo Misri. Matokeo hayo yasiwafanye wabweteke sababu hata pamoja na matokeo hayo bado Simba ilitolewa mashindanoni kwa faida ya goli la ugenini. Simba wanapaswa kuwaheshimu Al Ahly na kucheza nao kwa tahadhari kubwa, huku wakiweka juhudi kubwa kwenye kuhakikisha wanatoka na ushindi wa kutosha kwenye dimba la Mkapa ili wakienda misri shughuli ikawe kulinda ushindi tu!

MUNGU IBARIKI SIMBA, MUNGU IBARIKI TANZANIA.

 
Al Ahly hawachezi kwa kasi ugenini.

Al Ahly weakness yao ni kucheza set pieces.
 
Umeongea vitu vya maana Ila kwa kuongezeka.wawashauri wachezaji wao wasikae na mpira muda mrefu Hadi adui akapata muda wa kujiandaa.
Shabalala, Mzamiru, Saidoo na Kibu Dennis ni baadhi ya wachezaji wanapopata mpira hawafanyi maamuzi ya haraka hapo naongezrs na Inonga.
Kwa beki Shabalala asijisahau.akawa anataka aonekane winga huwa anampa.kazi Sana Marlone, pale katikati Simba wanaposhambuliea huwa Kuna ueazi mkubwa sababu Simba Mara nyingi wanaposhambuliea wanakimbilia golini badala ya kukaba watu.
Mara nyingi Kona inapopigwa kuelekea Simba wachezaji wengi wanajazana golini badala ya kukaba wasianzishe Kona fupi.
Pale mbele Saidoo na Kibu waache papara na kutaka kufunga wajitahidi wanapopata mpira waachie haraka kwa wenzao.
Jobe asiwe anakimbia mbele awe anajiposition vizuri.
 
Back
Top Bottom