andate
JF-Expert Member
- Jun 9, 2011
- 2,651
- 1,029
Kila mwanamke ana aina ya wanaume anaovutiwa nao kwa haraka, na mara nyingi hu-deal na aina hiyohiyo ya wanaume hatoki nje ya hapo.ni kweli. Ila sometimes men are couser of this.
It hard to know a good man. Damn
Kuna wanawake wanaovutiwa na mabitozi, wengine wanavutiwa na matapeli, wengine na wanaume wanaojiheshimu, n.k.
Kuna mdada mtaani kwetu watu walikuwa wanasema ni nuksi, ukitembea nae utafungwa jela kwa sababu bwana zake wote anaowapata wanaishia kufungwa jela. Katika upelelezi wangu nikakuta kwamba yule dada huwa anavutiwa sana na wanaume wezi, huwaga hakubali wanaume wengine isipokuwa wezi. Cha ajabu ni kwamba huyo mdada anakuwa hajui kama hao wanaume ni wezi lakini automatically huwa anakubali wezi na kuwakimbiza wengine. Mimi nadhani kuna nguvu fulani iliyofichika ndani ya mwanamke ambayo ndio inamsukuma kupenda watu wa aina fulani.
Hapa nadhani inategemea moyo wako umeumbiwa wanaume wa aina gani, kama umeumbiwa mabitozi ma-player, matapeli, utaishia kubanjuliwa na kukimbiwa, kwa sababu utaachana na tapeli huyu na utahamia kwa tapeli mwingine kwa sababu unapenda matapeli.
Naongea kwa experience nimeshuhudia 100% ya wanawake walioangukia kwa wanaume wanaojiheshimu wote wameolewa na wana ndoa zenye furaha.
