Kweli harusi sasa zinazidi kututia umasikini

Kweli harusi sasa zinazidi kututia umasikini

Uzuri wa hii kitu uwe kwako pia hukuwachangisha wao wakikuletea unaweka kwenye dustbin hupati shida mie nilijikunja nikafanya simple hasa hivi wakileta nawapotezea, na hakuna wa kulalama sababu sina deni nao.
 
Bora umesema wenzako na wewe, waache wenye nazo wafanye wee unakereka nini? Ni siku haitajirudia kamwe wacha waenjoy to the fullest

Una uhakika kwamba haitajirudia, acha kutetea ujinga!. Akili za watanzania wengi haziko sawa, hiyo harusi bora ifanyike kwa wiki nzima kila siku. Hata mm znanikera sana, mil 20 mnakula siku moja tu. wa_Tz tunahitaji maombi sana
 
mimi nilishasema kabisa, kikubwa ni ndoa tu. ila msosi watu watakula ubwabwa hata kilo 200 na nyama na soda baaaaas kwisha, hata mil 1 haizidi kulisha watu wakashiba mpunga wakaenda zao, ila tarumbeta send off, kitchen part na utumbo mwingine NO!
na kwa nilivojaribu kufanya utafiti wangu kwa ndoa zilizofanya harusi za matarumbeta na mbembwe nyingi hua zina migogoro sana, ila ndoa za kimaskini nyingi naona zina dumu sana, sijui ni kwa nini
 
Me kuna mitaa huku sipiti kisa michango,imekuwa adhabu kabisa yaani kama deni vile
 
Hili nalo neno.Afadhali umeliona hili ndugu yangu.Ukweli ni kwamba ni ulimbukeni na kutojitambua.Mimi mwenzio nilishaachana na ujinga huo siku nyingi.Wasiojitambua ngoja waendelee,mimi nilishajitambua.
Huwa najiuliza mwisho wake lini Watanzania wa hali ya kati na chini kimaisha, hasa mijini, wataachana na ulimbukeni wa kufanya gharama kubwa za harusi?

Tukio ambalo linachukua mamilioni halafu linafanyika within few hrs watu wanakula wanakunywa wanaondoka, bajeti ya milioni 9 baada ya honey moon maharusi wanayaanza maisha kwa taabu kulipa madeni n.k., kwanini Watanzania hatubadiliki?

Wazungu miaka ya nyuma walishapita humu wakabadilika miaka mingi ilopita karne hii wakihudhuria harusi zetu wanatushangaa na kutuona ni matajiri sana kumbe hamna kitu!

Kweli hatukatai wapo wanaojiweza kifedha wacha wafanye, lakini wenzangu na miye unajikamua unafanya sherehe kubwa na mnaendelea katika circle ya kuchangiana the whole year unajikuta unachangia harusi tu, sijui kama kuna wanaopiga hesabu ya hizo kadi familia iliochanga kwa mwaka na si kana kwamba ina mwisho, no, na mwaka ujao hivyo hivyo.

Tuamke Watanzania, tufanye harusi za gharama ndogo, kama ni swala la kuchangishana basi tuchangishane ada-fees-watoto wakasome vyuoni Malaysia, London na US, matunda yatakuja onekana. Wakenya wenzetu waliliona hili mapema, leo wengi ni maboss ktk nchi yetu wenyewe!

Tubadilike Watanzania! Harusi nacho ni chanzo cha kutiana umasikini!
 
Kwa hiyo unafanya mwenyewe?

Feminine way of asking questions. YES, hata wewe unapaswa kufanya mwenyewe. Kitu cha kufanya kwa michango ya watu ni kama msiba au nyumba yako ikiezuliwa na kimbunga sababu hayo huna ghafla pasipo kuyatarajia.

Km swali lako lililenga kunikejeli wala sitajali, jamii yetu imejaa watu wasiotaka kufikiri.

