Kwanini Zito yupo kimya sakata la uvunjwaji Katiba lilifanywa na Spika kupitia wabunge 19 wasio na chama?

kifupi kirefu

JF-Expert Member
Oct 29, 2018
539
3,507
Zitto ni mwepesi sana kutetea na kukosoa uvunjwaji wa Katiba. Ni mchambuzi wa siasa na hoja za maendeleo, Ni mchambuzi wa masuala ya uchumi.

Suala la akina mdee linagusa engo zote ambazo Zitto ni mbobezi Kama ifuatavyo;
Kwanza, linakosa usimamizi na utetezi wa kisiasa kwa sababu mfumo wa nchi umejengwa kwa wanasiasa kuwa wanachama wa vyama vya siasa kwa kuzingatia Katiba ya nchi, sheria za vyama vya siasa pamoja na Katiba za vyama vya siasa. Hawa wabunge 19 hawana chama Cha siasa kwa mujibu wa Katiba

Pili, Wapo bungeni kinyume kabisa na Katiba ya nchi kwa sababu hawakupitishwa na chama Cha siasa na hata baada yakuapishwa walivuliwa uanachama kwa mujibu wa sheria. Wamevunja Katiba ya nchi na katiba na taratibu za kibunge

Tatu, hawakupitishwa kihalali na tume ya uchaguzi kwa sababu tume upokea majina kutoka kwenye chama Cha siasa. Haikufanyika hivyo na tume haijawahi kutoa ushahidi wa wahusika kuteuliwa na chama Cha siasa

Nne, watu Hawa wanalipwa mishahara na posho hewa. Si wabunge lakini wanalipwa Kama wabunge. Hapa nilitegemea Zito ajadili kuhusu ubadhirifu wa Mali za umma lakini yupo kimya

Tano, Bunge limejiwekea utaratibu wa kuingiza watu bungeni wakianza na yule Mbunge wa Mtwara aliyefukuzwa Chadema akakosa sifa ya ubunge lakini akiwa zake nyumbani Spika akamwita na kumwambie aendelee kuwa Mbunge nakumlipa maslahi yote ya kibunge kinyume na sheria, hapa Zitto anasemaje

Kwa discripacy hizi najiuliza kwanini hii hoja siyo yamsingi kwa Zitto? Au anasubiri awasajili? Au atapiga kelele akitendewa wa chama chake?
 
ZITTO HUJIHUSISHA NA MASUALA YENYE MASLAHI KWAKE BIINAFSI.!!! KUNA MARAFIKI ZAKE WA SIKU NYINGI KATI YA WALE MACOVID KWAHIYO USITEGEMEE KUMSIKIA.
 
Mkuu Mama Samia aliposema anakusudia kukutana na vyama siasa alimaanisha CHADEMA na CHAUMA wazee Ubwabwa peke yao

Kwa maana anataka kuonana na MBOWE, LISSU, MNYIKA na HASHIM RUNGWE

Hao wengine ni walewale MATAGA waunga juhudi tu kama MATAGA wengine wa LUMUMBA
 
Back
Top Bottom