Kwasababu CCM wanapenda uongo na magoli ya mikono, COVID-19 haipendi uongo itawaondoa madarakani!

Sema ndugu zako wamekufa wangapi na hawajatangazwa au wanaumwa na sio kila siku kuwasemea watu ambao hawajulikani walipo, na kama wapo acha waseme wenyewe kuwa ndugu zao wanakufa ila hawatangazwi, na sio wewe, maana huna ushahidi, na kama unao weka hapa tuuone.
Kwani watanzania wenzako siyo ndugu na hauwajali? Kwa taarifa yako, model hii inayofuatwa, lazima ukufikie. We endeleza kejeli.
 
Kuna watu wanajipa stress za kujitakia tu yani wanamchukia mtu ambaye hawawezi kumfanya kitu.
Hakuna anayemchukia pasipo na sababu. Kwa namna ambavyo vilio vya Watanzania vimepamba moto kona zote za nchi, mwambieni nduli makufuli asitoke kabisa huko chato. Siku atakapojaribu kutoka tu, corona itaondoka naye fasta.
 
Hakuna anayemchukia pasipo na sababu. Kwa namna ambavyo vilio vya Watanzania vimepamba moto kona zote za nchi, mwambieni nduli makufuli asitoke kabisa huko chato. Siku atakapojaribu kutoka tu, corona itaondoka naye fasta.
Tatizo sio sababu hakuna kisicho na sababu ila tatizo unampomchukia mtu ile kupitiliza yani umemtilia X kabisa halafu huyo mtu mwenyewe huwezi kumfanya kitu hapo ndipo stress zinapo wapata watu,kuna watu unaona kabisa hawapo sawa.
 
Mkuu kwanini unasahau kuwa nchi hii ina watu zaidi ya milioni 55? Unadhani miaka yote watu hawa wataendelea kupelekeshwa na kikundi cha watu wasiozidi milioni kumi kinachoitwa ccm? Wanao shiriki maigizo yenu ya uchaguzi ni wajinga wenzenu wanaccm na wanachama na mashabiki wachache wa vyama ambao jumla yao hata haifiki 20 milioni sasa tell me hawa wengine zaidi ya milioni 40 wako wapi na wanafikiria Nini kuhusu siasa uchwara mnazoendesha hapa Tanzania
CHADEMA kwa sasa hivi wanachama wake wamepukutika na ni nadra kufika laki nne Tanzania nzima! Kama unabisha tumia statistics za viongozi wa CHADEMA waliohama.
 
Sasa nchi yetu uchumi kwanza corona iwepo tu maana mpaka Sasa hamna mipango yoyote ya kuokoa uchumi hasa kipindi hichi Cha corona I thought juzi Mr. President angeongelea hatua gani ambazo wamejiandaa ili ku boost uchumi, hasa sector binafsi ambayo imepata madhara, utalii ambao ni chanzo Kikuu Cha mapato na feza za kigeni, maana hatuna lockdown Ila vitu na biashara nyingi zimepata madhara.

Pia serikali nayo hatua za kudhibiti guidelines ni Kama imepuuza guidelines za WHO Sasa huku nchi nyingine zikifanikiwa kudhibiti corona sisi si ndo tutapigwa stop kabisa Mana tutaonekana ni supplier wacorona, nafikiria serikali ifikirie future zaidi, maana serikali watenda maamuzi akili zimegoma wanawaza uchaguzi mkuu zaidi, kuliko hata kudhibiti hii corona.

Sent using Jamii Forums mobile app
Nyinyi uchaguzi mmeisha kata tamaa? Basi jipange 2025.
 
Wale waliokuwa hawaamini kuwa ccm ni waongo, wale waliobakia, wengine wanalalamika ndugu zao kuzikwa na huku taarifa ni watu kumi tu ccm wametoa.
Muda si mrefu tunaendakuongoe lugha moja.....sidhani kua wanaccm wanaweza kufika hata 10% watakaompigia kura magufuli...THE FAILED AND INCOMPETENT PRESIDENT
 
Tatizo sio sababu hakuna kisicho na sababu ila tatizo unampomchukia mtu ile kupitiliza yani umemtilia X kabisa halafu huyo mtu mwenyewe huwezi kumfanya kitu hapo ndipo stress zinapo wapata watu,kuna watu unaona kabisa hawapo sawa.
Mkuu mtu ambaye haoni huyu mtu alivyofanya damage kubwa kwenye nchi hii,mtu ambaye haoni huyu mtu alivyovunja na kusambaratisha protocol za nchi hii,mtu ambaye haoni kiwango cha double standards alizoasisi mtu huyu,mtu ambaye haoni mtu huyu alivyosusha morali ya watu wengi kulitumikia taifa hili,mtu ambaye haoni mtu huyu alivyoharibu sector ya utumishi wa umma,mtu ambaye haoni mtu huyu alivyoharibu sector ya kilimo ya nchi hii hususani mazao ya biashara Kama korosho,kahawa na tumbaku,mtu ambaye haoni mtu huyu alivyoharibu sector ya fedha Tanzania,mtu ambaye haoni mtu huyu alivyoharibu sector binafsi ya nchi hii,mtu ambaye haoni mtu huyu alivyoasasi ufujaji wa pesa ya umma kwa kiwango cha SGR,mtu ambaye haoni uhovuo wa namna mtu huyu anavyoshughulikia majanga yanayoishia kugharimu maisha ya watanzania,mtu ambaye haoni mtu huyu alivyoharibu mahusiano ya nchi yetu na nchi mbalimbali na mashirika ya kimataifa,mtu ambaye haoni mtu huyu alivyoharibu mshikamano na utengamano miongoni mwa watanzania mtu huyo Kama si agent wa shetani ni nani basi
 
Back
Top Bottom