muhomakilo jr
JF-Expert Member
- Jul 28, 2013
- 15,912
- 14,882
Aisee...mtu anakudai mchango mpaka kelo..
Wewe tumia akili kidogo. Wewe kama unauwezo unachangisha watu pesa za nini??. Mtoa mada kaweka wazi kabisa ya kwamba kama wewe unauwezo basi fanya hiyo shughuli kwa gharama yako mwenyewe. Watu hawataki michango, hii michango inachangia kwa kiasi kikubwa kutia watu umasikini, kisa ni ulimbukeni. Eti kuji enjoy, ji enjoy kwa pesa yako, acheni kuchangisha watu michango isiyokuwa na maana.
Mimi nina miaka mitatu sasa tangia nimeweka fulstop kwenye suala zima la kuchangia Harusi, kipaimara, sijui send off party etc.. Mtu akiniletea kadi namtaarifu kabisa kuwa mimi huwa nachangia Misiba, masuala ya ugonjwa na mambo kama hayo. Nachangia haya mambo kwakuwa ni mambo ambayo yanatokea bila taaria, na linaweza kukukuta wakati wowote.
Sasa nyie mmekaa mnafanya yenu siku zooote, mmepanga kuishi pamoja mnakuja kutukurupusha na michango, tena mnaweka na kima cha chini as if mnafahamu kipato changu. Halafu mtu huyo huyo anaenda hospitali kumuangalia mgonjwa anaenda mikono mitupu, au anapeleka Juice ya kijoti. This is nonsense
Unafaa kuwa Mwalimu au Doctor, mambers wote wa JF tungekuwa kama wewe basi JF ingekuwa na heshima sana asante kwa kunielimisha.
Unaua nzi na nyundo mkuu.
Bora umesema wenzako na wewe, waache wenye nazo wafanye wee unakereka nini? Ni siku haitajirudia kamwe wacha waenjoy to the fullest
ukweli mtupu ulichosema...mie huyo wa sasa kila siku kutext na kufanyiana countdown ya days as if tunazindua jengo nilisoma naye advance miaka 12 iliyopita...tumekutana tukabadilishana number...lol imekuwa tabu...mchango....mchango. ...mchango! !!Mwingine mawasiliano ni wakat huo ana shida ya kuoa tu,let say mlimaliza chuo 5yrs ago,hamkua mnawasiliana ila linapokuja suala la kuoa basi hapo sms na calls haziishi,akishaoa mawasiliano yanakufa tena,
ukweli mtupu ulichosema...mie huyo wa sasa kila siku kutext na kufanyiana countdown ya days as if tunazindua jengo nilisoma naye advance miaka 12 iliyopita...tumekutana tukabadilishana number...lol imekuwa tabu...mchango....mchango. ...mchango! !!
Kwaiyo kama mtu ana uwezo unataka asiji enjoy? Msio na uwezo jikuneni mkono unakofika
Dr. Wansegamila, bajeti yako kwa mwenye akili ataitumia kama dira. Mimi nilishawahi kulisemea hilo hata kwenye public sababu watu wamefikia sehemu wamekosa vipaumbele hata vya maisha yao wenyewe. Inafikia sehemu tunashindwa kusalimiana na watu huku mitaani kisa shughuli ya masaa ma3 iliyotazamiwa kufanyika kwa nguvu ya mifuko ya watu wengine.
Mara kadhaa utaona mtu (mathalan mfanyakazi mwenzako) aliyekosa aibu anakuletea kadi ya mchango, eti kakaake au pengine hata shemeji yake anaoa. Mimi huwa najiuliza maswali mengi sana hapa:
1. Kakaako hana rafiki zake?
2. Kuna umuhimu gani wa mtu usiyemjua kuhudhuria harusi yako?
3. Wingi wa watu kwenye sherehe yako ya ndoa una impact gani kwenye maisha yako yanayoanza baada ya hiyo siku?
Huu ni ulimbukeni. Kukosa aibu na kuiga mambo yasiyo na msingi ni shida sana. Leo hii imekuwa ni dhambi mtu kufanya sherehe nyumbani kwake, lazima yatumike mamilioni kukodi ukumbi.
Ashakhum si matusi, tuache UPUMBAVU. Kama tunaweza kupata MUDA wa kukaa VIKAO na kukusanya MILIONI 20 kwa ajili ya jambo ambalo lingeweza kufanywa na mhusika mwenyewe kama ambavyo tendo la ndoa atafanya peke yake, basi lets be productive. VIKAO vyetu viwe vya kukusanya milioni 60 tukanunue SHAMBA, TREKTA na MBEGU tupande MATIKITI MAJI. Ile kasi ya kuwapata watu 300 wa kuchanga na kuhudhuria harusi iwe kasi ya kila mmoja wetu kuwapata watu 100 wa kununua matikiti tutakayozalisha.
Upumbavu ni mzigo mzito sana
Mtu mwenye uwezo hatembezi kadi kama Marehemu Matonya, mtu mwenye uwezo hualika watu. Shida yako tumegusa UNAPOLALA sasa umeingia mshawasho wa kujibu hata ambacho hukuulizwa.
Kama mtu ana uwezo na ameona hiyo ni investment ya maana kwake acha afanye, lkn huu mchezo wenu wa kukosa haya kama mahayawani na kuanza kukera watu si mchezo wa maana. Maana mwaka fulani niliwahi kuletewa kadi ya mchango wa Kipaimara, hapo ndio utaahira wa mwanadamu ulidhihirika.
Kipaimara ni sherehe ya kiroho, tena inahusu watoto. Unaamka bila aibu umejaa ndevu uso mzima unaenda kuchapisha kadi ili wanaume wenzio wachange fedha ununue pombe kwa fahari ya shetani kwenye tukio la Kimungu, sio UPUMBAVU huo?
Pole sana, sijawah kupitisha bakuli kwenye harusi yangu, labda unanipa tafsiri ya ulichokifanya
Pole sana, sijawah kupitisha bakuli kwenye harusi yangu, labda unanipa tafsiri ya ulichokifanya
Kwaiyo kama mtu ana uwezo unataka asiji enjoy? Msio na uwezo jikuneni mkono unakofika