Madeleka: Serikali itakuwa inasema uongo wananchi hawajahi kutoa maoni kuhusu Mikataba ya HGA

brazaj

JF-Expert Member
Jul 26, 2016
27,882
35,900
Mapambano na CCM hayataki lelemama. Ni Kwa maneno, mwonekano au vitendo? Hakupaswi kuwapo shaka popote.

"Ni Mwabukusi, Mdude, Madeleka, Lissu, Slaa, Mwamakula, Ponda, au wa namma hiyo?"

Wapi lugha zao zikabadilika? Wapi wasiwepo kwenye mstari wa moto? Wapi wakatishika? Wapi wakaghairi kwenye wanachokiamini? Au wapi wakaishiwa hoja?

"Ama kwa hakika walipo tupo."

Aluta continua!

====

"Wekeni hiyo mikataba wazi, na muiweke leo sio kesho. Ili haya yaliyoandikwa na mnayotaka tuyaamini tuweze kuyaona wote kwa mamcho.

"Kama serikali inasema ilizingatia maoni ya watu, serikali itakuwa inasema uongo kwa sababu wananchi wa Watanzania hawajawahi kutoa maoni yoyote kuhusu mikataba ya HGA kwasababu haipo, ndio imesainiwa juzi, sasa hayo maoni wameyatoa wapi? Wananachi walikuwa wanatoa maoni kuhusu IGA, kwahiyo kama maoni yamezingatiwa hayo maoni yatakuwa ni kuhusu IGA, na kama yamezingatiwa kweli tuonyeshwe mkataba mpya wa IGA uliosaniwa ukiwa na hayo maoni ya hao wananchi.

"...Lakini mkiisoma IGA, DP World ametafsiriwa tu kama kampuni inayotoka Dubai inayomilikiwa na serikali ya Dubai, lakini hakuna kokote DP World imetajwa kwenye mkataba kama mwakilishi wa serilikali ya Dubai kwenye uendeshaji wa shughuli za bandari za tanzania. Hana mamlaka yoyote na wala serikali ya Dubai haimjui.

"Na ndio maana aliyesaini mkataba kwa niaba ya serikali ya Dubai kuhusiana na mkataba wa IGA ni Chief Executive Officer of the Ports Customs and Free Zones Cooperation, sio hata DP World. Yaani DP World anachomekwa chomekwa katika mazingira ambayo hata kesho kutwa likitokea la kutokea hamuwezi kumuwajibisha.

"Mkataba unazibana pande mbili zilizosaini, DP World haijasaini na hii ndio katiba ya uwekezaji pale bandarini.

"Kwahiyo ituambie huyu DP World ni nani, ni akaina nani hawa DP World?"
 
WeHuyo mjinaga tu na anafahamu wajinga ndiyo waliwao.

Haelewi hata anaongea nini, anafoka foka tu.

Tulizana. Hili si la vyama tena. Hili ni la watanzania. Tulikosa kuwapa ujemedari wa vita wa namna hii:

a) Kwenye katiba mpya na bandari: Atataka katiba mpya sasa. Biashara ya bandari haipo, sasa na hata milele.
b). Atasimama na wananchi siku zote.
c). Huyu si kigeugeu. Agenda za wananchi kwake ni za kudumu.
d). Akiitisha maandamano atakuwapo mstari wa mbele. Yuko tayari kufa au hata kufungwa badala au kwa niaba ya wananchi wake.
e) Siyo mnafki, ni muwazi na anachosema au ukimwangalia, (usoni) ana maanisha.
f) Ni kipenzi cha watu.
g) Hushawishi kwa nguvu za hoja si kwa hoja za nguvu.
h) Huyu huwa na wafuasi wa dhati, siyo wafuasi wa kulipwa (chawa). Hoja zake zajiuza. Hahitaji kukingiwa kifua.
I) Amedhamiria. Lugha yake, adui huielewa Kwa ukamilifu wake.

Habari zimfikie mama Abduli na vibaraka wake. Na bado:

F9RnspRX0AAbCPK.jpeg
 
View attachment 2792476
Sayansi ipi ya PCM, PCB au Computer Science au Political Science. Mtakuwa zaidi ya comedy

Sent from my Infinix X656 using JamiiForums mobile app
 
Mapambano na CCM hayataki lelemama. Ni Kwa maneno, mwonekano au vitendo? Hakupaswi kuwapo shaka popote.

"Ni Mwabukusi, Mdude, Madeleka, Lissu, Slaa, Mwamakula, Ponda, au wa namma hiyo?"

Wapi lugha zao zikabadilika? Wapi wasiwepo kwenye mstari wa moto? Wapi wakatishika? Wapi wakaghairi kwenye wanachokiamini? Au wapi wakaishiwa hoja?

"Ama kwa hakika walipo tupo."

Aluta continua!

====

"Wekeni hiyo mikataba wazi, na muiweke leo sio kesho. Ili haya yaliyoandikwa na mnayotaka tuyaamini tuweze kuyaona wote kwa mamcho.

"Kama serikali inasema ilizingatia maoni ya watu, serikali itakuwa inasema uongo kwa sababu wananchi wa Watanzania hawajawahi kutoa maoni yoyote kuhusu mikataba ya HGA kwasababu haipo, ndio imesainiwa juzi, sasa hayo maoni wameyatoa wapi? Wananachi walikuwa wanatoa maoni kuhusu IGA, kwahiyo kama maoni yamezingatiwa hayo maoni yatakuwa ni kuhusu IGA, na kama yamezingatiwa kweli tuonyeshwe mkataba mpya wa IGA uliosaniwa ukiwa na hayo maoni ya hao wananchi.

