Kweli Siasa za CCM Mpya ya Magufuli si mchezo!

Kweli Siasa za CCM Mpya ya Magufuli si mchezo!

Siasa za CCM Mpya ya Magufuli si mchezo !

Leo Comrade Mwigulu Lameck Nchemba amenywea na kupotea kabisa!

Kiburi ,kujikweza na kuvaa maskafu ya Bendera ya Taifa hadi chooni kwisha kabisa!

Timu yake ya Singida United inatupiwa virago nje na NHC na kupigwa mnada kwa kushindwa kulipa Tshs.3 Milioni !

Mwenye Timu ( Mwigulu Lameck Nchemba ) anapigiwa simu hapokei na anajificha!

"Vijana" wake waliokuwa na majivuno kama Festo Sanga wanakuwa wadogo kama kidonge cha Pilitoni!

Comrade January Makamba anapotea kwenye ulingo wa siasa za CCM na ndoto zake za Urais zimeyeyuka kama barafu juani anabaki kuiga mitoko,pozi na mavazi ya Barack Obama na kupiga tu picha kwenye locations alizopita Obama naye aonekane visionary!

Ubunge wa Bumbuli tena hautamani kwani mbele anaona giza tu!

Comrade Nape Nnauye kiburi kile cha kupita juu ya viuno vya akina Mama kule jimboni Mtama kwisha kabisa!

Anapigishwa kwata kuingia Ikulu kutokea getini huku akifuta jasho na kugeuka geuka nyuma mithili ya Kibaka anayefukuzwa baada ya kukwapua sidiria au chupi pale Manzese Darajani!

Ma- Guru wa siasa za CCM Mzee Abdulrahaman Kinana, Mzee Yusuph Makamba na Kachero Mbobezi Bernard Kamillius Membe wakiitwa kwa dharau kuhojiwa na akina Humphrey Polepole!

Hayo yote yakiwatokea Ma- comrades wangu hawa ! ;

Comrade Paul Makonda mambo yake yako mstari kiasi kwamba ni Mkuu wa Mkoa tu wa DSM lakini anaogopeka na ana nguvu kuliko hata Waziri Mkuu wa JMT.

Mwanaharakati Cyprian Nyamagambire Musiba ana nguvu kiasi ambacho vyombo vya dola havina budi kufanyia kazi maelekezo yake! akikusonta Musiba kuwa unampinga Rais Magufuli jua umekwisha!

Omba Mungu watu wasiojulikana wakikufuata mipango yao itibuke ama sivyo historia yako itakuwa kama ya Ben Saanane au Azory Gwanda! You will be silenced forever !

Mwita Mwikwabe Waitara aliyekuwa akibeza CCM majukwaani 2015 leo ana nguvu ndani ya Serikali ya CCM na anapowajibu Wapinzani Bungeni na kumtetea Rais Magufuli anafanya hivyo kwa nyodo huku akicheua kichuri kilichochanganyika na pombe ambayo harufu yake inaweza kukatwa tu na dawa zinazodungwa kuhifadhia maiti mochwari!

KWELI CCM MPYA CHINI YA MAGUFULI NI KIBOKO!
Aaaaiiiiseeee! Na kwenye cm wanaogopa kuongea watadukuliwa
 
Ji
Mwigulu alitengeneza makundi ya Vijana ya I'll yateke na kutesa wapinzani ...Iramba amejenga chuki miongoni mwa Vijana,Leo hii amechoka ndembendembe ,hoi poloi ...Shetani Hana Rafiki'
Jinga Sana yule
 
Kama wangekuwa wengi hivyo usemavyo tungeona uwanja sawa wa ushindani. Lakini kwakuwa ni wachache wenye uwezo inabidi kuwe na matumizi makubwa ya vyombo vya dola ili kuwabeba wenye uwezo duni.
Huu ni mtazamo tu
 
Kama ni wengi si tungeona ya marekani kwa trump yakifanywa na bunge LA hapa,au tungeona busara yao kwenye bunge LA katiba
Kumbukumbu Marekani sio tz, wana misingi Bora na mikubwa juu ya utawala wao
 
Huu ni mtazamo tu

Huu si mtazamo bali ndio ukweli. Najua sio jambo linalowafurahisha wanaccm wote kuonekana kama chama kinachotegemea mabavu ya dola kufanya siasa, lakini wanaccm msiotaka hali hiyo sio wenye maamuzi ya hayo, bali wenye maamuzi wa matumizi ya vyombo vya dola kuibeba ccm hiyo ndio tabia yao ya asili. Kwakuwa mnafaidika na tabia hiyo, mnaingiwa upofu wa kuuona ukweli huo.
 
kuna watu wakipata vimadaraka wanatuona wengine kenge tu, ukimshauri anaona kama makelele ya mbu.
na muda mwingine hata ukimsogelea tu, hujasema kitu anaingiza mkono mfukoni anakurushia 20k[emoji23][emoji23] yani hataki usumbufu na wewe.

