Kweli airtel yatosha.

Imany John

Verified Member
Jul 30, 2011
2,912
2,000
Híi kampuni ni mteja wao wa siku nyingi toka enzi za CELTEL. Kuna tatizo ambalo linawakumba wateja wengi (ikiwemo na mimi) la kutopata menyu yao ya "airtel yatosha" .

Nimejaribu kwa nguvu zangu kuwasiliana na huduma kwa wateja wanachosema ni kwamba,tatizo linajulikana na wanalishughulikia, je nikweli wanashugulikia tatizo zaidi ya wiki tatu sasa?

Kila ukibonyeza zile code zao za kujiunga kushuhudia mabadiliko wayasemayo nakutana na ujumbe huu.." huduma hii haipatikani kwa sasa,jaribu tena baadaye".

Hao wataalamu wanafanya nini maofisini?wateja tunafanya jitiada za mwisho hivi kuwakimbia. Rekebisheni kasoro zenu.
 

Blac kid

JF-Expert Member
Apr 1, 2012
5,551
2,000
Tatizo jingine lipo kwenye tafadhali nipigie ni bora wangesema tu kwamba washaifuta!!
 

kenwood

JF-Expert Member
Nov 29, 2013
757
195
Nadhani washaifuta au wanataka kuifuta sasa wanaangalia upepo unakwendaje.
Mimi niliwauliza customer care wakasema kuna tatizo wanalishughulikia na wakaniambia kuna watu wanapata wengine hawapati sasa sijui ni kweli au uwongo, wanaopata mtujuze mnafanyeje au ndiyo mambo ya akufukuzae hakwambii . . .
 

snipa

JF-Expert Member
Dec 10, 2013
4,136
2,000
menu yao *100#
nikajifanya mjanja kuchange language, niweke kizungu,
.
Mpaka kesho hyo menu siipati
.
.
 

Kakakuona

JF-Expert Member
Nov 15, 2013
361
250
Yani mimi huwa naomba igome tena na tena ikija kukubali najikuta na bundle zaidi ya ilivyotakiwa,kujua kama umepata zaidi unatuma txt '' salio'' kwenda15444
 

Imany John

Verified Member
Jul 30, 2011
2,912
2,000
labda eneo ulipo cjawahi kutana nabhilo

Nimetoka kuwapigia huduma kwa wateja muda huu,wamepokea wakawa hawaangaiki na mimi then baada ya muda wajakata,nikawapigia wakapokea na mhudumu anajifanya hanisikii. Akakata naye. Huu ni uhuni, mimi na wiki ya 3 sipati menyu ya yatosha.
 

Imany John

Verified Member
Jul 30, 2011
2,912
2,000
Nadhani washaifuta au wanataka kuifuta sasa wanaangalia upepo unakwendaje.
Mimi niliwauliza customer care wakasema kuna tatizo wanalishughulikia na wakaniambia kuna watu wanapata wengine hawapati sasa sijui ni kweli au uwongo, wanaopata mtujuze mnafanyeje au ndiyo mambo ya akufukuzae hakwambii . . .

Naungana na wewe,yani ukweli mtupu usemayo. Wanatuibia sana.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom