Kwenye hili la COVID19, naweza kuona mahesabu ya Rais Magufuli. Je, tumuunge mkono?

Hataki tume huru ije nchini
Mhn! Hoja fikirishi hii!
Kilio/madai ya Tume Huru ya Uchaguzi siyo agenda sahihi ya kunishawishi mimi mpiga kura kumchagua kiongozi anayefaa bali ni fikra/dhana potofu ya mgombea dhaifu kutaka ushindi.

Mgombea anapaswa kunadi Sera zake ambazo wapiga kura wataamini zinaweza kuondoa kero za Kijamii, Kisiasa na Kiuchumi kuliko za kiongozi aliyeko madarakani.

Kwa mfano wa mpira wa miguu, refa anaweza kuchangia katika ushindi pale tu timu itakuwa imeonyesha uwezo wa kusakata kambumbu, lakini hawezi kuibeba timu dhaifu
 
Great thinking, nakupa big up kwa hili!



Wanajamvi, nimeona nianze kwanza na hako kakipande hapo juu ili niweze kwenda kwenye hoja yangu moja kwa moja!

Kwanza niseme nimekuwa nikisumbuka sana na hali inavyoendele nchini, kana kwamba kiongozi mkuu na wasaidizi wake kuna jambo wao wanalifahamu lakini sisi hatulifahamu!

Hata hivyo, juhudi zote za kujiuliza na kijifikirisha, zimepelekea mimi kuja na wazo hili. Kwasababu ni wazi tumetofautiana wengi wetu na kama Taifa kuhusiana na namna serikali yetu inadeal na hii world pandemic!


Scenario ninayodhani inachukuliwa Tanzania.

Kama data zinavyoonyesha, ni kwamba Tanzania ina idadi ya vijana ambao ni asilimia 90 ya Watanzania wote. Wazee wenye miaka 64 na kuendelea, ni asilimia 3.1 tu ya wananchi wa Tanzania. Ina maana tuna risk ndogo sana inapokuja kwenye corona. Na wengi wenye magonjwa sugu wanaangukia kwenye group la wazee.

Sasa kuna aina mbili za immune ambazo zinafahamika na kukubalika duniani kote, nazo ni...

I)kupitia chanjo(vaccine)

II)Kupitia “herd immunity” ama kinga inayopatikana baada ya kupona gonjwa hilo.

Kila gonjwa, huwa linapewa asilimia zake za kufikia kutokana na jinsi ambavyo lina kasi katika maambukizi, mfano ugonjwa huu wa covid-19, wataalam wanasema kutokana na kasi yake ya maambukizi, basi ni lazima asilimia 70 ya wananchi wote wapate corona ndipo tunaweza kusema Tanzania tuna kinga kupitia “herd immunity”. Hapo ikiwa ina maana asilimia 30 iliyobakia inaweza kulindwa mfano wazee, wenye magonjwa sugu nk. Lakini kwasababu tuna vijana asilimia 90, basi ina maana hatutapata shida hata kidogo kuzipata hizo asilimia 70 zinazohitajika na WHO.



Kwasababu vijana hawaathiriwi sana na corona, ina maana tuna faida inapokuja kwenye “herd immunity”, ama huu mfumo unaotumika sasa nchini kwasababu kama tuna vijana asilimia 90, hatuwezi kukosa asilimia 70 za kutuwezesha kupata herd immunity na kuishinda corona.

Lakini hata hivyo data ni muhimu kufahamu tulipofikia. Pengine viongozi wameliona hilo kwasababu wao ndo wenye kuziona data, na ndiyo maana wanakuwa optimistic na kutangaza kuwa tumeishinda corona.

hata hivyo, pia ukifuatilia kauli zao na matendo, ni kama vile wanataka wananchi wengi kadri iwezekanvyo, waupate ili tufikie ile asilimia 70 inayotakiwa.

To be continued...

Tanzania Population 2020 (Demographics, Maps, Graphs)

Nguruvi3 Kalamu1 JokaKuu Daudi Mchambuzi
 
Mada hii sikuiona ila ulijenga hoja nzuri sana tangu nione hoja zako humu.!
The age-related death risk probably reflects the strength, or weakness, of the respiratory system. About half of the 109 Covid-19 patients (ages 22 to 94) treated at Central Hospital of Wuhan, researchers there reported, developed acute respiratory distress syndrome (ARDS), in which fluid builds up in the small air sacs of the lungs. That restricts how much air the lungs can take in, reducing the oxygen supply to vital organs, sometimes fatally; half of the ARDS patients died, compared to 9% of patients who did not develop the syndrome.

The ARDS patients had an average age of 61, compared to an average age of 49 for those who did not develop ARDS. Elderly patients “were more likely to develop ARDS,” the researchers wrote, suggesting how age can make Covid-19 more severe and even fatal: age increases the risk that the respiratory system will basically shut down under viral assault.

Who is getting sick? A look at coronavirus risk by age, gender, and more

Detective J Mag3 Kalamu1
 
Nchi zinazotangaza zimepata mabadiliko gani katika kupunguza au kuongezeka maambukizi. Nadhani mkakti sahihi ni wa rasimali nyingi kutumika katika kudhibiti maambukizi na si kuyashangilia.
Kwa maoni yangu, nadhani kutoa taarifa ni vizuri zaidi kuliko kuacha kama sasa hivi. Data ni muhimu kabla ya maamuzi.

Kama ni kweli kuwa tatizo la mashine lilipatiwa ufumbuzi, ilitakiwa tuendelee na kutoa taarifa. Kwasababu hata mimi imani yangu ilikuwepo sana kwenye facts nilizoweka kwenye bandiko la kwanza.
 
Ni ukweli kabisa kwamba imefanya kasi sehemu mbali mbali dunia ambako kuna unafuu wa maambukizi. Nilichokuwa ninapinga ni suala lenyewe kuanza kutumika kisiasa kama wafanyavyo waamerica.
Je, siyo kweli kuwa "lockdown" kwenye iliyofanya kazi ilikuwa ni kwa muda mfupi tu? Km Kenya, Uganda na Rwanda ambako sasa maanbukizi yanaongezeka.

Watalaamu wa afya wanasema, kwa uhakika, kutokana na tafiti, kuwa kuambukizana kunaongeza kingamwili "herd immunity" hasa kwa virusi. Yawezekana, kwa sababu hiyo, wanaojifungia ndani hupoteza uwezo huo.
 
Je, siyo kweli kuwa "lockdown" kwenye iliyofanya kazi ilikuwa ni kwa muda mfupi tu? Km Kenya, Uganda na Rwanda ambako sasa maanbukizi yanaongezeka.

Watalaamu wa afya wanasema, kwa uhakika, kutokana na tafiti, kuwa kuambukizana kunaongeza kingamwili "herd immunity" hasa kwa virusi. Yawezekana, kwa sababu hiyo, wanaojifungia ndani hupoteza uwezo huo.
Sidhani. Mbona marekani ni tofauti?
 
Back
Top Bottom