Zion Daughter
JF-Expert Member
- Jul 9, 2009
- 8,921
- 4,235
Sidhani kama kuna mapenzi ya kweli kwenye zama hizi. Sijui watu wote humu wako pande gani za dunia lakini huku niliko mimi hii dhana ya mapenzi ya kweli inazidi kudhihirika jinsi ilivyo potofu.
Mambo ninayoyashuhudia makazini-maofisini na kwenye ma warehouse kwa wabeba maboksi yanazidi kuniaminisha kuwa hakuna kitu kinachoitwa mapenzi ya kweli. Labda sielewi kwa ujumla dhana nzima ya mapenzi ya kweli ni nini lakini kwa kile kidogo ninachokielewa hakuna mapenzi ya kweli.
Jaribuni kupitia hapa www.ashleymadison.com. Mwenye muda anaweza kujiandikisha tu kwa ajili ya kautafiti kadogo na aone jinsi watu walivyo wahakikishiwapo faragha yao.
Huku kwetu Bongo angalau bado yapo,mimi nakuhakikishia.Labda huko dunia ya kwanza.Kila kitu mnakuwa wa kwanza