"...Lakini mkiisoma IGA, DP World ametafsiriwa tu kama kampuni inayotoka Dubai inayomilikiwa na serikali ya Dubai, lakini hakuna kokote DP World imetajwa kwenye mkataba kama mwakilishi wa serilikali ya Dubai kwenye uendeshaji wa shughuli za bandari za tanzania. Hana mamlaka yoyote na wala serikali ya Dubai haimjui.

"Na ndio maana aliyesaini mkataba kwa niaba ya serikali ya Dubai kuhusiana na mkataba wa IGA ni Chief Executive Officer of the Ports Customs and Free Zones Cooperation, sio hata DP World. Yaani DP World anachomekwa chomekwa katika mazingira ambayo hata kesho kutwa likitokea la kutokea hamuwezi kumuwajibisha.

"Mkataba unazibana pande mbili zilizosaini, DP World haijasaini na hii ndio katiba ya uwekezaji pale bandarini.

"Kwahiyo ituambie huyu DP World ni nani, ni akaina nani hawa DP World?"
Msitupotezee muda, hiyo hoja imekwisha. DP WORLD anaanza kazi tarehe 1 Novemba. 2023. Huo ndiyo mwisho wa mirija yenu ya wizi.

Kama Madeleka na wenzio hamna kazi ya kufanya shauri yenu, lakini watanzania tunataka kuona efficiency ya TPA ikipanda na makusanyo ya TRA yakiongezeka, period.
 
Tulizana. Hili si la vyama tena. Hili ni la watanzania. Tulikosa kuwapa ujemedari wa vita wa namna hii:

a) Kwenye katiba mpya na bandari: Atataka katiba mpya sasa. Biashara ya bandari haipo, sasa na hata milele.
b). Atasimama na wananchi siku zote.
c). Huyu si kigeugeu. Agenda za wananchi kwake ni za kudumu.
d). Akiitisha maandamano atakuwapo mstari wa mbele. Yuko tayari kufa au hata kufungwa badala au kwa niaba ya wananchi wake.
e) Siyo mnafki, ni muwazi na anachosema au ukimwangalia, (usoni) ana maanisha.
f) Ni kipenzi cha watu.
g) Hushawishi kwa nguvu za hoja si kwa hoja za nguvu.
h) Huyu huwa na wafuasi wa dhati, siyo wafuasi wa kulipwa (chawa). Hoja zake zajiuza. Hahitaji kukingiwa kifua.
I) Amedhamiria. Lugha yake, adui huielewa Kwa ukamilifu wake.

Habari zimfikie mama Abduli na vibaraka wake. Na bado:

View attachment 2792476
Imekwisha hiyo. Hakuna sisimizi yeyote wala panzi atakayefanya maandamano. Tafuteni hoja ngingine
 
Uongo wananchi walitoa maoni yao kwa Viongozi wa Dini baada ya kuona wabunge hopeless kabisa hawakutaka kuchukua maoni ya wananchi wakawa tu wanaongea yao ambayo hawakupewa na wanancni

Asante Kanisa katoliki kwa kupokea maoni ya wananchi na kuyawawakilisha ipasavyo

Hata Mihimili mitatu yote ikileta za kuleta kwa collusion wananchi endeleeni kukimbilia kwa Viongozi wa dini

Hii nchi sio yao tu hao Mihimili mitatu
 
Nani kakwambia kuna suala moja? Katiba mpya imepatikana?

F. KATIBA MPYA

Katiba yetu ya sasa ni ya CCM ni katiba ya chama kimoja, Katiba Itapatikana kwa njia moja tu, Lazima kutumia nguvu ya umma, Hakuna njia nyingine, Tunatakiwa kwenda nchi nzima kushinikiza Nguvu ya umma pekee ndio itatupatia katiba sio vingivyo.

Hotuba ya Lissu Marekani - Part B

Habari ndiyo hiyo.
 
Kwani mheshimiwa paroko si anasema haya kuhusu TEC?

Baraza la Maaskofu Katoliki (TEC): Bado hatuungi mkono Mkataba wa Bandari

Au CCM mna TEC yenu?
 
Muongo kapost vilivyopitwa na wakati hilo tamko lilikuwa kabla wakati waraka unasomwa na serikali kabla kuzingatia ushauri wa maaskofu

Kuhusu hao wajomba zetu ngoma bado mbichi:

Mkataba wa DP World na TPA (HGA) umevusha sheria ya mwaka 2017 ulinzi wa maliasili inakataa kuingia mkataba kabla ya kupelekwa bunge.

Hotuba ya Lissu Marekani - Part B

Habari ndiyo hiyo.
 
Nani kakwambia kuna suala moja? Katiba mpya imepatikana?

F. KATIBA MPYA

Katiba yetu ya sasa ni ya CCM ni katiba ya chama kimoja, Katiba Itapatikana kwa njia moja tu, Lazima kutumia nguvu ya umma, Hakuna njia nyingine, Tunatakiwa kwenda nchi nzima kushinikiza Nguvu ya umma pekee ndio itatupatia katiba sio vingivyo.

Hotuba ya Lissu Marekani - Part B

Habari ndiyo hiyo.
Nani kakuambia kuwa Katiba Mpya hatupati? Serikali imeanza na elimu kwanza.

Kenya wana Katiba Mpya lakini bado uchaguzi ukiisha Raila Odinga anakataa
 
Back
Top Bottom