Kwenye hili la COVID19, naweza kuona mahesabu ya Rais Magufuli. Je, tumuunge mkono?

Kwa hiyo serikali yetu inakusudia watu 1,721,996.6 wafe ili kufikia hiyo herd immunity?

Death rate ya COVID19 Taniania ni 4.13% =(21/509 x 100%)

70/100 x 59,545,138 =41,681,996.6

4.13/100 x 41,681,996.6= 1,721,450.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu jmushi, mara nyingi huwa mvivu wa kusoama makala hizi ndefu, lakini nimeona hiyo sentensi inayohusu 'demography'; halafu nikafikiri ndiyo unayoihusisha na kichwa cha habari ya mada yako.

Nataka tu nikuulize swali juu ya uhusiano huo na maamuzi yaliyofanywa na rais.

Hivi unafikiri wakati Rais Magufuli anaamua aliyoamua kuhusu jinsi ya kuikabili coronavirus wakati huo, kilichomsukuma kufanya maamuzi hayo ni hiyo 'demography' ya population yake?

Umewahi kusikia nchi yoyote iliyofanya maamuzi kuikabili coronavirus kwa kuitegemea 'demography'?

Je, taarifa za coronavirus kushambulia wazee na watu wenye matatizo zaidi ziliwahi kufanyiwa uchunguzi popote na machapisho yake yakawepo ya kuweza kuwaongoza watu wanaofanya maamuzi kuzitumia taarifa hizo (based on scientific study and publications).

Kama uamzi aliochukua Magufuli unayategemea majibu ya ndio kwa maswali hayo, basi na mimi niweke kwenye orodha ya kumpa hongera nyingi kwa uamzi wake huo.

Vinginevyo, maamzi yake hayatofautiani na mcheza kamali; tofauti pekee iliyopo ni kuwa kamali hii iliweka rehani ya maisha ya waTanzania.

Coronavirus, bado haijulikani sababu zinazosababisha pawepo na tofauti kubwa ya mashambulizi katika nchi za kiafrika, ikiwa ni pamoja na hiyo ya 'demographics.
Nina hakika sababu zitajulikana muda si mrefu. Joto/mionzi ya jua na unyevunyevu vikiwa sehemu ya sababu hizo.

Sasa kama yeye tayari alikuwa na ufahamu wa hayo yote alipofanya uamzi, basi tunaye Rais mwenye uwezo wa ajabu sana!

Mimi ningekuwa karibu na Magufuli, ningemshauri awatumie wataalam wake wa afya wafanye utafiti wa kujua bahati yetu hii inatokana na nini, ili kama ni kitu tunachoweza kuwauzia wengine, basi biashara itanoga sana!

Sijui kama kwenye maandishi yako humo umeweka mchango mkubwa wa sala zetu kwa Mungu? Kama sababu ndiyo hiyo, pia itakuwa ni faida kwetu kwa sababu tutawafundisha dunia yote jinsi ya kuwasilisha maombi kwa Mwenyezi Mungu ili ayakubali. Sio kujisalia tu kama wao wanavyofanya. Tutawafundisha.

Au ni dawa yetu ya 'kujifukiza' na tangawizi, limao..., na nini tena?
Hoja fikirishi

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hapa ni Survival of the fittest. Wenye immunity Ngangari watapita,wale afya mgogoro wata R.I.P.
 
Wewe ndiyo unaongelea kijumla. Na mbaya zaidi unaongea ujinga mtupu. Ukiona umepingwa kwa hoja unasema ni chuki binafsi. Hizi shule za kukariri ni shida sana!
Huwezi kuimba pambio watu wanakufa wengi, ukiombwa takwimu unakimbilia kubishana akili na uelewa.

Kwani watu wameanza kufa kipindi cha corona tu? Halafu unajiona una akili, kutwa unashindwa jamii forum kutukana watu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu kwanza tuweke baadhi ya mambo sawa

Herd immunity inapatikana pale population kwa kiwango fulani inapojenga immunity
1. Kupitia vaccination, kwamba, 80% kama sikosei ikiwa na immunity, 20% inalindwa
2. Pale ugonjwa unapokuwa na tabia ya kutengeneza ''immunity'' na hasa viral infections

Hakuna vaccination ya ugonjwa COVID-19
Hakuna ushahidi kwamba COVID-19 mtu akipata hatapata tena, ironically, kuna matukio ya kujirudia

Hapa inatueleza mambo kadhaa kuhusu viongozi. Kwamba, wanataka watu washangilie bila hoja ya kisayansi.