Hasara Umfika Mwenye Mabezo
 
Mimi naisubiria tu ile Ccm itakayozaliwa baada ya Rais Magufuli kumaliza muda wake wa kukaa madarakani. Hapo ndipo tutakaposhudia unafiki wa makada kwa kuanza kumsimanga Rais "Mstaafu" ya kwamba alikuwa na madhaifu mengi! na huku wakimpamba Rais wetu wa wakati huo His Excellency Pascal Mayalla.
pascali mayalla atakuwa magu part two
 
mtu kama january acha aisome namba, maana ali-facilitate kwa nafasi kubwa kuanzishwa kwa sheria ya cybercrime.

hii sheria imewaponza vijana wengi sana na inaendelea kufanya hivyo kila iitwapo leo.

naona siku hizi amegeuka motivational speaker kule twitter, anatweet sana kuhusu masuala mbalimbali ya kijamii. anatafuta huruma fulani ya kijamii(public sympathy)

tutaelewana tu kidogo kidogo, ngoja tuonyeshane makali(kwa sauti ya dr. shika)


kapotelea wapi huyu daktari jeuri na mwenye akili nyingi
 
Siasa za CCM Mpya ya Magufuli si mchezo !

KWELI CCM MPYA CHINI YA MAGUFULI NI KIBOKO!
Naunga mkono hoja

P
 
Kwa kifupi ni kuwa hadithi hii inatufundisha kuwa unapokuwa na madaraka usijione ndo mwisho wa dunia hata wanaotamba leo subiri huko mbeleni watakiona cha moto tuu, nawashangaa wabunge wa ccm wanapishindwa kuweka mambo sawa wakati wanayo nafasi badala yake wanakalia ushabiki tuu wakidhani wataongoza hilo bunge milele, nani alidhani Yusuph Makamba na Kinana wataitwa kuhojiwa? bilashaka hayupo! Wewe ungewaza hivo ungepigwa shaba.
Utamu wa madaraka huwa unapofusha usione ya mbeleni ndio maana hata wenye madaraka leo wameppfishwa wanadhani nguvu waliyonayo itadumu milele hadi vizazi vyao vya nne

Hivi kuna mtu alowah kuwa na nguvu nchi hii kama Nyerere? leo hata watoto wake hawapo kweny mfumo

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Siasa za CCM Mpya ya Magufuli si mchezo !

Leo Comrade Mwigulu Lameck Nchemba amenywea na kupotea kabisa!

Kiburi ,kujikweza na kuvaa maskafu ya Bendera ya Taifa hadi chooni kwisha kabisa!

Timu yake ya Singida United inatupiwa virago nje na NHC na kupigwa mnada kwa kushindwa kulipa Tshs.3 Milioni !

Mwenye Timu ( Mwigulu Lameck Nchemba ) anapigiwa simu hapokei na anajificha!

"Vijana" wake waliokuwa na majivuno kama Festo Sanga wanakuwa wadogo kama kidonge cha Pilitoni!

Comrade January Makamba anapotea kwenye ulingo wa siasa za CCM na ndoto zake za Urais zimeyeyuka kama barafu juani anabaki kuiga mitoko,pozi na mavazi ya Barack Obama na kupiga tu picha kwenye locations alizopita Obama naye aonekane visionary!

Ubunge wa Bumbuli tena hautamani kwani mbele anaona giza tu!

Comrade Nape Nnauye kiburi kile cha kupita juu ya viuno vya akina Mama kule jimboni Mtama kwisha kabisa!

Anapigishwa kwata kuingia Ikulu kutokea getini huku akifuta jasho na kugeuka geuka nyuma mithili ya Kibaka anayefukuzwa baada ya kukwapua sidiria au chupi pale Manzese Darajani!

Ma- Guru wa siasa za CCM Mzee Abdulrahaman Kinana, Mzee Yusuph Makamba na Kachero Mbobezi Bernard Kamillius Membe wakiitwa kwa dharau kuhojiwa na akina Humphrey Polepole!

Hayo yote yakiwatokea Ma- comrades wangu hawa ! ;

Comrade Paul Makonda mambo yake yako mstari kiasi kwamba ni Mkuu wa Mkoa tu wa DSM lakini anaogopeka na ana nguvu kuliko hata Waziri Mkuu wa JMT.

Mwanaharakati Cyprian Nyamagambire Musiba ana nguvu kiasi ambacho vyombo vya dola havina budi kufanyia kazi maelekezo yake! akikusonta Musiba kuwa unampinga Rais Magufuli jua umekwisha!

Omba Mungu watu wasiojulikana wakikufuata mipango yao itibuke ama sivyo historia yako itakuwa kama ya Ben Saanane au Azory Gwanda! You will be silenced forever !

Mwita Mwikwabe Waitara aliyekuwa akibeza CCM majukwaani 2015 leo ana nguvu ndani ya Serikali ya CCM na anapowajibu Wapinzani Bungeni na kumtetea Rais Magufuli anafanya hivyo kwa nyodo huku akicheua kichuri kilichochanganyika na pombe ambayo harufu yake inaweza kukatwa tu na dawa zinazodungwa kuhifadhia maiti mochwari!

KWELI CCM MPYA CHINI YA MAGUFULI NI KIBOKO!
Hapo mwisho


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hekima ni kwa mtu mwenye hofu ya Mungu na mwenye kujua kwamba hatima ya mwanadamu ni kaburi.
 
Back
Top Bottom