Kweli kuna wanawake wanaroho mbaya

Mpango wa MUNGU ulikuwa ni tujazane wanaume tu humu duniani? Aisee bora alibadili mawazo. ASANTE MUNGU.
 
Mkuu aliekuambia uwaseme vibaya mama zetu,dada,shangazi,wake zetu ni nani..?
Hivi ulishaona alshabab wakike hata kumi..?
Wezi je mitaani..?
Wanaobaka watoto je..?

Hawa viumbe mi nawatetea wana huruma,wastahimilivu,they care n.k
Karibu pm nikupe zawadi yako mkuu
 
Mwanamke ni binadamu wa kwanza kuonana na shetani ana kwa ana. Kuna mambo mengi Eva aliongea na shetani ambayo wanaune hatuyajui. Tujipange namna ya kuishi nao.
 
Mkuu hivi unafikiri siku ya hukumu Mungu ataangalia source na siyo impact?

Jiulize kwanini baada ya Adam na Evah kula tunda wote walipewa adhabu na siyo Evah peke yake ambaye ndiye aliyesababisha Adam ale tunda?

Ulichofanya hapa ni kuitupia lawama jinsia ya kike kama ambavyo Adam alimtupia lawama Evah!

Pale alipoulizwa na Mungu kwanini amekula tunda akajibu eti ni huyu mwanamke uliyenipa ndiye aliyenishawishi akidhani kwamba Mungu angempa adhabu Evah peke yake lakini sote tunajua aliwapa adhabu wote wawili!

Evah aliambiwa atazaa kwa uchungu na Adam aliambiwa atakula kwa jasho lake!

Ingekuwa hivyo basi kusingekuwa na hukumu siku ya mwisho kwa sababu chanzo cha dhambi ni shetani hivyo angehukumiwa peke yake lakini jiulize kwanini hataenda kuhukumiwa peke yake bali wenye dhambi wote (hata kama yeye ndiye aliyewashawishi) nao wataenda kuhukumiwa naye?

Ni kwa sababu Mungu amempa kila mwanadamu (mwanaume na mwanamke) nguvu na uwezo wa kumshinda shetani na kuishinda dhambi kupitia Mungu mwenyewe!

Vivyo hivyo wanaume mna uwezo wa kuvishinda vishawishi vyote vya wanawake na wala hakuna kisingizio chochote chini ya jua kinachowafanya mshindwe kuzishinda dhambi zinazowakabili!

Hivyo endeleeni kudanganyana huku duniani na kuwatupia lawama wanawake tu (kwa sababu ni nature yenu wanaume kutupa lawama kwa wanawake kwenye kila kitu kumbuka ilianzia kwa Adam)!

Lakini kaa ukijua siku ya hukumu kila mtu atahukumiwa kulingana na imani yake na matendo yake hakutakuwa na kutupiana lawama tena eti sijui nani alinisababisha nitende dhambi kwa sababu hata shetani mwenyewe hautaruhusiwa kumtupia lawama sembuse mwanamke!

Kwanini ni kwa sababu Mungu alimruhusu shetani aje kututia majaribuni lakini pia akatupa uwezo wa kumshinda huyo huyo shetani!

Kilichobaki wewe tubu umrudie Mungu wako mkuu kutupa lawama kwa jinsia fulani hakutakusaidia chochote kwa sababu ukishakufa utahukumiwa wewe kama wewe hakuna mtu atakayebebeshwa mzigo wako wa dhambi utaubeba wewe kama wewe!

Wewe ukibaka na usipotubu lazima ukahukumiwe kwa kubaka na hata ukiua na usipotubu lazima ukahukumiwe kwa kuua

Maandiko yako wazi na sheria ziko wazi Mungu alishaviweka tuache kujifanya tunang'ang'ania kurejea maisha ya Adam na Evah kana kwamba tulikuwepo wakati wanatenda hizo dhambi!
 
Mkuu aliekuambia uwaseme vibaya mama zetu,dada,shangazi,wake zetu ni nani..?
Hivi ulishaona alshabab wakike hata kumi..?
Wezi je mitaani..?
Wanaobaka watoto je..?

Hawa viumbe mi nawatetea wana huruma,wastahimilivu,they care n.k
hiyo ni asili... usipingane na asili KENZY
Mungu kakupa tahadhali uishi na hao dada, mama, shangazi na mke wako kwa akili nyingi
 
Leo kwenye daladala wanawake wamegoma kumpisha seat mwanamke mwenzao mwenye mtoto cha ajabu zaidi Mtoto anasumbua ndio kwanza wanakaza macho kuangalia nje.... Sijawahi ona mwanamke anampisha mwanamke mwenzie seat. Mostly wanaume ndio tuna huo upendo.
 
