Kweli harusi sasa zinazidi kututia umasikini

Kweli harusi sasa zinazidi kututia umasikini

ibanezafrica

JF-Expert Member
Joined
Oct 23, 2014
Posts
7,261
Reaction score
6,556
Huwa najiuliza mwisho wake lini Watanzania wa hali ya kati na chini kimaisha, hasa mijini, wataachana na ulimbukeni wa kufanya gharama kubwa za harusi?

Tukio ambalo linachukua mamilioni halafu linafanyika within few hrs watu wanakula wanakunywa wanaondoka, bajeti ya milioni 9 baada ya honey moon maharusi wanayaanza maisha kwa taabu kulipa madeni n.k., kwanini Watanzania hatubadiliki?

Wazungu miaka ya nyuma walishapita humu wakabadilika miaka mingi ilopita karne hii wakihudhuria harusi zetu wanatushangaa na kutuona ni matajiri sana kumbe hamna kitu!

Kweli hatukatai wapo wanaojiweza kifedha wacha wafanye, lakini wenzangu na miye unajikamua unafanya sherehe kubwa na mnaendelea katika circle ya kuchangiana the whole year unajikuta unachangia harusi tu, sijui kama kuna wanaopiga hesabu ya hizo kadi familia iliochanga kwa mwaka na si kana kwamba ina mwisho, no, na mwaka ujao hivyo hivyo.

Tuamke Watanzania, tufanye harusi za gharama ndogo, kama ni swala la kuchangishana basi tuchangishane ada-fees-watoto wakasome vyuoni Malaysia, London na US, matunda yatakuja onekana. Wakenya wenzetu waliliona hili mapema, leo wengi ni maboss ktk nchi yetu wenyewe!

Tubadilike Watanzania! Harusi nacho ni chanzo cha kutiana umasikini!
 
Hakuna haja ya kufanya harusi.cha msingi ndoa! Upo nyumba ya kupanga unatumia millions kadhaaa.ukachangiwa ujue unadaiwa
 
Mi muda mwingine huwa nachoka mana kuna baadhi ya watu wakikupa kadi zao utajuta kwan wanakuwa kero.
 
Nishaachana kitambo na kupokea kadi za harusi. Ukipokea tu basi lishakuwa deni.
 
harusi za matarumbeta zimekuja kwa kasi kubwa yani kumbe ni ulimbukeni tu utasikia mtu kasha choka anajidai nilifunga harusi bajeti yake milion 20 .bora uswahili kidogo saiv wao nawo wanaowana kiutani utani tu hakuna kuchangishana wala nini mnafungiwa mziki wa kigodoro apo imetoka mpyaa iyo ndoa tayari mshasherekea
 
Bora umesema wenzako na wewe, waache wenye nazo wafanye wee unakereka nini? Ni siku haitajirudia kamwe wacha waenjoy to the fullest
 
Bora kwetu Uswazi tunaweka kitu cha kigodoro tu night nzima asubuhi chai maandazi.Harusi imeisha.
 
siku hizi hakuna harusi kuna maigizo ebu fikiria hata wenye mimba nao wanavaa shela waliokwisha zaa nao hivyohivyo wasiokua bikra nao hivyohivyo yaani ni tabu tupu
 
Bora umesema wenzako na wewe, waache wenye nazo wafanye wee unakereka nini? Ni siku haitajirudia kamwe wacha waenjoy to the fullest


Ndivyo hivi mnavyojazana ujinga?

Eti siku haitajirudia wakati huna asset yeyote ya maana?

Acheni huo ulimbukeni.
 
Mwingine mawasiliano ni wakat huo ana shida ya kuoa tu,let say mlimaliza chuo 5yrs ago,hamkua mnawasiliana ila linapokuja suala la kuoa basi hapo sms na calls haziishi,akishaoa mawasiliano yanakufa tena,

Umeonaee, mimi yamenikuta hayo miaka chungu nzima mtu yupo kimya, hata aibu haoni mwee!!!.
 
Huu uzi vijana wausome kwa umakini! Una busara nyingi za manufaa.
 
Back
Top Bottom