Kushangilia ni katika kufunika kile kinachoendelea na kuaminisha umma na dunia hakuna Corona Tz

Hilo linafanyika sambamba na kutotoa takwimu ili kujenga mazingira siku ikifika kwamba tumeshinda.

Mathalani, utasema vipi tuna korona ikiwa huna takwimu? na utasema vipi haipo ukiwa huna takwimu?

Jibu lolote lile ni sahihi kwasababu hakuna msingi wa kupinga au kukubali kwa maana ya takwimu.

suala la umri, hali ya hewa ya joto n.k. ni vitu tusivyoweza kufanyia tathmini kwasababu havisimami vyenyewe bila kuwa na nguzo nyingine.

Katika mambo yanayonishangaza ni pamoja na kuingiza masuala ya dini katika shughuli za serikali.
Kwamba watu wanataka imani zao ziwe imani za Taifa, nadhani hatutendi haki kwa wengine na wasioamini

Serikali haina dini, kazi hiyo iachwe kwa watu binafsi.
Mambo ya maombi si ya kitaifa, Tanzania ina watu wa imani tofauti na wasioamini .

JokaKuu Pascal Mayalla
Umewakilisha vyema sana

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kalamu

JPM hakuweka rehani, aliamua

1.corona haiishi leo hata kesho
2.corona can be controlled na wahusika wa eneo husika kwa njia zao

3.kesho kikitokea kirusi kingine utakimbilia ndani?

4.maisha ya watu na kula yao inategemea kazi ya siku wangeishije? Na jibu utakalotoa mpaka lini?

5.mbona lockdown dunia nzima imeshindwa watu wanarudi mtaani na watapata tena na tena

6.Nani alikuwa na solution sahihi??


Hakuna chochote ambacho rais angeamua bila kupata upinzani wa aidha nyie mnaojifanya wasomi au wananchi kupinga

Lockdown hata JPM angeamua, wananchi wangeingia mitaani

Nyie mnaishi mikocheni nyumba za kurithi na kupokea kodi kila mwezi, mimi natoka home asbh sijui familia yangu itakula nini...you cant lock me down, never

Acheni upuuzi wa kujiona mna akili na soon mtaaibika

Mpaka leo hauoni trend ya dunia inarudi kwenye solution za sweden na Tanzania?

Viongozi wa sweden unawaitaje???
Shida ya Bavicha UJUAJI UCHWARA mwingi. Hilo desa la jamaa limejaa UPUMBAVU mwingi sana hadi kujibu unaona uvivu .

Senti bai yuzingi tecno T301
 
Kwahiyo lengo la kuficha data ni nini? Hofu?
Utakavyoona wewe kama zinafichwa.

Iwapo mmoja wa familia au ndugu yako amekufa unataka jamii ijue, twambie tu idadi yao. Na mwingine, humu JF, mitandao ya kijamii, waandishi wa habari, viongozi wa kisiasa ngazi za chini, nk wakiwa tayari kutaja, kama wewe, tutakuwa tumepata takwimu za maambukizi na vifo, hata kama Serikali itaficha.
 
Asante sana mkuu. Hata mimi nakubali kabisa. Magufuli anachopania hapa ni uchaguzi tu. Anajua kabisa wananchi wengi wanaamini kuwa lockdown ni kuwanyima watu kutoka nje ya nyumba zao kabisa kwa muda fulani. Amechukuwa hili neno ili kuwatisha watu huku akiwahakikishia kuwa yeye anawapenda na kuwajali sana ndiyo maana hataki lockdown. Ni mnafiki mkubwa. Mkuu mpaka sasa wamekufa watu wengi sana kwa corona ila idadi imefichwa. Maabara ya kupimia imeingiliwa na sababu za vifo vingi hazionyeshi tena kama watu wamefariki kwa corona hata kama ndiyo sababu ya kifo. Hii yote ni kuwa anajaribu kukwepa ushahidi siku zijazo kwa sababu kama watakuja kufuatilia kuna uwezekano mkubwa wa kujua idadi kamili. This guy is just a killer by nature na hataki ushauri wowote tofauti na anavyotaka yeye. Hata wizara ya afya ameondoa wale wote waliokuwa angalau wanaonyesha utaalam na kubakisha wale manyumbu. In fact nchi nyingi sana zimekiri kuwa lengo la lockdown siyo kumaliza tatizo bali ni kuokoa maisha ya wananchi kwa kufanya watu wengi wasiugue kwa wakati mmoja na hospital zikaelemewa. Hata kwa wale wanaotaka ''herd immunity'' ni kuwa wanasema ni lazima kuwa na namna ya ku-control wingi wa watu wanaougua kwa wakati mmoja ili hospital ziweze kuhudumia wale ambao watazidiwa. Kinachonishangaza ni kuwa Magufuli anakasirika na kubeza anapoona watu wamevaa maski au wanachukuwa tahadhari nyingine za kibinafsi ambazo haziingiliani na ujenzi wa Taifa hata kidogo. Narudia tena mpaka sasa ni watanzania wengi wameshafariki kwa korona, na hivi vifo vingeweza kuzuilika kabisa. Iko siko mambo yatajulikana tu kwani sasa hivi namna madaraka yamelevya watu mpaka kujiona watadumu hapo walipo milele.
Hiyo idadi kubwa waliokufa na kuficha kuna familia au ukoo wako?

