Kwanini wenzetu Sweden wanapenda kulipa kodi?

Jidu La Mabambasi

JF-Expert Member
Oct 20, 2014
15,327
24,209
The Nordic Way - BBC Reel

Wananchi wenzetu huko Sweden wamefanikiwa kujenga a Welfare State.

Nchi ambako Shule ni bure hadi Chuo Kikuu, Matibabu ni bure, Usafiri na nyumba ni sawa na bure.

Wazazi wakijifungua matibabu na matunzo ni bure.

Nasema bure kwa maana kodi wananchi wanazotoa zinalipia huduma zote hizo.

Nimefika Sweden kwa hiyo najua haya ninayosema ni kweli.

Tanzania kodi zetu vipi?
 
Wenzetu kodi inayokusanywa inatumika kwa vizuri hata mwananchi anaridhika
Huku kodi utozwe, mazingira ya mwananchi mlipa kodi hayaboreshwi zaidi ya kodi hizo kuwanufaisha watu wachache
Ujanjajanja tu wa baadhi ya watu wanaosimamia
Fedha hizo kupiga tu
Ndomaana namba 1 kutwa kulia nao

Ova
 
Hivi unadhani vijana kuambiwa tujiajiri usidhani kwamba wanatupenda sana na kua wanatuonea huruma tukikaa bila kazi. Ila wanachowaza wao ni mjiajiri ili wawapige kodi na ushuru, na ndio maana miaka nenda rudi wafanya biashara wadogo wanalia mazingira mabovu lakini hayaboreshwi ila means za kukusanya mapato zinaboreshwa.
 
Tanzania wakati wa Nyerere elimu ilikuwa bure na matibabu bure na ajira bwerere tele serikalini na watu walikuwa wagumu kulipa kodi!! Hayo ya sweden tulishapita huko watanzania kwenye kodi vichwa ngumu
 
Nchi za wenzetu tu wana tax relief
Kwa walipa kodi,sisi ni mwendo wa kulipa tu
Kulipa tu

Ova
 
Kule ndio kuna Matibabu bure ya uhalisia na pia elimu ya juu bure hata hizo MD wanapata bure tu mradi umefikia vigezo sasa njoo huko kwingine unapoambiwa kodi kubwa sijui nini bure wakati ni changa la macho
 
Hapa bongo shida , wewe unaona ticket za electronic tu watu wanapinga, bado hujaenda duka la jirani anakuuzia mkate juu kwa juu, kodi itafikaje
 
Hii ngozi nyeusi wote Wezi, anayetakiwa kulipa anaogopa wanaopokea wataifuja tu, na Mtoaji siku zote anawaza jinsi ya kumpunja kama sio kukwepa kabisa.

Alafu pia sidhani hata kama tuna busara ya kukokotoa na kudai kodi, hivyo kutulinganisha na hao Wenzetu wenye misingi tofauti kabisa na huku ni sawa na kumuuliza Punda kwa nini hakimbii kama Farasi....atakuangalia tu.
 
Tanzania wakati wa Nyerere elimu ilikuwa bure na matibabu bure na ajira bwerere tele serikalini na watu walikuwa wagumu kulipa kodi!! Hayo ya sweden tulishapita huko watanzania kwenye kodi vichwa ngumu
Enzi hizo ndiyo tulikuwa tunaanza kuipandikiza Elimu ili elimu ituzalishie maisha bora,kwa hiyo ilikuwa rahisi zaidi kukusanya kodi miaka hiyo kuliko sasa,ila kodi yenyewe ndio ilikuwa hakuna!!

Sasa hivi kodi ipo kwa watu wasio na maisha bora,kwa hiyo nao wanatamani kuitumia hiyo hiyo hela(kodi)ili kuboresha maisha yao,na serikali nayo inapambana kufa na kupona kuichukua hiyo hela(kodi?) Ili kuitumia kwa mambo mengine,kwa hiyo hapa kila mmoja haridhiki na anachokitoa(mwananchi),huku mwingine haridiki na anachokipata(serikali) mwananchi anataka serikali imwezeshe huku serikali ikimtaka mwananchi aiwezeshe!! Ligi ndiyo ipo hapa!!
 
Back
Top Bottom