Zion Daughter
JF-Expert Member
- Jul 9, 2009
- 8,921
- 4,236
ZD
Kama alivyosema NN, ukiangalia maisha katika uhalisia wake - weka kando misaafu (maana kuna wengine hawaijui) - utagundua tunajichosha kwa kuishi maisha yakufikirika. Uzoefu wangu ni kuwa unapojaribu kuishi 'mapenzi ya kweli', utakwaa kisiki maana hayana definition. Mfano utakutana na mwanamke/mwanaume anakuheshimu kuliko wazazi wake, hayo ndio mapenzi ya kweli? Unakutana na binti/mkaka ni mkarimu kupita kiasi hayo ndio mapenzi ya kweli? Haya utakutana na mwongo/mnafiki utasema hana mapenzi ya kweli? Hapo kuna dhana mbili tu, kuwa na/au kukosa utu na ubinadamu. Wizi, uongo, majivuno, dharau, ukatili ni kukosa utu na ubinadamu na wala si kukosa mapenzi ya kweli
Bado msimamo wangu upo palepale kuwa mapenzi ya kweli yapo! na mapenzi ya kweli ni mkusanyiko wa vitu vingi sio heshima tu na ni lazima yawe Natural.Usichanganye madhaifu ya mtu na recipes za mapenzi ya kweli.unapoanza kuangalia suala la mapenzi lazima ulitafakari hili neno UPENDO.upendo ni neno lenye mkusanyiko wa vitu vingi sana.Na nakwambia kweli yupo somewhere mtu wako anayekufaa mwenye mapenzi ya dhati kwako ila hujafanya bidii ya kumtafuta.Na unaweza usimuone kirahisi hata ukikutana nae kwa sababu you are blind tayari-yani huamini kama anaweza kuwa na mapenzi ya kweli.