Senti bai yuzingi tecno T301
 
Wewe ndio ulitakiwa uweke sawa, ukweli ni upi.

Sio kuanza kuhoji elimu ya mtu.

Stupid kabisa

Sent using Jamii Forums mobile app
Niweke nini sawa na wakati wewe ulitakiwa uulize maswali? Badala yake unabugia matango pori kisha unilaumu mimi?

Hata kama unasema “dunia inajizungusha kwenye muhimili wake”, unadhani hautaulizwa umejuaje?

Kimsingi kama jibu ni la kisayansi, basi kuna research imefanyika. You can’t just own it! You’ve got to give credit where it is due.

Tafadhali chunga kauli.
 
Tupac,umekuja na uchambuzi mzuri.Idadi ya vijana ni kubwa sana nchini.Ulichokiandika ni sahihi na ndicho kimetokea Tanzania.Kwenye miji ambako kuna misongamano vijana ni wengi sana (U30) na hawa Corona haiwasumbui.Kwenye hili Mhe.Rais alikuwa na yuko sahihi hata kama alibahatisha (na kwa kweli umaarufu wake umepanda).Watu wasilazimishe watu wafe kwa Corona kama equation inagoma.Leo nimepita Kariakoo duh kuna msongamano hatari na watu ~80% hawajavaa Barakoa,ukiangalia ule umati asilimia karibu 90 ni U30.
 
Umejiuliza kwa nini nchi zenye utajiri kuliko Tz zinaondokana na "Lockdown" kuchukua hatua za Rais Magufuli kudhibiti maambukizi? Au huko kirusi cha korona kimesambaratishwa?
Ni upotoshaji wa kijinga kuhusisha hatua wanazochukua nchi zilizoweka 'lockdown' na "hatua za Rais Magufuli kudhibiti maambukizi."

'Actually', sio upotoshaji, ni ujinga.
 
Utakavyoona wewe kama zinafichwa.

Iwapo mmoja wa familia au ndugu yako amekufa unataka jamii ijue, twambie tu idadi yao. Na mwingine, humu JF, mitandao ya kijamii, waandishi wa habari, viongozi wa kisiasa ngazi za chini, nk wakiwa tayari kutaja, kama wewe, tutakuwa tumepata takwimu za maambukizi na vifo, hata kama Serikali itaficha.
Kuna utaratibu wa kutoa taarifa kwenye vyombo vingine kama mataifa mengine yanavyofanya. Je kuficha ni jitihada za kuepuka hofu? Ama ni uoga kwamba hata hao wataokufa ikijulikana italeta matatizo kisiasa?
 
Tupac,umekuja na uchambuzi mzuri.Idadi ya vijana ni kubwa sana nchini.Ulichokiandika ni sahihi na ndicho kimetokea Tanzania.Kwenye miji ambako kuna misongamano vijana ni wengi sana (U30) na hawa Corona haiwasumbui.Kwenye hili Mhe.Rais alikuwa na yuko sahihi hata kama alibahatisha (na kwa kweli umaarufu wake umeoanda).Watu wasilazimishe watu wafe kwa Corona kama equation inagoma.Leo nimepita Kariakoo,o duh kuna msongamano hatari na watu ~80% hawajavaa Barakoa,ukiangalia ule umati asilimia karibu 90 ni U30.
Well said! Sasa wewe umenisoma fresh kabisa.
 
Kimsingi kama jibu ni la kisayansi, basi kuna research imefanyika. You can’t just own it! You’ve got to give credit where it is due.
A very profound statement, that unfortunately is losing meaning (or has no meaning) for most of our fellow citizens.

This is a very serious issue that we are bound to pay a heavy penalty for it.

And very unfortunately, the perpetrators of such belief are the political leaders, who in fact supposed to know better.
 
Back
Top Bottom