Kweli harusi sasa zinazidi kututia umasikini

Kweli harusi sasa zinazidi kututia umasikini

Ha ha ha , Hii kitu inakera sana mkuu. Unakuta mtu unarundo la kadi, kisa mtu anakufahamu tuu anakuletea kadi sijui ya mdogo wake na rafiki yake. Nakaa natamani sana kuiona Tanzania inaondokana na huu ugonjwa, huu ugonjwa unavunja urafiki, unavunja ushirikiano katika jamii kwenye mambo yaliyo ya msingi. Usipomchangia mtu kwenye harusi yake, eti hata kwenye msiba wako haji. Huu ni ugonjwa wa ajabu sana. Umejikita kwenye jamii tumekuwa kama Mateja, wanajisikitikia kula unga lakini hawathubutu kuacha kutumia unga. Ukifuatilia sana utagundua watu wanasikitikia sana hii michango lakini wanakosa ujasiri wa kusema sasa noo. Hembu tubadilike

Na ubaya zaidi watu wameshafanya ni haki yao kuchangiwa.

Usipomchangia mnakuwa maadui.
 
Huwa najiuliza mwisho wake lini Watanzania wa hali ya kati na chini kimaisha, hasa mijini, wataachana na ulimbukeni wa kufanya gharama kubwa za harusi?

Tukio ambalo linachukua mamilioni halafu linafanyika within few hrs watu wanakula wanakunywa wanaondoka, bajeti ya milioni 9 baada ya honey moon maharusi wanayaanza maisha kwa taabu kulipa madeni n.k., kwanini Watanzania hatubadiliki?

Wazungu miaka ya nyuma walishapita humu wakabadilika miaka mingi ilopita karne hii wakihudhuria harusi zetu wanatushangaa na kutuona ni matajiri sana kumbe hamna kitu!

Kweli hatukatai wapo wanaojiweza kifedha wacha wafanye, lakini wenzangu na miye unajikamua unafanya sherehe kubwa na mnaendelea katika circle ya kuchangiana the whole year unajikuta unachangia harusi tu, sijui kama kuna wanaopiga hesabu ya hizo kadi familia iliochanga kwa mwaka na si kana kwamba ina mwisho, no, na mwaka ujao hivyo hivyo.

Tuamke Watanzania, tufanye harusi za gharama ndogo, kama ni swala la kuchangishana basi tuchangishane ada-fees-watoto wakasome vyuoni Malaysia, London na US, matunda yatakuja onekana. Wakenya wenzetu waliliona hili mapema, leo wengi ni maboss ktk nchi yetu wenyewe!

Tubadilike Watanzania! Harusi nacho ni chanzo cha kutiana umasikini!

Mimi niliachana na mchumba wangu ambaye tayari nilikuwa nimemtolea mahali,alikuwa ananishinikiza tufanye harusi ya kifahari,nikaona ni upuuzi.
 
Usichangie kila mtu,chagua wachache
Au changia zawadi ya kikundi afu usiende baaas
 
Mchango
sare
usafiri
bla bla bla

hapana hapa kibaruani nimewaeleza waz sina hela wala salary slip hakuna mahal imendikwa mchango wa harusi kipaimara wala besdei hapa hata besdei kuna mchango mfyuuu sitaki kuskia na wameshaweka vichwan mwao wamenuelewa
 
Dr. Wansegamila, bajeti yako kwa mwenye akili ataitumia kama dira. Mimi nilishawahi kulisemea hilo hata kwenye public sababu watu wamefikia sehemu wamekosa vipaumbele hata vya maisha yao wenyewe. Inafikia sehemu tunashindwa kusalimiana na watu huku mitaani kisa shughuli ya masaa ma3 iliyotazamiwa kufanyika kwa nguvu ya mifuko ya watu wengine.

Mara kadhaa utaona mtu (mathalan mfanyakazi mwenzako) aliyekosa aibu anakuletea kadi ya mchango, eti kakaake au pengine hata shemeji yake anaoa. Mimi huwa najiuliza maswali mengi sana hapa:
1. Kakaako hana rafiki zake?
2. Kuna umuhimu gani wa mtu usiyemjua kuhudhuria harusi yako?
3. Wingi wa watu kwenye sherehe yako ya ndoa una impact gani kwenye maisha yako yanayoanza baada ya hiyo siku?

