Hacha kupotosha chief, issue ya kodi aina mausiano yoyte na umri wa nchi,
Hapa tunachotakiwa kusema ni mifumo mibovu ya uendeshaji nchi, na siyo swala nchi gani kongwe na nyingine syo kongwe,
Nadhani ukifikiri kwa makini utaelewa maana ya MUDA.
Taifa lina karne 15 za kujijenga na kutengeneza misingi imara ya kijamii, kiutamaduni, kisiasa, kiuchumi, (ikiwemo mifumo ya kodi)nk.
Kabla sisi hatujapata uhuru wao tayari walikuwa:
Walishajitawala kwa miaka. 1500;
Wamefuta ujinga 100%
Wamesambaza maji 100%
Umeme 100%
Huduma za afya.
Reli Barabara Bandari viwanja vya ndege100%
Wanamaendeleo makubwa ya sayansi na teknolojia na mapinduzi ya viwanda.
Uchumi mkubwa (wanauza magari ya SCANIA dunia nzima). Aidha makampuni yao makubwa yenye mamia ya miaka yametapakaa Dunia nzima kupitia mifumo ya hisa na hivo mirija hiyo inafyonza utajiri toka duniaani kote.
Kifupi walikuwa wameweka miundo ya kijamii na kiuchumi ambayo multiplier effect yake ni kutengeneza mifumo ya ajira na kujiajiri na kuimarisha biashara, kutoa mikopo na ruzuku hifadhi ya jamii na mafao kukosa ajira kwa wananchi.
Hizi ndio sababu wameweza kukusanya kodi kubwa sana.
Kwa mfano Sweden wana wigo mpana ukusanyaji kodi na wakusanya 43 ya ya GDP, ukija kwenye kodi ya mapato wanachukua mpaka 57% ya mshahara.. yaani kama unapokea milioni wanachukua takriban laki tano na na sabini. Wakati makusanyo yao ni makubwa bado hawahitaji kuongeza mashule..mahospitali.. mabarabara mareli viwanja vya ndege mabandari kufua umeme au chochote.
Je Umejiuliza hayo mapato ya kodi yanaenda wapi sasa!?
Bila shaka ni kutoa huduma bora na zingine bure kwa wananchi na kutoa misaada kwa mataifa masikini kama sisi.