tuanzie kwny katiba Yao ipoje?pili tuje kwny mfumo wa maisha ya viongozi wao upoje manake huwezi kuwa na magari ya gharama af uwe na amani wananchi wako kunywa maji machafu
Kuna watu wachache waliokaririshwa mambo ya Katiba... Kwao Katiba ni muarobaini wa matatizo yote🤣🤣
Katiba ni sheri tu na ili ifanye kazi lazima kuwepo na mambo mengine muhimu zaidi japo huonekana kama madogomadogo sana.
QURAN NA BIBLIA ni katiba ya Mungu kwa wanadamu na wengi tunaamini juu ya usahihi wa Kariba hizi kila mtu kwa imani yake.
Lakini bado Biblia haijafanya watu wote waokoke au kuwa waumini wazuri. Hata Quran haijafanya hata nusu ya waumini kuwa Wachamungu.
Uzuri na ubora wa katiba utaonekana tu kama raia husika watakuwa mila desturi utamaduni na mtazamo chanya.
Ndio maana kuna watu hawajui Quran wala Biblia lakini ni wema mbele ya Mungu kabla ya Imani zao.
Tunahitaji kuelewa na sio kukariri kwamba kila tatizo suluhisho lake ni Katiba pekeesio
Hilo ndilo hasa tunapaswa kujifunza kutoka kwake,ni ujinga kujifunza kwa failure mwenzako,tuwaige waliofanikiwa,siyo waliofeli,asa
Mkuu inawezekana uko sahihi kwa mujibu wa historia.Lakini the fundamental issue sio "umri" wa nchi.Nadhani maadili ni muhimu zaidi,,zile core values kama taifa ni zipi? Kama uko tayari watu wafe ili upate madaraka maana yake kama huo ndo mwelekeo hata baada ya miaka 1000 hakuna mabadiliko ya maana yatatokea,kwahiyo kwangu maadilli ni muhimu zaidi.
Fundamental Resources kubwa moja wapo ni muda. Maadili ni sehemu ndogo tu ya Utamaduni ambao hugawanyika zaidi ktk mila na desturi.
Bila shaka utahitaji muda kujenga tamaduni ya jamii/taifa ikiwa ni pamoja na maadili unayosema. Tamaduni ni matokeo ya uzoefu ulipatikana ktk maisha ya jamii husika mpaka kufikia kukubaliana hiki sawa na hiki sio sawa.
Walikopita sweden kama taifa ni mbali sana wameuana wamepigana wao kwa wao na mataifa mengine pia.
Hata Marekani unayoiona leo ni matokeo ya maisha yao ambayo wamepitia kudhulumiana kunyanyasana kutawaliwa kupigana kuuana kuwekana utumwa na kubaguana. Na mpaka leo wamekuwa wakipambana kukubaliana kitaifa juu ya baadhi ya mambo ikiwemo ubaguzi..
Mambo yote hayo yanaamuliwa na UZOEFU ambao huwezi kuupata kama rasilimali UDA haijatumika.