Kama mtu wa kufanya research ndogondogo hii hali inatisha kwakwel sio kawaida ya watanzania kabsa toka nizaliwe watanzania wao ni mpira na ngono tu lakini hali kwasasa ni tofaut Kwenye mitandao yote sio jamii forum tu
Kote hali tete, mada za kiwaki zote hazna wachangiaji kabsa
Kweli watu hubadilika sikutegemei hili kabsa kwa kizaz hichi cha mchicha mwiba
Lucha Lucas Mwashambwa gallow bird stakehigh Ritz na wengine mchelemchele
Hadi haszu nasikia alikua Frontline October 29
Alisema Kabudi kwamba siku moja Watanganyika wakija kubalidilika watakua watu wabaya sana , na aliweka msisitizo kwamba bora Wazanzibar mambo yote kwao yako mezani ila watanganyika wameyashikilia Moyoni , je maneno yake yanaweza bagazwa tena hata kama alienda kuonja dawa corona Madagasca wakati amelamba ASALI ya mwendazake ,ila kama taifa tunayaona, very soon Taifa linaelekea kwenye civil war kama kibuli cha hawa waliopora uchaguzi kwa jeuri ya pesa na kile wao husema mtandao wao ni mkubwa.
Umeona wapi kiburi/ jeuri ikashinda wenye nchi ? ambao ni wananchi?
Leo zipo propaganda ati za watu kulipwa , hivi tupo na akili kweli, mie vijana wangu wameuwawa, na hawakua kwenye maandamano je walilipwa na nani iyo pesa ya madafu inayosemwa , wanangu walijua sipo na kipato kikubwa kama mafisadi wengine ila kile Mungu amenijalia tulipatiana Mgao sawa ,leo uniulie wanangu then uje na propaganda za kipuuzi kabisa .
Haya mambo yanachukuliwa kitoto sana ,wakati watu nyoyo zetu zinavuja Damu.
Alafu mnateuana huku sie nyoyo yetu inavuja Damu , leo mtoto wa Mwigulu tena mdogo tu , why hawe na maisha makubwa kuliko ndugu zetu ambao hata makazi ya kuishi hawana achana na kukosa mlo wa siku, kisa baba yake alikua uvccm na kuratibu mambo ya ajabu huko Arusha, akwawa waziri ya Mambo ya ndani, akawa waziri wa fedha ,then teuliwa katika serikali batili ati kuwa Waziri mkuu, zipo tuhuma za kuchapisha fedha mbona hajalijibu kifasaha mpaka sasa ?
Atwambie alisikika akishukuru kuwa na noti za fedha ambazo zipo na saini yake ,atwambie tangu iyo imekuepo zimeingia noti ngapi katika Mzunguko wa fedha za nchi kwanza na kwa nini wasemao zipo fedha zilichapishwa ,asije na majibu yasiotia shaka ?
Kama tumeamua Taifa uhawa kwa mambo ya kipumbavu acha life ,wajukuu , wajao wenye akili watalijenga upya .
Utakua ni unafiki kuchukia mtu yoyote pata cheo ,swala hicho cheo unakipata katika mazingira gani ,kwa sababu zipi , kwa nyakati zipi, haiwezekani ,katika mazingira kama haya.