WomanOfSubstance
Platinum Member
- May 30, 2008
- 5,457
- 975
"Dunia ya sasa siyo ile ya enzi za Mwalimu,
Dunia ya sasa hapendwi mtu bali kitu,
Dunia ya sasa penzi la kweli ni adimu,"
.................
Kuna dhana ya jumla kuwa wanaume na wanawake wote ni matapeli wa mapenzi.
Nani zaidi?
Hili ni swali gumu sana kujibu maana kila mtu ana agenda yake kichwani kwa wakati ule.Malalamiko kwa akina kaka ni kuwa wanawake wamezidi kutaka vitu badala ya kutoa penzi la kweli.Binafsi nadhani wapo wanawake wengi tu wenye kuwa na mapenzi ya kweli endapo wewe mwanaume utakuwa na mwanzo mzuri katika safari yako ya kutafuta mpenzi wa kweli.Hebu twende hatua kwa hatua.
1. Ni mara ngapi mkaka umeanza kwa kumtamani mwanamke kwa muonekano wa nje yaani alivyojipodoa na kujiupara, katilia viwalo vya bei mbaya, umemuona yuko bomba kimavazi, anajishebedua maana anajiamini.
2.Ni mara ngapi unachukua muda kujiuliza, huyu binti, tena mwanafunzi wa mwaka wa kwanza chuo, aliyetoka familia ya kawaida au ya kimaskini anaweza vipi kujimudu kwa maisha ya hali ya juu - anamiliki simu Blackberry na iko hewani muda wote , amesuka nywele za lakini tano, amevaa nguo za bei mbaya from Mwasu Fashion au Mariedo....( hesabu ya harakaharaka kwenye mavazi ya siku hiyo, viatu, handbag na accessories havipungui milioni!)
Je umewahi kujiuliza huyu mdada, karani wa kawaida mwenye kuendesha "Kompressor" ya bei mbaya, mwenye kuishi kwenye "golf course appartments" kodi dollar 1000 kwa mwezi , mwenye kwenda club mara tatu kwa wiki,anatoa wapi uchache wa kumudu maisha yake ya hali ya juu.
3. Unapomtokea mdada kama huyu, ukaona anakukubali wewe usiye na kitu au hata unacho uwe mpenzi wake, ulishajiuliza kama kweli anakupenda wewe au anapenda kitu fulani kutoka kwako?
4. Mdada anaweza kufurahia mazungumzo na wewe au kampani yako tu na siyo kuwa wapenzi na wewe.Je, ni mara ngapi umeweza kujua mipaka ya uhusiano wenu? Wapo akina dada wengi hupendelea marafiki wa kiume - urafiki wa kawaida na siyo upenzi.Je wewe unaweza kutofautisha/kupambanua hili?
5.Wewe bwana kaka unamfuata mwanamke au msichana mwenye nusu ya umri wako, ulishajiuliza huyu dada anaacha wa umri wake na kukupenda wewe.... is it genuine love or? Exceptions hazikosekani. Najua kuna wenye penzi la kweli na hili tutalijadili baadae lakini katika hali ya kawaida hii ikoje?
Kaka zangu wote hapa JF kuanzia akina Gudboy na wengineo mnaolalamika kuwa mnadanganywa na wapenzi wenu, tuanzie hapa kwanza ndipo tuelezane wapi wanapatikana wadada wenye mapenzi ya kweli.
Fidel najua una mkakati wa 2012... haya maswali muhimu ulishayafikiria?