hiyo ni asili... usipingane na asili KENZY
Mungu kakupa tahadhali uishi na hao dada, mama, shangazi na mke wako kwa akili nyingi
Achana na maswala ya kupelekwa Kama kondoo ndugu nawe unaubongo fikiri wanawake nao ni binadamu Kama sisi me.. hakuna cha kusema sijui vile au hivi hizo historia zisikutishe we jaribu kuangalia kosa source yake Kama ni dhambi alianza kuasi shetani na si mwanamke lkn Yule aliemtengeneza huyo shetani akaamua amtupe shetani duniani ambapo ameweka viumbe anaowapenda na kawaumba kwa mfano wake!.. shetani akafanikiwa kumshawishi mwanamke na hatimae mwanaume! Hivi ukifikiri kiundani Kama kweli unakichwa kizuri cha kufikiri utagundua mwanzo wa yote ndie mwanzo wa kila kitu ndugu! Hakuna tabia yoyote kiumbe kinarithi kutoka mahali pasipofahamika isipokuwa kiumbe kinarithi tabia kutoka katika source yake.. pasipo kumung'unya maneno Mungu ndio chanzo cha wema na ubaya! Kama yeye ni mwema tu basi Kuna sifa inapungua kubwa sana ya uweza na utambuzi wa kila kitu na hapo yeye atakuwa si chanzo cha kila kitu maana ukiutenga ubaya hivyo tutasema ubaya hajui ulipotoka hivyo sifa ya ujuzi wa kila kitu na mwanzo wa kila kitu inamvuka!

Shetani tabia ya ubaya alirithi wapi Kama sio chembechembe za sifa toka kwa aliemuumba..? Au unafikiri tabia ya dhambi aliipataje Kama alipoumbwa hakuwa na sifa hiyo..?
Hakuna cha shetani Wala mwanamke mlaumiwa wa kwanza ni source mwenyewe maana hakuna kinachofanyika bila ithibati yake.. ukitumia upeo wa mavimavi hutaelewa nilichoandika..
 
Tafuta helaaaaa !!!!!! Wanawake ni paradise ndogo ntakuja kuelezea baadae lkn tafuta helaaaaa kwanza bila iooooo hawa viumbe ni nyokaaaaa kabisaaaa na ana sumu kali
Acha ushamba wewe usifikiri watu wote wanaandila thead humu hawana pesa.
 
Mkuu aliekuambia uwaseme vibaya mama zetu,dada,shangazi,wake zetu ni nani..?
Hivi ulishaona alshabab wakike hata kumi..?
Wezi je mitaani..?
Wanaobaka watoto je..?

Hawa viumbe mi nawatetea wana huruma,wastahimilivu,they care n.k
Bado hujawaelewa vizuri, subiri muda ukifika utautafuta huu uzi.

Sio kila binadamu aweza kuwa Shabaab au mbakaji. Yeye pia ana anga zake ukijichanganya anakutenda. Rejea uzi tena itaelewa
 
Bado hujawaelewa vizuri, subiri muda ukifika utautafuta huu uzi.

Sio kila binadamu aweza kuwa Shabaab au mbakaji. Yeye pia ana anga zake ukijichanganya anakutenda. Rejea uzi tena itaelewa
Yote kheri mkuu..
 
inategemana na malezi yake, sio wote wenye roho mbaya lkn ukikutana na ambaye hana malezi ya kiroho utajuta na utashangaa atakayo kufanyia, hivyo ni muhimu tuwahimize Dada zetu, wake zetu, watoto wetu, shangazi zetu na wadogo zetu kupata mafundisho ya kiroho Makanisani au Madrasa/msikitini. Mwanamke mwema na mwenye huruma ni yule aliye pata mafundisho barabara ya IMANI yake vivo hivyo kwa mwana Mume . kinyume cha hapo wote ni mashetani
 
We ungeandika thread yako ueleze hayo unayoyataka,mimi nina sababu zangu za kuandika hivi.. kwa hiyo ubongo wako ndio mdogo kabisa kama panzi.
 
Mkuu aliekuambia uwaseme vibaya mama zetu,dada,shangazi,wake zetu ni nani..?
Hivi ulishaona alshabab wakike hata kumi..?
Wezi je mitaani..?
Wanaobaka watoto je..?

Hawa viumbe mi nawatetea wana huruma,wastahimilivu,they care n.
Lait wangekuwa na nguvu hayo wangefanya tu km wanaweza kuuza miil yao hili ni dk tu
 
Dah !!! Hii stor ilitokea kenya iliniuma sn yaan wanawake ni washenz
 
Wanawake wana huruma sana,wavumilivu,wana upendo sana..mungu wabariki wanawake wote.
 

Mwanamke ni binadamu wa kwanza kuonana na shetani ana kwa ana. Kuna mambo mengi Eva aliongea na shetani ambayo wanaune hatuyajui. Tujipange namna ya kuishi nao.
🤔🤔
 
Mwanamke anapande zote umesahau upande wa mazuri,hawa wanawake ukikaa nao vizuri wamebeba hatima yako,muulize Yakobo bila mama yake baraka kwake ilikuwa ngumu kupata,waulize wanasiasa,mashehe na wachungaji watakwambia wamama wana play part gani kwenye maisha yao.

Sent using Jamii Forums mobile app
 



Wewe mlevi na mbinafsi kaa kimya.

Hakuna kitu unaweza sema kupindisha ukweli huu...

Mwanamke wa kiafrika ndiyo NGUZO ya jamii ambayo wewe jinga unaishi ndani yake.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…