Kujaza watu wasiokufahamu kwenye sherehe yako ya ndoa, kukodi ukumbi, magari ya kifahari na pilikapilika zingine ambazo zisizo na lazima havimzuii mwanaume **** ujauzito mke wake.

Ndoa ndio ya lazima, harusi jipime uwezo
 
mimi nilishasema kabisa, kikubwa ni ndoa tu. ila msosi watu watakula ubwabwa hata kilo 200 na nyama na soda baaaaas kwisha, hata mil 1 haizidi kulisha watu wakashiba mpunga wakaenda zao, ila tarumbeta send off, kitchen part na utumbo mwingine NO!
na kwa nilivojaribu kufanya utafiti wangu kwa ndoa zilizofanya harusi za matarumbeta na mbembwe nyingi hua zina migogoro sana, ila ndoa za kimaskini nyingi naona zina dumu sana, sijui ni kwa nini

Ningekuwa na dada ningalitamani aolewe na mwanaume wa kaliba yako. Mtu mtimilifu na rijali wa maisha huwa anavyo vipaumbele kwenye maisha.

Vijana wa leo akili wanashikiwa. Ukiona unajimudu kulisha pilau watu 25-50, kununua gauni la mkeo na suruali yako, basi unajimudu kufanya sherehe. Waalike nyumbani, wenye utimamu wa akili watakuja, wanaodhani kuwa ndoa ni ukumbi na watabaki majumbani kwao, lkn hawatakuzuia kuishi kwa raha na mkeo
 
Bora umesema wenzako na wewe, waache wenye nazo wafanye wee unakereka nini? Ni siku haitajirudia kamwe wacha waenjoy to the fullest

Huo msemo wa "siku haitojirudia" ndipo ujinga ulipo lala.
 
Mi nishagombana sana na ndugu kuhusu hiki suala na ninaonekana mtu tofauti nisiependa ushirikiano.
Lkn huo ndo ukweli haina haja ya kutuchangisha mamilioni kwa ajili ya shereh ya siku moja.
Ndoa ishafungwa c waende wakapumzike kula kunywa yatuhusu nn tena
 
Kama hujachangisha mtu kwa harusi yako unakuwa na kiburi cha kutokuchangia mtu yeyote.
Lkn km harusi yako ulichangiwa unakuwa mtumwa wa wale waliokuchangia.
Simama mwenyewe mwanaume jitetee
 
Feminine way of asking questions. YES, hata wewe unapaswa kufanya mwenyewe. Kitu cha kufanya kwa michango ya watu ni kama msiba au nyumba yako ikiezuliwa na kimbunga sababu hayo huna ghafla pasipo kuyatarajia.

Km swali lako lililenga kunikejeli wala sitajali, jamii yetu imejaa watu wasiotaka kufikiri.

Kujaza watu wasiokufahamu kwenye sherehe yako ya ndoa, kukodi ukumbi, magari ya kifahari na pilikapilika zingine ambazo zisizo na lazima havimzuii mwanaume **** ujauzito mke wake.

Ndoa ndio ya lazima, harusi jipime uwezo

Mkuu huwa unapoint lakini uwasilishaji wa point zako ndio tatizo!
Binafsi kukuuliza hilo swali nilitaka kujua mtazamo wako upo vipi, labda kuna kitu nawezajifunza kutoka kwako!

Anyways nimekuelewa, ahsante!
 
Michango ya harusi wanawake ndani ya nyumba hugeuka maajent. Kila siku swali kwa mume ni kuulizwa kama mchango kwa fulani umeshalipa. Kina mama nia kubwa ni kwenda kuoneshana vito na mavazi! Na gharama zipo kwenye muda wa vikao, nauli na zawadi. Kwa mwaka familia zetu hutumia hela nyingi kwa harusi huku tuko nyumba za kupanga.
 
Upo sawa kabisa.

Wanawake ndio wanaopokea kadi na wanaomshawishi mwanaume alipe.
 
Back
Top Bottom