Huu ni ulimbukeni. Kukosa aibu na kuiga mambo yasiyo na msingi ni shida sana. Leo hii imekuwa ni dhambi mtu kufanya sherehe nyumbani kwake, lazima yatumike mamilioni kukodi ukumbi.

Ashakhum si matusi, tuache UPUMBAVU. Kama tunaweza kupata MUDA wa kukaa VIKAO na kukusanya MILIONI 20 kwa ajili ya jambo ambalo lingeweza kufanywa na mhusika mwenyewe kama ambavyo tendo la ndoa atafanya peke yake, basi lets be productive. VIKAO vyetu viwe vya kukusanya milioni 60 tukanunue SHAMBA, TREKTA na MBEGU tupande MATIKITI MAJI. Ile kasi ya kuwapata watu 300 wa kuchanga na kuhudhuria harusi iwe kasi ya kila mmoja wetu kuwapata watu 100 wa kununua matikiti tutakayozalisha.

Upumbavu ni mzigo mzito sana
Kbd says thank you for this useful post
 
Last edited by a moderator:
Harusi 11 hela wanakutafutia wao?

Nikichangia ujueni ya ndugu wa karibu au rafiki wa dhati...... (tena inategemea hali ya kifedha na mipango yangu)

Otherwise wacha wanune tu

Kuna wengine wanadai ( hawaombi tena, wanadai)utadhani waliweka...

Mkuu, mm nimeamua suspend line yangu ya Tigo mpaka January Mwakani, maana ilikuwa balaa! Mwezi huu wa 11/2015 nina harusi 18 za kuchangia, nafanyeje hapo! Solution nikaona ni ku-ban line kwa muda, sasa hivi napumua maana sipati msg wa calls za kukumbushwa kuchanga...
 
Mada hii nzuri sana maana nimesumbuliwa michango utafikiri tutachangia wakati wa tendo!
 
Mimi hapa nilpo nina kadi sita na nne kati ya hizo zina kiwango(single elf 30,double 50).
Hadi sendoff kadi jamani?
Aisee, saa nyingine hata kuzikataa unashindwa maana unazikuta mezani ofisini au nyumbani!
 
Nimelaumiwa sana mpaka WAMECHOKA.......narudia tena sichangii jitu harusi tusisumbuane
 
Bora umesema wenzako na wewe, waache wenye nazo wafanye wee unakereka nini? Ni siku haitajirudia kamwe wacha waenjoy to the fullest

Wafanye kwa hela zao, si kwa michango ya kulaximisha
 
Huwa najiuliza mwisho wake lini Watanzania wa hali ya kati na chini kimaisha, hasa mijini, wataachana na ulimbukeni wa kufanya gharama kubwa za harusi?

Tukio ambalo linachukua mamilioni halafu linafanyika within few hrs watu wanakula wanakunywa wanaondoka, bajeti ya milioni 9 baada ya honey moon maharusi wanayaanza maisha kwa taabu kulipa madeni n.k., kwanini Watanzania hatubadiliki?

Wazungu miaka ya nyuma walishapita humu wakabadilika miaka mingi ilopita karne hii wakihudhuria harusi zetu wanatushangaa na kutuona ni matajiri sana kumbe hamna kitu!

Kweli hatukatai wapo wanaojiweza kifedha wacha wafanye, lakini wenzangu na miye unajikamua unafanya sherehe kubwa na mnaendelea katika circle ya kuchangiana the whole year unajikuta unachangia harusi tu, sijui kama kuna wanaopiga hesabu ya hizo kadi familia iliochanga kwa mwaka na si kana kwamba ina mwisho, no, na mwaka ujao hivyo hivyo.

Tuamke Watanzania, tufanye harusi za gharama ndogo, kama ni swala la kuchangishana basi tuchangishane ada-fees-watoto wakasome vyuoni Malaysia, London na US, matunda yatakuja onekana. Wakenya wenzetu waliliona hili mapema, leo wengi ni maboss ktk nchi yetu wenyewe!

Tubadilike Watanzania! Harusi nacho ni chanzo cha kutiana umasikini!

Kwahyo huko Kenya hakuna harusi za hela nyingi?
 
Back
Top Bottom